mgombea uvccm2017
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 505
- 376
Nimeamua kumuombea mdogo wangu ushauri humu kwa sababu id anayotumia humu ni halisi hivyo hataki kujiexpose.
Iko hivi;
"Nina mpenzi wangu ni mchaga kwa kabila anasoma chuo(udaktari).
Huyu binti kwakweli nampenda na yeye ananipenda sana na ni mwaminifu!
Tatizo linalonipa shida ni kuwa hawezagi kuvumilia shida hata kidogo
Ikitokea hali ya uchumi ikayumba anakuwa mtu wa kulia tuu na kuwaza hata nimpe faraja kiasi gani hatulii ingawa hali hiyo hamfanyi awe na tamaa.
Mfano mwaka jana hali ya kiuchumi ya nyumbani kwao iliyumba sana hivyo hata pesa aliyokuwa anatumiwa na mzazi wake ilipungua kiwango kikubwa, akawa mtu wa kulialia kila wakati na kuwaza mpaka akakonda hapo ikabidi niingilie kati kumbeba kiuchumi.
Kwa sasa hali ya nyumbani kwao imetulia ila ya kwangu imeyumba kidogo ila cha kushangaza tena anakuwa mtu wa kulia machozi sana na kuwaza mpaka ameanza kupungua.Ukimuuliza sababu anasema hajazoea shida na anaumia hela anapokosa.
Nashindwa kuelewa huko mbele hata nilikimuoa na ikatokea maisha yakabadilika maana kuna kupata na kukosa maisha atayaweza kwa style yake hii ya vilio kila mara?
Naomba mchango wa mawazo yenu.