Hawa watu wawili (2) walizaliwa hapa Tanganyika/Tanzania nyakati zisizo sahihi kwao!

1. Mwl. Julius Kambarage Nyerere

Ukitazama akili, ushawishi na maarifa aliyokuwa nayo ingepaswa azaliwe kipindi ambacho nchi inao wasomi wa kutosha kumpa changamoto. Waliokuwepo wachache kama akina Hayati Kambona lakini kwa nchi kutokuwa na wasomi akina Hayati Kambona waliishia kuonwa wasaliti.

2. Zitto Zuberi Kabwe

Huyu anapambana kipindi ambacho tuna watu wanaojidai wasomi lakini wengi ni wachumia tumbo tu! Wasomi wa aina ya akina Mwigulu NcHuhemba, Palamagamba Kabudi n.k.
Huyo wa kwanza uliyemtaja ndio katufikisha kwenye matatizo yote haya alipewa nafasi ya kujenga msing akajenga msingi mbovu.
 
4. Chifu Mkwawa.
Aliweza kupambana na wakoloni miaka hiyo. Alitakiwa aishi enzi za TANU na angefaa kuws Rais wa kwanza wa Tanganyika na Tanzania. Pamoja hakuwa msomi na hakuenda hata darasa moja ila alikuwa na akili sana. Kama angekuwa enzi za TANU nchi na akawa Rais nchi ingekuwa mbali sana.
Naona TANU unaisikia tu kwenye halaiki, TANU ilisambalatishwa baada ya Uhuru ikabaki na Nyerere na Kawawa, utashangaa wapo waliomkaribisha Nyerere ukiambiwa hao ndiyo waanzilishi utakataa kwani walipigwa marufuku kusikika, hapa ndipo tutakapoanza kubishana kati ya walioiona TANU ikianza na wale walioimbishwa kwenye halaiki za uwanja wa taifa.
 
Madalali wa wazungu? Kina mkapa na kikwete?? Hivi matehemu Seth chachage aliwaandika kina nani kwenye kitabu chake cha "makuwadi wa utandawazi"

We dogo tu. huna unalolijua hapa duniani zaidi ya ushabiki tu.
Dalali ni Zitto anayekwenda nje kuongea na wazungu ili wadogo zake kule Kigoma wasipate pesa ya elimu.

Aina hii ya watu kule jirani kwa Kagame au enzi za Moi siku nyingi wangeshafukiwa.

Kikwete na Mkapa walizunguka dunia nzima ili hospitali zijengwe, ili vyuo vijengwe, ili maji yapatikane, ili Mloganzila ijengwe, ili usafiri wa mwendo kasi uweze kuwepo, huwezi kabisa ukawalinganisha na wanasiasa wanafiki na waliojaa hila kama Zitto.

Wewe ndio dogo unayeongea vitu usivyovifahamu kwa kina.
 
Huyo wa kwanza uliyemtaja ndio katufikisha kwenye matatizo yote haya alipewa nafasi ya kujenga msing akajenga msingi mbovu.
Ungepata picha japo kidogo tu ya aina ya uhusiano aliokuwa nao Mwalimu Nyerere na pande mbili kwa maana ya urusi na marekani miaka ya mwanzoni baada ya uhuru usingekuwa na mawazo uliyonayo.
 
Ungepata picha japo kidogo tu ya aina ya uhusiano aliokuwa nao Mwalimu Nyerere na pande mbili kwa maana ya urusi na marekani miaka ya mwanzoni baada ya uhuru usingekuwa na mawazo uliyonayo.
Inaelekea uko uninformed, na una utumwa wa kifikra na inaonekana wewe ni wale waru mna laumu wakoloni kwa nchi zetu kukosa maendeleo miaka 50+ ya uhuru.
 
Inaelekea uko uninformed, na una utumwa wa kifikra na inaonekana wewe ni wale waru mna laumu wakoloni kwa nchi zetu kukosa maendeleo miaka 50+ ya uhuru.
Mtumwa wa kifikra humjui, unasikia tu wakubwa wanaongea na wewe unapita humo humo. Nyerere alikumbana na presha kubwa wakati nchi ndio kwanza imepata uhuru.

Mzungu siku zote anataka akutawale, hata asipokuwa karibu na kivuli chako bado anazitumia sera zake kama fimbo ya kukuchapia, anatupia taasisi zake kubwa kama fimbo za kukuweka utumwani. Maisha ni vita.
 
Uko misinformed brother, period!
 
Ilikuwepo,na tz ilikua inafanya vema,
Kipindi hicho sehemu kubwa ilikua ni kujitolea hata mishahara kama ilikuwepo basi ni finyu sana tofauti na sasa wachezaji wanapewa mpaka makazi,usafiri n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli, lakini kuna ukweli mwingi ambao wengi tunaupuuza kwa hapo awali maisha yalikuwa bora kuzidi sasa.
Mfano nyumba zilikuwa za kupanga na zinapatikana ambapo ujenzi wa mabondeni na slums haukuwa kama sasa. Pia usafiri kwa daladala na hata treni za kwenda mikoa ulikuwa reliable kuzidi sasa.
Ndio maana pamoja na sasa kupewa hizo prevallage bado wanalialia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom