Hawa watu huwa wanamaanisha nini?

Short-Gun

Member
Jun 3, 2014
94
7
Kuwekuwa na tabia inayofanywa na watu wengi kwenye mitandao mbalimbali ukikutana nao mnakuwa marafiki na wanakuambia wao ni wakimbizi wapo senegal au sudan kwahiyo wanakuomba mawasiliano yako ili wakuhamishie fedha walizoachiwa na wazazi sasa, swali ni kwamba kama wao wana hizo fedha kwanini wasizitumie wenyewe?.Wanakera sana ndio maana nimehamia JF nipate elimu sio kuibiana kimachomacho.
 
Ni matapeli zaidi ya uujuavyo utapeli, ukisikia harufu yao chomoka nduki
 
Kuwekuwa na tabia inayofanywa na watu wengi kwenye mitandao mbalimbali ukikutana nao mnakuwa marafiki na wanakuambia wao ni wakimbizi wapo senegal au sudan kwahiyo wanakuomba mawasiliano yako ili wakuhamishie fedha walizoachiwa na wazazi sasa, swali ni kwamba kama wao wana hizo fedha kwanini wasizitumie wenyewe?.Wanakera sana ndio maana nimehamia JF nipate elimu sio kuibiana kimachomacho.
Niliingia fb 2011 nikakumbana na mmoja aliyejifanya msichana, tena mrembo sana aliponitumia picha yake. Aliniambia amenipenda sana na akataka nimtumie namba ya akaunti yangu ya benk ili aniwekee hela huko. Niliogopa sana na tangu desemba 2011 mpaka leo sijaingia tena fb. Nimegundua fb ni kituo cha matapeli.
 
Wao wanachotaka ni kupata account number yako. Ukishalogwa ukawapa, umekwisha. Hautajua pesa zimechotwa vipi, lakini utakuta account yako nyeupe. Jihadhari na hao matapeli wa kimataifa.

Tiba
 
Halafu kibaya zaidi hata kama umeoa/kuolewa bado wanapost picha zao ili upagawe uwatumie taarifa muhimu za akaunti yako
 
Wao wanachotaka ni kupata account number yako. Ukishalogwa ukawapa, umekwisha. Hautajua pesa zimechotwa vipi, lakini utakuta account yako nyeupe. Jihadhari na hao matapeli wa kimataifa.

Tiba

Kuna babu mmoja amestaafu mwezi April 2013 alijikoka huko yaliyomkuta siyasemi, ila utamhurumia
 
Wao wanachotaka ni kupata account number yako. Ukishalogwa ukawapa, umekwisha. Hautajua pesa zimechotwa vipi, lakini utakuta account yako nyeupe. Jihadhari na hao matapeli wa kimataifa.

Tiba

Urongo. mie acct yangu ni 10202845001 Barclays Temeke. Jina T. Bategereza
 
Sasa wewe ndugu yangu unanipa account yako umesikia mimi ninahiitaji? Wasubiri hao wanigeria wakuandikie email halafu uwapatie hiyo account yako. Lakini suala la msingi sio kujua account yako suala ni je hiyo account ina hela? Kama zipo ni ngapi?

Tiba
 
Wao wanachotaka ni kupata account number yako. Ukishalogwa ukawapa, umekwisha. Hautajua pesa zimechotwa vipi, lakini utakuta account yako nyeupe. Jihadhari na hao matapeli wa kimataifa.

Tiba

hahaha ngumu sana mbona account number zipo hadharani,si kweli

huwa wanasema hela zao zipo fixed ili wapate zinatakiwa zitumwe kwa mtu wa karibu akiwa nchi tofauti

utapeli ni wewe sasa kutuma gharama za usafirishaji afu baada ya kutuma wao kimya.
 
Mkuu account ziko wazi wapi? Ya kwangu unaijua? Kumbuka ili wakuibie account lazima iwe na pesa pia ili wawe na cha kuiba. Kwa nini gharama za kusafirisha pesa zilipwe na wewe zisikatwe kwenye account zinakotoka?

Tiba
 
Back
Top Bottom