Hay maker

Hay maker

CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2010
Posts
571
Reaction score
157
Wadau, habari zenu?
Mimi ni mjasiriamali chipukizi; mwenye malengo ya kuwekeza katika miradi ya Agribusiness (dairy & poultry projects - kwa uchache).

NAOMBA MSAADA WENU (HAJA YANGU ITATATULIWA WAPI/ NA NANI)?



Kutokana na uhaba wa nyasi na kupatikana maeneo ya mbali na mahali nilipofugia ng'ombe kwa sasa ninahitaji kifaa cha kukatia nyasi katika vipande vidogovidogo na kuvibana pamoja ili kuhifadhi nyasi kiasi kingi sana katika ujazo mdogo ili kuepuka kutumia nafasi kubwa katika kuhifadhi na kuepuka ubebeji wa mizigo kwa "trip" nyingi kwa gari; pia itanisaidia kuhakikisha nyasi zinazopotea na kukanyagwa na ng'ombe zinakuwa chache ili kuepuka kupoteza nyasi nyingi.



Kwa kifupi ninahitaji mashine inayofanya kazi kama mashine ya kusaga/ kukoboa nafaka ili niwe naweka nyasi ndani ya kinu halafu zinasagwa na kutoa vipande vidogovidogo na kuvipeleka katika mfumo mwingine ili vipande hivyo viweze kubanwa na kutengeneza vipande vinavyoweza kuhifadhiwa.


Ninahitaji mashine itakayokuwa inatumia umeme - umeme unaweza kuwa wa TANESCO, solar au wa mafuta.



Kama mnazo mashine za namna hiyo naomba mnijulishe, kama hamna, mnaweza kutengeneza kwa ajili yangu?

Nina ng'ombe wanane tu na ninawafugia ndani ya banda - eneo la Pugu Viwege/ Majohe.

NOTE: Miaka ijayo nina mpango wa kuweka miradi hii ya ng'ombe wa maziwa katika maeneo ya pembeni kidogo mwa mji (mashambani).



Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Wenu katika ujenzi wa Taifa.

 
Back
Top Bottom