Keyboard_Warrior
JF-Expert Member
- Oct 10, 2015
- 6,361
- 11,192
Habari zenu wazalendo na wale wasiokuwa wazalendo!!?
Naamini mpo salama kabisa.
Sasa ipo hivi, vijana tunapenda sana mabadiliko.
Lakini pamoja na kuhitaji mabadiliko, hatuhitaji kuvuruga nchi yetu kupata mabadiliko hayo.
Hatuhitaji wanaharakati uchwara kutupeleka kwenye mabadiliko tunayoyahitaji, wanaharakati uchwara watatuharibia nchi yetu. Tunahitaji wanaharakati na wanasiasa wazalendo.
Kijana ambaye anaendesha maisha yake kwa kucheza kamari hatoshi kutuongoza kwenye mabadiliko tunayoyahitaji, kijana anayeongoza maisha yake kwa kucheza kamari atacheza kamari na maisha yetu.
Kijana ambaye yupo uhamishoni hatoshi kutuletea mabadiliko tunayoyahitaji, kwasababu hawezi kujali endapo taifa letu litavurugika.
Salamu ziwafikie, HAWATOSHI KUTUFANYA TUKAVURUGA TAIFA LETU.
Mabadiliko tunayoyataka yataletwa na watu wazalendo, mabadiliko tunayoyataka yataletwa na watu sahihi, mabadiliko tunayoyataka yataletwa na watu waliopo mahali sahihi, sio uhamishoni.