Bigjahman
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 900
- 512
mkuu we pita tu uendelee na maisha hii nchi ina wenyewe...nilishangazwa na habari nilizozikuta arusha mitaa inaitwa Fire karibu na unga ltd, kuna majambazi yamezaliwa pale ( majina nayatunza),na yanajulikana mpaka central lakini hakuna wa kuyafanya kitu. Kuna binti alibakwa relini pale, akaenda kusema kwao kuwa kawaona waliombaka wameelekea nyumba gani, baba yake akaongozana naye kuwajua kufika akakuta ni wale jamaa, alichofanya eti akawauliza ,'nilikuwa nauliza njia ya kwenda kwa balozi'...hakuthubutu hata kuhoji walichomfanya mwanae, ukienda polisi wanawakamata, next day wako nje alaf wanakutafta na kukupiga mpaka ufe...hii nchi ni ya tofauti!! Alaf pakitokea msako ikajulikana wezi wamekimbilia sehemu flani ,then polisi uenda fire kuwakodi hawa majambazi ili wakawakamate hao wengine, yani ni vituko duniani!!mmoja wao kamuoa dada wa jamaa aliyenipa habari, eti kamuoa kwa nguvu/lazima na kawataadharisha siku akikimbia ataenda kwao na kuwaua wote...uyo binti akirudigi tu home kusalimia wanamfukuza arudi kwa mmewe haraka isije kuwa shida, vyombo vya usalama angaika na hawa watu jamani, ni hatari katika jamii!!
Mmoja ni kamanda maarufu sana wa green army