Hawaaminiani tena Dodoma

Bi. Senti 50

JF-Expert Member
Apr 17, 2007
290
12
Leo baada ya Lowassa kutoka kwenye Ukumbi na hasa baada ya maneno ya Dr. Mwakyembe ni wazi kuwa hawa ndugu zetu hawaaminiani tena. Chama chetu ambacho kimetulea na kutufikisha hapa; chama ambacho kilisikifika kwa umoja na mshikamano, leo hii kimejaa shuku na kebehi. Kuna wabunge hawakai sehemu moja na juzi kuna mahali tulikuwa na mbunge fulani wa kaskazini alipokuja mwenzie wa kusini kama kusabahi yule mwingine akatuaga haraka haraka kabla hajapokea mkono wa mbunge mwenzie.

Ndugu zangu hali ni mbaya ndani ya CCM. Hata maneno ya Chitalilo juzi hii kuhusu "kuvunja ndoa ya mtu" alikuwa anawalenga watu fulani fulani. Sijui CCM itakwenda wapi. Naomba wana CCM wenzangu tuwatake viongozi wetu kukaa chini pamoja na kumaliza tofauti zao ndani ya chama. Vinginevyo lile "lililotabiriwa" litatokea. Tusiwape wapinzani wetu nafasi ya kufurahi na wabaya wetu kushangilia.

Wale mnaofanya kazi maeneo ya Bungeni na wakeretwa tuwasiliane tuone jinsi gani tunaweza kuwasaidia wabunge wetu na kukiimarisha chama chetu. Tusiache wapinzani wavune wasichopanda. Kuna watu ambao wanapata sifa za bure tu kutokana na mapungufu ya chama chetu. Tusimame na sisi.

Asanteni.
 
Tatizo kwenye hiki chama chetu kuna kulindana hata kama mtu kweli kafanya kosa!Cha maana hapa ni kutokulindana ili kulinda heshima ya chama.Sasa kama mwenyekiti wa chama anawasaficha mafisadi kweli hiyo ni haki?inabidi kuondoa unafiki ili mtu unapokwenda kinyume na maadili ya kazi unaadabishwa hata kama ni mwenyekiti mwenyewe wa chama!hapo watu wataogopa kuaibika na watafanya kazi kwa uadilifu bila kufisadi nchi!
 
Bi Senti Hamsini,
Wapinzani nao ni Watanzania kama ninyi. Kilichopandwa Tanzania tumepanda sote. Kama CCM imefikia hali inaonekana kuwa basi chakavu la abiria lililoishiwa petroli basi liacheni kwenye kilima na jiungeni na basi jipya la upinzani ili kuendelea kuijenga Tanzania isiyo na ufisadi na vijembe.
 
Leo baada ya Lowassa kutoka kwenye Ukumbi na hasa baada ya maneno ya Dr. Mwakyembe ni wazi kuwa hawa ndugu zetu hawaaminiani tena. Chama chetu ambacho kimetulea na kutufikisha hapa; chama ambacho kilisikifika kwa umoja na mshikamano, leo hii kimejaa shuku na kebehi. Kuna wabunge hawakai sehemu moja na juzi kuna mahali tulikuwa na mbunge fulani wa kaskazini alipokuja mwenzie wa kusini kama kusabahi yule mwingine akatuaga haraka haraka kabla hajapokea mkono wa mbunge mwenzie.

Ndugu zangu hali ni mbaya ndani ya CCM. Hata maneno ya Chitalilo juzi hii kuhusu "kuvunja ndoa ya mtu" alikuwa anawalenga watu fulani fulani. Sijui CCM itakwenda wapi. Naomba wana CCM wenzangu tuwatake viongozi wetu kukaa chini pamoja na kumaliza tofauti zao ndani ya chama. Vinginevyo lile "lililotabiriwa" litatokea. Tusiwape wapinzani wetu nafasi ya kufurahi na wabaya wetu kushangilia.

Wale mnaofanya kazi maeneo ya Bungeni na wakeretwa tuwasiliane tuone jinsi gani tunaweza kuwasaidia wabunge wetu na kukiimarisha chama chetu. Tusiache wapinzani wavune wasichopanda. Kuna watu ambao wanapata sifa za bure tu kutokana na mapungufu ya chama chetu. Tusimame na sisi.

Asanteni.

Bi senti,

karibu tena jamvini. Ulipotea sana mwenzangu nikadhani Pinda amekunyang'anya kitumbua?

Usipotee hivyo mwaya!
 
Leo baada ya Lowassa kutoka kwenye Ukumbi na hasa baada ya maneno ya Dr. Mwakyembe ni wazi kuwa hawa ndugu zetu hawaaminiani tena. Chama chetu ambacho kimetulea na kutufikisha hapa; chama ambacho kilisikifika kwa umoja na mshikamano, leo hii kimejaa shuku na kebehi. Kuna wabunge hawakai sehemu moja na juzi kuna mahali tulikuwa na mbunge fulani wa kaskazini alipokuja mwenzie wa kusini kama kusabahi yule mwingine akatuaga haraka haraka kabla hajapokea mkono wa mbunge mwenzie.

Ndugu zangu hali ni mbaya ndani ya CCM. Hata maneno ya Chitalilo juzi hii kuhusu "kuvunja ndoa ya mtu" alikuwa anawalenga watu fulani fulani. Sijui CCM itakwenda wapi. Naomba wana CCM wenzangu tuwatake viongozi wetu kukaa chini pamoja na kumaliza tofauti zao ndani ya chama. Vinginevyo lile "lililotabiriwa" litatokea. Tusiwape wapinzani wetu nafasi ya kufurahi na wabaya wetu kushangilia.

Wale mnaofanya kazi maeneo ya Bungeni na wakeretwa tuwasiliane tuone jinsi gani tunaweza kuwasaidia wabunge wetu na kukiimarisha chama chetu. Tusiache wapinzani wavune wasichopanda. Kuna watu ambao wanapata sifa za bure tu kutokana na mapungufu ya chama chetu. Tusimame na sisi.

Asanteni.

Bibi Cent umezoea kula vya bure vya kunyoka vya kufisadi sasa unaogopa utavikosa ehe? Anza kukaza buti utafute vya halali kama binadamu wengine. Au ukiona mambo yanaenda vibaya kwa macheni panalipa...
 
Bi, point yako ya hii topic ni nini? unavyosema chama chetu unamuongelea nani? webmaster kama hakuna hoja futa hii topic
 
kama hawaaminiani si watwangane tu.Furaha ya panzi ni faida kwa kunguru,awe wa bara au yule wa Zanzibari
 
Ndugu zangu hali ni mbaya ndani ya CCM. Hata maneno ya Chitalilo juzi hii kuhusu "kuvunja ndoa ya mtu" alikuwa anawalenga watu fulani fulani. Sijui CCM itakwenda wapi. Naomba wana CCM wenzangu tuwatake viongozi wetu kukaa chini pamoja na kumaliza tofauti zao ndani ya chama. Vinginevyo lile "lililotabiriwa" litatokea. Tusiwape wapinzani wetu nafasi ya kufurahi na wabaya wetu kushangilia.

Kumbe kule kuvunja nyumba ndiyo huku! Mimi nilikuwa na wasiwasi kuwa mheshimiwa hakumaanisha mvunjaji kibaka bali wa design hii. Basi iko kazi.
 
Mwalimu alikufa!
Wanamtandao ambao waligharamia shughuli zake za kampeni walifurahia na kuiuza nchi moja kwa moja!
Wanamtandao wanajua mwalimu alikufa na nini?
Kifo cha mwalimu kilikuwa ni kifo cha ccm na uhakiki wa uhai na utawala wa wanamtandao.
ccm ilishazikwa na mwalimu na mnatakiwa kufahamu hili ili Tusonge mbele na kulirudisha taifa letu kwa wananchi!
 
Bi 50 senti
Pole sana mama. Huu ni wakati mafisadi mnapambana toka ndani na nje. Usihofu. Soma alama za nyakati.
Kigumu chama cha mafisadi.
 
Mafisadi wako hoi brother. Wamelikoroga na walinywe.
Maana naona fisadi mchanga Mkullo anaendelea kukoroga lake asubiri kulinywa pia.;)

Lazima mafisadi wazimie kwa pressure, hivi unafikiri nani anaweza tena kumwamini Lowassa katika tanzania. Wakati siku anaachia kiti vyombo vyote vya habari kuanzia bongo mpaka Arusha, mpaka mwanza mpaka kila kona, either vilisikika au vilionyesha live.

Nakwambia hata wananchi wote Tanzania nzima walime Dodoki na kumuuzia Lowassa akitumia pesa zote za Richmond na EPA hataweza kutakata kabisa.

Sana sana anajitafutia umasikini tu. Ningelikuwa mimi ningestaafu siasa na pia kuwaomba watanzania msamaha.

Wale wote katika kikundi wana mapungufu tu hata juzi unasikia kijana mdogo Serukamba naye anajiingiza kwenye moto.

Kilichobakia ni kuparaganyika hili tukawapeleke segerea vizuri. Na muda si mrefu hilo litatokea. Nafikiri JK hawezi kujiunga na kundi ambalo limeisha poteza kabisa imani kwa wananchi wa tanzania waliomchagua kwa kishindo.

Otherwise kuanzia siku atakayojiunga na kundi hilo na yeye moto utakuwa huo huo mpaka atakapomaliza kipindi chake mwaka 2010.
 
Haiwezekani kuwekwa sawa tayari wameshapata kensa katika chama chao na hakuna dawa ,ila kutakuwepo kuvumiliana na atakaezubaa atawekwa upande ili kuimarisha kikosi cha wapendanao ,kwa mantiki hiyo hiyo kila upande utakuwa unaheshimu upande mwengine ukitokea upande mmoja kuukamata shati upande mwengine hapo ndio inapozuka patashika ,wanaokimbilia magazetini wanaokimbilia redioni na wanaokimbilia wazee wote watasimama kidete kila mmoja akimunyooshea kidole mwenziwe.Bora tupate raisi zezeta kuliko mwenye akili nyingi na busara ,tutakuwa hatufiki sehemu kila tunapoona pana ubora mwenye akili atapanga mikakati mbinu na njia za kulifikia lakini tukipata Raisi zezeta basi atakatisha njia ya mkato japo ina miba lakini tutafika tunapokwenda haizuru ikiwa wengine watazurika na sumu ya miba na kufa njiani kizazi kijacho kitanufaika.

WanaCCM, chama chenu kiko taabani. Kinaelekea kule kule ilikokwenda KANU ya Daniel arap Moi, Malawi National Congress ya Kamzu Banda, UNIP (United National Independency Party) ya Kenneth Kaunda, na vinginevyo.
Vipimo vinaonyesha wazi kwamba virusi vya UKIU (Ukosefu wa Kinga ya Ufisadi), vimeenea mwili mzima wa chama kuanzia kichwani (Makao Makuu) hadi nyayoni (kwenye mashina). Napenda niwakumbushe kwamba hapo chama kilipofikia hakuna kinga wala tiba tena labda mjaribu kubadilisha kabisa damu (total blood transfusion) ambapo unaondoa damu yote mwilini yenye virusi na kuweka damu safi.
 
ccm wakiwakamata mafisadi basi wataiponya nchi!
Raia wema walioko mitaani na mafisadi hao wanaogopana... kama mafisadi wakishinda vita hii basi raia wema wana tabu!
 
JK aliingia madarakani kwa mizengwe , wizi wa kura , dhuluma , hila na uchfu mwingi .CCM wamekuwa wakiiba kwa nguvu na kuwadharau watanzania .Mungu kaamuwa kuwafanya zile za mnara wa Babeli .Leo Kilango , kesho Chitalilo na wengine humo humo .Mungu ana nia ya kuikomboa Tanzania na hakuna wa kuzuia hili .Watanzania simameni sasa semeni kwa sauti moja daini haki na wakati ndiyo huu .
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom