Hawajui kutumia hili neno. Wananiudhi!

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,257
Habari zenu wana MMU,

Lipo neno la kiswahili lenye nguvu nyingi sana litumiwapo lakini
kuna watu hawajui kulitumia. Niwape mandhari.

Siku moja najiandaa kwenda matembezini nafungua geti niishie zangu ghafla akatokeza mdada fulani tunayefahamiana. Alikuwa amevaa gauni la kitambaa chenye michoro mizuri sana na gauni kwa kweli lilimpendeza mno kwenye umbo lake la kuvutiwa.

Nikajikuta namwambia: Aisee Glory, umependeza sana. Alitabasamu, na kutoa maneno ambayo sikuyatarajia.
Aliniambia: "Kwa nini?" Hapo nikaishiwa nguvu nikarudia tena, "Umependeza sana"

Nimeshasifia watu kadhaa mchanganyiko, waume kwa wanawake na wananishangaza sana pale wanaposhindwa kutamka neno moja tu, 'asante' badala yake wanataka maelezo kwa kuuliza
'Kwa nini?' Wananiudhije?

Umeshakutana na watu wasiojua kusema 'asante?' unapowasifia?
 
hata mm nimeshakutana na watu wa aina hiyo sijui kwanini wanashindwaga kusema asante
siwaelewi
Habari zenu wana mmu.
Lipo neno la kiswahili lenye nguvu nyingi sana litumiwapo lakini
kuna watu hawajui kulitumia. Niwape mandhari.

Siku moja najiandaa kwenda matembezini nafungua geti niishie zangu ghafla
akatokeza mdada fulani tunayefahamiana. Alikuwa amevaa gauni la kitambaa chenye
michoro mizuri sana na gauni kwa kweli lilimpendeza mno kwenye umbo lake la kuvutiwa.
Nikajikuta namwambia: Aisee Glory, umependeza sana. Alitabasamu, na kutoa maneno ambayo sikuyatarajia.
Aliniambia: "Kwa nini?" Hapo nikaishiwa nguvu nikarudia tena, "Umependeza sana"

Nimeshasifia watu kadhaa mchanganyiko, waume kwa wanawake na wananishangaza sana pale
wanaposhindwa kutamka neno moja tu, 'asante' badala yake wanataka maelezo kwa kuuliza
'Kwa nini?' Wananiudhije?
Umeshakutana na watu wasiojua kusema 'asante?' unapowasifia?
 
Anauliza jibu kwanini kapendeza, kwani we ndo ulimpendezesha? Yy si ndiyo mwenye jibu la hilo swali kwann kapendeza. Shukrn ya punda teke
 
Kwa kweli ni ushamba uliopitiliza. Nakumhuka miaka ya nyuma mwenzangu mmoja kazini aliwahi kushitakiwa kwa boss na binti/mdada mmoja kisa anamtongoza kwa kumwambia kapendeza. Hebu jiulize neno "umependeza" linahusiana nini na mtu kudhani akisifiwa ni kwa sababu mwanaume amem mind kiaina. Wanatia aibu sana watu wa aina hii.
 
mzima wewe?
vipi jamani Erotica hajambo??
Halo mwalimu wangu gfsonwin. Mie sijambo sana.Nashukuru
umejitokeza maana ulipotea kwa muda hapa JF. Ya Erotica yamekatika! Kapotea tangu Desemba 2012!
Kaniachia wale mapacha. Vipi, shemeji kesharudi kutoka ng'ambo?
 
Last edited by a moderator:
Ahsante na samahani ni misamiati migumu kwa wengi, sijui kwanini. Wengine ni kutokujua thamani ya haya maneno. Wengine wapuuzia tu.
 
Nafikiri wanataka kufahamu wapi/kipi kilichofanya hadi umuone au uwaone wamependeza labda nywele, nguo, viatu nk ili kwa siku nyingine wawe wanavaa mara kwa mara mtindo wa hivyo ili wapate sifa tele
 
mzima wewe?
vipi jamani Erotica hajambo??

hata mm nimeshakutana na watu wa aina hiyo sijui kwanini wanashindwaga kusema asante
siwaelewi

Nina hamu na lollipop

Ahsante na samahani ni misamiati migumu kwa wengi, sijui kwanini. Wengine ni kutokujua thamani ya haya maneno. Wengine wapuuzia tu.

Mwingine anakujibu"mbona kawaida"
Mumependeza sana. mia
 
Ahsante na samahani ni misamiati migumu kwa wengi, sijui kwanini. Wengine ni kutokujua thamani ya haya maneno. Wengine wapuuzia tu.
Kweli kabisa Bantu lady. Inaudhije? Mtu anakupiga kikumbo barabarani kisha anakutazama halafu anakunja ndita!
 
Last edited by a moderator:
Hii tabia ya kusema "asante" au kumsifu mtu au kumpongeza ina mahusiano makubwa na malezi tuliolelewa nayo. Asilimia kubwa tabia hii hujengwa na wazazi au walezi wetu. Hujawahi kuona watoto wadogo ambao,mfano,wanapofika ugenini husalimia kila mtu au hushukuru kwa kila wanachopewa? Vilevile Hujawahi ona mtoto ambae akiambiwa "msalimie Anko" ndio kwanza anazidi kumkumbatia Mama yake? Hao watoto ndio vijana wa kesho...na sisi ni watoto wa jana.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom