Waberoya, naomba kutofatiana na wewe, sio kweli kuwa CCM wote ni wezi!. Naomba tuwe more realistic bila kuendekeza hisia!
Japo ni kweli CCM wengi ni wezi, ila sio wote!. Ndani ya CCM bado kuna wasafi wachache, wengine nawajua ila usiombe niwataje!
Kuna wana CCM wanaishi kwenye object poverty, simply ni destitute!. They have nothing at all, hata kama labda wanamawazo ya kiiwizi but have nothing at all hata hicho cha kuiba hakuna!. Watu kama hawa kuwaita wezi, sio kuwatendea haki!.
Kuna viongozi wakubwa wa CCM, walikuwa na kila opportunities za kuiba na kujilimbikizia mali na kugeuka mabilionea!. Unaamini kuna viongozi wakuu waliokuwa wakiishi maeneo ya Oysterbay, walikuwa wajijifugia tu mbuzi /kuku kama miradi yao?. Unaweza kuamini kiongozi mkuu anaishi aneo la Sea View by the beach, anaishi na ng'ombe eneo hilo!. Sasa watu kama hawa, kuwaita wezi, kiukweli sio kuwatendea haki!.
Nimefika kwa baadhi yao ambao walikuwa safi, walilitumikia taifa hili kwa uadilifu mkubwa mpaka wakastaafu kwa heshima.Lakini baada ya kustaafu waligeuka masikini wa kutupwa na kuonewa huruma, sasa watu kama hawa, unapoaita wezi, sio kuwatendea haki!
Waberoya, wakati mwingine, tuwe wakweli, japo sio lazima sana kuwa wakweli kwenye keyboard ila tuwe wakweli ndani ya nafsi zetu!.
Kwa mapenzi mema na nchi yetu na mwana (CCM) napenda niwape mfano hai wa Bwana Lowasa asivyo muadilifu na asivyopenda kuwajibika kichama CCM na kiserikali. Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu mheshimiwa Edward Lowasa alikuwa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais mwaka 1995 na akaenguliwa kwa hoja nzito ya kutokuwa muadilifu na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, kwa ukweli (wala sio tuhuma) kuwa alikuwa amejilimbikizia mali nyingi kwa kipindi kifupi ndani ya CCM na
Serikali. Muda mfupi alikuwa ni mtumishi wa CCM, muda mfupi kama Mkurugenzi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha.
Mfano hai wenyewe uko hivi; tufuatane kwa kuusoma tafadhali:-
Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowasa alinipigia simu na kusema yafuatayo:
"Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma'. Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowasa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu. Hiyo ikawa itifaki njema kwangu!
Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema "Bwana Kasori,jana ulizungumza na Edward Lowasa; naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa taifa tafadhali".
Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu.
Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa "Mheshimiwa Edward Lowasa kupitia kwa Mhe. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma". Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa "Nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa"!
Watanzania wote, leo nawaomba radhi kuwa jibu hilo kwa uzito wa maneno hayo kuwa "Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa" kweli kwa kuzingatia heshima kati ya wazee hao wawili; "Kawawa sikumwambia hivyo"! Badala yake nilimdanganya (nawaomba radhi tena watanzania) jibu nililompa Mzee Kawawa ni kuwa juma lililokuwa linafuata tungekuwa Dar es Salaam na kwamba aje Msasani aongee na Baba wa Taifa. Mhe. Kawawa alikubali.
Nikarudi kwa Baba wa taifa kusema uongo (naomba radhi tena) kuwa "Mzee Kawawa ameomba mzungumze tatizo la Lowasa tutakapofika Dar es Salaam". Baba wa taifa alikubali na akaagiza nimuombe Mhe. mzee Kawawa kuwa Lowasa na Guninita na wapambe wengine wa Lowasa wote wafike Msasani.
Siku ya siku ikafika. Tukawepo Msasani na Mhe.mzee Kawawa akaja. Lowasa hakuwepo! Sababu anazijua mwenyewe.(muulizeni maana nasema ukweli). Mkutano ulipoanza mzungumzaji wa kwanza nikawa mimi, kueleza lengo la mkutano. Mzungumzaji wa pili alikuwa Baba wa Taifa na swali la kwanza ni kuuliza Lowasa yuko wapi?.
Bila kupoteza wakati Mwalimu alisema "Rashidi , huyu Kasori ananiambai eti niende Monduli nikasafishe jina la Mhe. Lowasa eti asikose ubunge kwamba nilimchafulia Dodoma katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Kutokana na ombi lako nilimtuma akuambie usiwe mjinga kama Lowasa. Kasori alikuambia eh?"
by:
Samwel. H. Kasori
Katibu mstaafu wa J.K.Nyerere
Simu: 0754 372141
NOTE:Wapambe wa lowassa mtusaidie kumuuliza lowassa kwa nini alikacha kikao cha msasani?? na Lowassa akipitishwa na ccm kugombea urais(kitu ambacho ni ndoto) kwa gharama zangu Huu waraka nimejitolea kuutembeza kila kijiji cha nchi hii na kuuonyesha kama zile sinema za yomba yomba zilivyokuwa zikionyeshwa bure kwenye viwanja vya wzi vijijini na kugawa kopi za kutosha kila kijiji,mjini ntawaachia chadema washughulike nae.....
nyie endeleeni kula hela zake na kumdanganya hapa!!!!