Hawaaminiani tena Dodoma

Hapa kujiokoa kwa chama chenu ni uwazi na ukweli sio wa chenkapa bali uwazi wa nani anahusika, amekula au ameoga hizo pesa za EPA na Richmond!
 
Leo baada ya Lowassa kutoka kwenye Ukumbi na hasa baada ya maneno ya Dr. Mwakyembe ni wazi kuwa hawa ndugu zetu hawaaminiani tena. Chama chetu ambacho kimetulea na kutufikisha hapa; chama ambacho kilisikifika kwa umoja na mshikamano, leo hii kimejaa shuku na kebehi. Kuna wabunge hawakai sehemu moja na juzi kuna mahali tulikuwa na mbunge fulani wa kaskazini alipokuja mwenzie wa kusini kama kusabahi yule mwingine akatuaga haraka haraka kabla hajapokea mkono wa mbunge mwenzie.
Ndugu zangu hali ni mbaya ndani ya CCM. Hata maneno ya Chitalilo juzi hii kuhusu "kuvunja ndoa ya mtu" alikuwa anawalenga watu fulani fulani. Sijui CCM itakwenda wapi.

Asanteni.

unajuaje kama walikutana kwenye unga unga????
 
[
QUOTE=Bi. Senti 50;230554]Leo baada ya Lowassa kutoka kwenye Ukumbi na hasa baada ya maneno ya Dr. Mwakyembe ni wazi kuwa hawa ndugu zetu hawaaminiani tena. Chama chetu ambacho kimetulea na kutufikisha hapa; chama ambacho kilisikifika kwa umoja na mshikamano, leo hii kimejaa shuku na kebehi. Kuna wabunge hawakai sehemu moja na juzi kuna mahali tulikuwa na mbunge fulani wa kaskazini alipokuja mwenzie wa kusini kama kusabahi yule mwingine akatuaga haraka haraka kabla hajapokea mkono wa mbunge mwenzie.

Ndugu zangu hali ni mbaya ndani ya CCM. Hata maneno ya Chitalilo juzi hii kuhusu "kuvunja ndoa ya mtu" alikuwa anawalenga watu fulani fulani. Sijui CCM itakwenda wapi. Naomba wana CCM wenzangu tuwatake viongozi wetu kukaa chini pamoja na kumaliza tofauti zao ndani ya chama. Vinginevyo lile "lililotabiriwa" litatokea. Tusiwape wapinzani wetu nafasi ya kufurahi na wabaya wetu kushangilia.

Wale mnaofanya kazi maeneo ya Bungeni na wakeretwa tuwasiliane tuone jinsi gani tunaweza kuwasaidia wabunge wetu na kukiimarisha chama chetu. Tusiache wapinzani wavune wasichopanda. Kuna watu ambao wanapata sifa za bure tu kutokana na mapungufu ya chama chetu. Tusimame na sisi.

Asanteni.
[/QUOTE]

Mama 50,

Hivi chama chenu ndiyo kile cha mafisadi ambao wakinyoshewa kidole tu basi inakuwa vurugu mtindo mmoja? Hivi unataka Fisadi amwamini nani zaidi ya Fisadi mwenzake?

Ushauri wangu ni kuwa Mafisadi wote walio kwenye hicho "chama chenu" watimuliwe au wajiengue wenyewe watuachie Chama chetu; hili si suala la chenu na chetu, tunataka kuona Tanzania yenye neema na maisha bora kwa kila mtanzani na si habari za chama chenu na chama chetu.

NAKUOMBA UWE MZALENDO ZAIDI, ULINDE MASLAHI YA TANZANIA KWA AJILI YA AMANI NA MUSTAKABALI MWEMA WA WATANZANIA, NA SI MUSTAKABALI WA CHAMA CHETU NA CHAO!
 
Sasa hawa jamaa kama hawaaminiani hivyo, wanaendeshaje nchi?

Machache mazuri tuliyonayo as a nation, yametokana na wao kutoaminiana, mkuu siku wakiaminiana tumekufa ni afadhali waendelee hivyo hviyo walivyo sasa yaani kutoaminiana!
 
Hapo umenena FMES.

Mama 50, wacha hali iendelee kuwa mbaya wachujane wenyewe kwa wanyewe mpaka wabaki wasafi.
 
AFu JK ana niudhi kweli, Hivi anashindwa nini kuacha haki ichukue mkondo wake?

Yaani watu tunawangwa vichwa badala tufikirie mambo mengine ya kutuletea maendeleo tunabakia kuimba ufisadi ufisadi, kwanini asiache haki itendeke? aliyekosea awajibishwe?

Hako ka kifua unako wakingia mafisadi mwishowe katapasuka mkuu, wacha kila mtu abebe mzigo wake! Kalagabaho!
 
Leo baada ya Lowassa kutoka kwenye Ukumbi na hasa baada ya maneno ya Dr. Mwakyembe ni wazi kuwa hawa ndugu zetu hawaaminiani tena. Chama chetu ambacho kimetulea na kutufikisha hapa; chama ambacho kilisikifika kwa umoja na mshikamano, leo hii kimejaa shuku na kebehi. Kuna wabunge hawakai sehemu moja na juzi kuna mahali tulikuwa na mbunge fulani wa kaskazini alipokuja mwenzie wa kusini kama kusabahi yule mwingine akatuaga haraka haraka kabla hajapokea mkono wa mbunge mwenzie.

Ndugu zangu hali ni mbaya ndani ya CCM. Hata maneno ya Chitalilo juzi hii kuhusu "kuvunja ndoa ya mtu" alikuwa anawalenga watu fulani fulani. Sijui CCM itakwenda wapi. Naomba wana CCM wenzangu tuwatake viongozi wetu kukaa chini pamoja na kumaliza tofauti zao ndani ya chama. Vinginevyo lile "lililotabiriwa" litatokea. Tusiwape wapinzani wetu nafasi ya kufurahi na wabaya wetu kushangilia.

Wale mnaofanya kazi maeneo ya Bungeni na wakeretwa tuwasiliane tuone jinsi gani tunaweza kuwasaidia wabunge wetu na kukiimarisha chama chetu. Tusiache wapinzani wavune wasichopanda. Kuna watu ambao wanapata sifa za bure tu kutokana na mapungufu ya chama chetu. Tusimame na sisi.

Asanteni.

Kumbe mwenzetu uko nao karibu hivyo!!! May be wasaidie kuwapa ushauri
 
Hawa wakuu sidhani kama walikua wanaaminiana siku zote, ni kwamba walikua wanaficha tu sura zao halisi, bila shaka ili kulinda ulaji. Hatukujua uhalisia wao.
 
kwi kwi kwi Kuvuja kwa pakacha...... kusema ukweli mi naomba wajichanganye hivyo hivyo ili 2010 tuwapige chini wafutike kama KANU maana hivi vyama tawala ukishaviondoa madarakani basi huwa vinakufa kifo cha mende. miaka 46 mliyoiba inatosha tupisheni wenye uchungu wa kuifikisha TZ kwenye maendeleo ya kweli.
 
Leo baada ya Lowassa kutoka kwenye Ukumbi na hasa baada ya maneno ya Dr. Mwakyembe ni wazi kuwa hawa ndugu zetu hawaaminiani tena. Chama chetu ambacho kimetulea na kutufikisha hapa; chama ambacho kilisikifika kwa umoja na mshikamano, leo hii kimejaa shuku na kebehi. Kuna wabunge hawakai sehemu moja na juzi kuna mahali tulikuwa na mbunge fulani wa kaskazini alipokuja mwenzie wa kusini kama kusabahi yule mwingine akatuaga haraka haraka kabla hajapokea mkono wa mbunge mwenzie.

Ndugu zangu hali ni mbaya ndani ya CCM. Hata maneno ya Chitalilo juzi hii kuhusu "kuvunja ndoa ya mtu" alikuwa anawalenga watu fulani fulani. Sijui CCM itakwenda wapi. Naomba wana CCM wenzangu tuwatake viongozi wetu kukaa chini pamoja na kumaliza tofauti zao ndani ya chama. Vinginevyo lile "lililotabiriwa" litatokea. Tusiwape wapinzani wetu nafasi ya kufurahi na wabaya wetu kushangilia.

Wale mnaofanya kazi maeneo ya Bungeni na wakeretwa tuwasiliane tuone jinsi gani tunaweza kuwasaidia wabunge wetu na kukiimarisha chama chetu. Tusiache wapinzani wavune wasichopanda. Kuna watu ambao wanapata sifa za bure tu kutokana na mapungufu ya chama chetu. Tusimame na sisi.

Asanteni.

Haya ni mawazo ya kifisadi. Wapinzani nao ni Watanzania ambao wamelitolea jasho Taifa la Tanzania. Hebu fumbua macho uone kwamba CCM tuliyoijua miaka ile siyo hii ya sasa, sasa kimekuwa ni chama cha mafisadi.
 
Back
Top Bottom