Haya hatukuyategemea....! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya hatukuyategemea....!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by suley, Sep 3, 2010.

 1. s

  suley Member

  #1
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kulingana na makubaliano yaliyofikiwa baina ya tume ya uchaguzi(NEC) na vyama vya siasa ikiwemo kutunga sheria mpya juu ya matumizi ya fedha pamoja na taratibu zingine za kuendesha uchaguzi. Mimi na ndugu zangu watanzania,tulijazwa matumaini makubwa tukiwa tunasubiri kampeni za kistaarabu,kwa kuwa tuliamini kuwa amani na utulivu tulivyonavyo vinaweza kuharibiwa ikiwa tutafika mahala tukaanza kudharauliana,kukejeliana na kubezana,tukala yamini kuwa tutadumisha miiko hii na hivyo ndivyo ulivyo msingi wa makubaliano yetu kama WATANZANIA. Vyama vikasaini na kukubali kufuata kanuni na taratibu zilizoanishwa katika sheria na kanuni zinazolinda maadili mpaka siku ya mwisho ya uchaguzi na matokeo.
  Ni kana kwamba haya hayakufanyika.,ni siku chache tu tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi tumeanza kusikia yale yale ambayo tulikubaliana kuwa hatutayafanya. Wapo viongozi wa baadhi ya vyama vya siasa wamekuwa wakifanya kampeni chafu zinazolenga kubezana,kutukanana na kukejeliana. Hali hii imepelekea hata baadhi ya wafuasi na wa shabiki wa viongozi hawa kufuata nyayo zao kwa kuleta kashfa na matusi waziwazi.
  Hali hii inatupa picha gani sisi wananchi au zinatujenga wananchi katika hali gani,na je wale wanaoendesha siasa hizi chafu zenye kutumia lugha za kejeli,dharau na matusi yenye kupalilia dhana ya ubaguzi na yenye kueneza chuki wanakusudia nini..?
  Kama tutarejea katika dhima ya makubaliano yetu ilikuwa ni kufanikisha mchakato mzima wa kampeni na uchaguzi kwa amani na utulivu. Makubaliano haya yalilenga kuhakikisha kuwa watanzania wanabaki wamoja na kudumisha mshikano hata baada ya uchaguzi. Ila kwa haya ambayo yameanza kujitokeza yakiwemo yale ya kutukanana na hata kushambulia na kuzuriana kama kule ubungo na yale yaliyosemwa kuwa kinana ni mmoja wa al shabab. Kwa mwendo huu kamwe hatutafikia malengo yalioanishwa katika mkataba wa makubaliano na naona wazi kuwa tunakoelekea si kuzuli hata kidogo.
  Labda niwakumbushe watanzania wenzangu(wakiwemo viongozi wa kisiasa pamoja na wananchi) na pia niwausie kuwa tunatakiwa kusoma kutokana na makosa ya wenzetu na sio kusubiri tukosee kisha tuseme kuwa tunajifunza kutokana na makosa kwani kuna baadhi ya makosa yanatoa masomo yenye maumivu makali na kisha kuacha makovu ya milele. Yale ambayo tuliyaona Kenya,tunayaona Somalia,Congo,Siera leone,Angola na kadhalika,hayakutokea kwa bahati mbaya au si kwa muujiza bali kwa yale ambayo viongozi wao waliyasema na kuyafanya huku wao wakiyaunga mkono bila kujali athar zake kwao. Ni kwa maneno ya kijinga na ya kishenzi yasio na msingi wowote yenye kueneza chuki kama haya ambayo tumeanza kuyasikia na kuyashangilia ndio ambayo yaliwafikisha pale tunapowaona leo hii. Yote yaliyojiri yalianza kama hivi,ni cheche moja tu inatosha kuteketeza ghala.,ni cheche moja tu inageuza msitu kuwa jangwa. Ikiwa tutadharau na kupuuza kwa kusema ni maneno ya wajinga wachache tu na yasio na ushahidi wowote,tukumbuke kuwa uwongo ukishamili ugeuka kuwa ukweli na unakuwa haupingiki tena.
  Nimeandika haya kwa kutoa angalizo na kuwasihi wanasiasa kuepukana na jazba,uzushi na matusi , kisha kuwataka wadumu katika kufanya yale tunayoyategemea watanzania nayo ni kuona kuwa tunatunza na kulinda misingi ya amani,upendo,mshikamano tuliyonayo.
   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Hivi hii amani tunayohubiriwa kama ibada huwa inakuwa na umuhimu wakati wa uchaguzi tu? Kwa nini? Mimi nadhani ni hofu kwamba haki haitendeki katika uchaguzi na kuna siku moja watu watasema ... basi, liwalo na liwe. Hivi CCM wanawezaje kujidai wanajali amani wakati wametoa mafunzo kwa vijana wa UVCCM kwa madhumuni ya kufanya fujo wakati wa uchaguzi? Kambi kubwa ya mafunzo ilikuwa Iringa na Kikwete aliitembelea. Mafunzo hayo yameishaanza kutekelezwa kw vitendo Moshi na Iringa. Na huu ni mwanzo tu. Ngojeni tunavyokaribia Oktoba 31.
   
 3. s

  suley Member

  #3
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna mengi hayajaandikwa wala hayajasemwa lakini yapo ama yatakuwepo..,si lazima mtu akubali kuwa kuna moto wa jahannam,lakini jua likimuwakia ataanza kupata picha...,nakubaliana na wewe kuwa huo ni mwanzo tuu....!
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Yale yaliyotokea Kenya na Somalia hatimaye taratibu yamezaa Katiba Mpya Kenya!
  Hatuwezi kupata amani tunayoiotea ndoto kama hakuna equal rights/opportunities katika maisha!
  Mimi ndoto zangu zinaniambia kama CCM wangeacha ufisadi nchi hii ingekuwa ni pepo, na yote uyaonayo sasa katika kampeni usingaliyaona...Tungelikuwa kama nchi jirani ndogo ya RWANDA!
   
 5. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Si ndio hapo sasa, mimi bado nasema kuwa Kikwete anataka kuitumbukiza hii nchi kwenye vita. Na anafanya yote haya kwa makusudi kabisaaaaa.
   
 6. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #6
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Ukiona mwenzako ananyolewa, tia maji kichwani. Nani kasema amani haiwezi kupotea nchini kwetu? USIPIME! Wananchi wakiamua, hata yaje majeshi ya Obama, haitasaidia. Tusifike huko!
   
Loading...