Haya Gwajima

Bahati mbaya sana huwezi kumfahamu huyu Mungu kwa kuwa hujakubali awe Mungu wako. Ukikubali hata leo utaelewa maana ya Mungu wa Israeli, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka na Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

It doesn't make sense kabisa, yaani nimkubali kisha ndio nitamwelewa? Mimi huwa naelewa kwanza baadae ndio nakubali. Kama ndio mnafanya hivyo basi mnacheza rafu sana, yaani mtu amkubali Mungu wenu wa Israel kisha mumjaze ujinga kichwani?
 
It doesn't make sense kabisa, yaani nimkubali kisha ndio nitamwelewa? Mimi huwa naelewa kwanza baadae ndio nakubali. Kama ndio mnafanya hivyo basi mnacheza rafu sana, yaani mtu amkubali Mungu wenu wa Israel kisha mumjaze ujinga kichwani?

Umesikia sana habari zake lakini umekataa kumkubali. Nakushauri umkubali Bwana Yesu leo ndani ya moyo wako na haya mengine yote utayafahamu. Sema, BwanaYesu, mimi ni mwenye dhambi. Natubu dhambi zangu kwa kumaanisha kuziacha. Karibu moyoni mwangu unifanye kiumbe kipya. Futa jina langu katika vitabu vya hukumu na uliandike katika kitabu cha uzima. Asante kwa kuniokoa. Amen.
 

Sijakataa kusikia, lakini habari zenyewe zote ni ngumu kumeza. Watu mnajiaminisha tu kwasababu mmekosa mawazo endelevu na kuhoji possibilities za hadithi mnazopewa na maisha halisi. Mmekuwa kama mbwa mliopotezwa kwa miruzi, nyi mnakimbia tu wala hamjijui. Walioleta dini wenyewe wameketi kama mabosi nyinyi mnaendelea kuamini tu.
 

Hayo ni mawazo yako. Kazi yangu nimemaliza. Ndiyo maana nilikuambia umemkataa Mungu ukabisha.
 
Samahani kwa wale ambao nitakuwa nimewakosea...
Hivi hawa Manabii wa sasa watu hawajitambui kuwa TULISHAAMBIWA kuwa kutatokea manabii wa uongo?
Kuhusu kufufua km wangekuwa wanafufua kweli si wengi wangekuwa hai?
Pili wagonjwa si wengi wangekuwa hawaumwi, kwanza now ndio idadi ya wagonjwa imezidi kuwa kubwa kuliko awali.

Enzi za Bibi zetu watu walikuwa wema mbona manabii hawakuwepo sasa zama za uovu ndio kibaoo..

Pili kama wewe nabii kweli, hela unayoipata usingezitumia kujenga mijumba ya kifahari, kuendesha magari ya kifahari, ungetumia hela hizo kupeleka vituo vya watoto yatima, kuwasaidia wasiojiweza, kuwasaidia wagonjwa wapo masikini wengi saana Tanzania na nchi nyingine za Africa.

Hawa manabii wa sasa kila kukicha wanaibuka sababu washajua ukiwa nabii unapata hela...Woote wanatafuta ulaji..
Nabii gani anatembea na mke wa mtu....Nabii ni kiumbe safi kisichokuwa na dhambi...

Yaani hizi zama zimeharibika ila baadhi ya watu hawalitambui hili....Omba jiombee mwenyewe...Kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe...Sio wewe uombewe...Piga goti mwenyewe



 
mbona hawafufuliwi wale watu ambao tunawajua katika jamii, wanafufuliwa watu ambao hatuwajui?
 
Mungu anayetumwa na mungu, tena aliye part yake....na yet mnaclaim kuwa monotheists...SMH...what a concoction!!

Yesu, “ Mungu Mkuu na Mwokozi” (Tito 2:13), na anaelezea ya kuwa Yesu, “alikuwa katika hali ya Mungu” (Wafilipi 2:5-8). Mwandishi wa kitabu cha waebrania asema juu ya Yesu kuwa, “ Kiti chako cha enzi wewe Mungu, kitadumu milele na milele” (Waebrania 1:8). Yohana aeleza kuwa, “Hapo mwanzo kulikuwako neno, naye neno alikuwako kwa Mungu, naye neno (Yesu) alikuwa Mungu” (Yohana 1:1). Mifano ya aya zinazofundisha juu ya u Mungu wa Yesu ni mingi (pia Ufunuo wa Yohana 1:17; 2:8; 22:13; Wakorintho wa kwanza 10:4; Petro wa kwanza 2:6-8; Zaburi 18:2; 95:1; Petro wa kwanza 5:4; Waebrania 13:20), kila mojawapo ya aya hizi inatosha kukujulisha ya kwamba wanafunzi wa Yesu walimwamini kuwa Yesu alikuwa Mungu.
 
Je, unaamini kuwa Mungu ndie mwenye uwezo wa kufufua?

Je, unaamini kuwa unabii upo kutokana na 1 Corinthians chapter 12?

Je, unaamini kuwa uponyaji ni sehemu ya Ukristo na Mponyaji ni Yesu?

Je, unaamini kuwa YESU NI MUNGU MKUU?

Je, Mungu anaweza kuponya na kufufua watu?
 

Out of context
 
mbona hawafufuliwi wale watu ambao tunawajua katika jamii, wanafufuliwa watu ambao hatuwajui?
It is God's will na sio human will to raise the dead, refer to Lazarus exhibit, inter-alia, jaribu kusoma Biblia katika context yake na sio yako.
 
"Sijamwacha mume wangu sababu ya Gwajima na kweli bado napenda sana Mbasha lakini nampenda zaidi Mungu"


Wakati anazungumzia suala hili Flora ameweka wazi kuwa kwa sasa ni mjamzito na ujauzito huo ni wa Mume wake ambae ni Emmanuel Mbasha maana ameishi nae katika ndoa zaidi ya miaka kumi na katika kipindi chote hicho hajawahi hata siku moja kumsaliti Mumewe na kwenda kwenye michepuko hivyo huo ujauzito ni wa Mume wake Emmanuel Mbasha na siyo Gwajima.
 

Teh teh tee.. Kitanda hakizai haramu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…