Habari zenu wana mmu.
Lipo neno la kiswahili lenye nguvu nyingi sana litumiwapo lakini
kuna watu hawajui kulitumia. Niwape mandhari.
Siku moja najiandaa kwenda matembezini nafungua geti niishie zangu ghafla
akatokeza mdada fulani tunayefahamiana. Alikuwa amevaa gauni la kitambaa chenye
michoro mizuri sana na gauni kwa kweli lilimpendeza mno kwenye umbo lake la kuvutiwa.
Nikajikuta namwambia: Aisee Glory, umependeza sana. Alitabasamu, na kutoa maneno ambayo sikuyatarajia.
Aliniambia: "Kwa nini?" Hapo nikaishiwa nguvu nikarudia tena, "Umependeza sana"
Nimeshasifia watu kadhaa mchanganyiko, waume kwa wanawake na wananishangaza sana pale
wanaposhindwa kutamka neno moja tu, 'asante' badala yake wanataka maelezo kwa kuuliza
'Kwa nini?' Wananiudhije?
Umeshakutana na watu wasiojua kusema 'asante?' unapowasifia?