Hawapo romantic au huyu hanipendi tu?

mamamzungu

JF-Expert Member
Nov 17, 2019
873
1,021
Nimekuwa na mahusiano na kijana kwa mwaka 1 na miezi 10 ila sijawahi kupata yale mahaba yenyewe. Ukitoa zile siku za mwanzo ni za mahaba, ile miezi 3 ya mwanzo.

Mfano kukuita majina mazuri mazuri like sweetheart, honey, mke n.k Yaani kiufupi hana matendo ya mahaba.

Unaweza kumuaga kwenda mahali akakwambia sawa ila hakuulizi unaenda wapi na kufanya nini, kiufupi hana amshaamsha.

Anaweza kukaa hata siku 3 hamjawasiliana na akikutafuta hamna hata stori.

Mwenzenu nimechoka natamani kupata mtu ambaye ana mahaba na mimi nifurahie.

Mpaka nimekumbuka Ex wangu alikuwa ananiita majina matamu hata kama ananidanganya.

Naombeni majibu-
  1. Ni tabia ya wanaume wa Kichaga?
  2. Ni Tabia ya mtu binafsi?
  3. Hanipendi?
 

mamamzungu

JF-Expert Member
Nov 17, 2019
873
1,021
Wasikudanganye,

Wote tupo ivo ivo, bora uyo alijitahidi miezi mitatu.

Amna siamini

Kuna mmoja alikuwa ananihadaa sana hata Kama haniiti darling

Alikuwa anapenda kuniita mke wangu

Sasa huyu hata ukimwambia nakupenda kwenye sms anakujibu Asante Sanaa

Yaani ukiona katamka neno nakupenda ni kipindi mnagombana ndio atatamka au mkiwa pamojaa
 
22 Reactions
Reply
Top Bottom