Hawa wanamuunga mkono Lowassa ktk CCM. Nani mwingine unamjua?

Duh wananchi wanaoishi bila umeme wanamtetea aliwaletea giza, ha! Ha! Ha! Mtu hakuiba anapewa nafasi bungeni ajibu tuhuma anakimbia, sasa anadai alionewa.

- Pasco Mwalimu naye vipi alimuonea bosi aliposema ni mwizi? Wewe mwenyewe umekubali kwamba Lowassa ni shetani sasa unageuka tena vipi mkuu? Lowassa kuondolewa CC haikuwa by accident mnahangaika bure! Hasafishiki!
nani alie msafi
 
Mkuu William, kadri ninavyozidi kukusoma ndivyo ninavyozidi kukufahamu uwezo wa uelewa wako kwenye serious issues kama Ripoti ya Mwakiembe!.

Nilisema huko nyuma ripoti ile sii lolote sii chochote na hapa narudia tena Ripoti ya Mwakiembe sii lolote sii chochote kwa hoja moja tuu!. Haikufuata principles za natural justice!. Ni kwa hilo tuu nineidismis!.

Nimeidismiss kwa kutumua utaratibu unaotuniwa kisheria ambao unasisitiza ili haki itendeke, haitoshi tuu kutendeka kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni bali pia lazima haki hiyo ionekane imetendeka!. (Justice must not only be done, but must be seen to be done).

Kitendo cha ripoti ile kushindwa kumuhoji Lowassa ndio udhaifu mkubwa wa ripoti hiyo kwa sababu imekiuka kanuni kuu ya kwanza ya utendaji wa haki inayosisitiza hakuna kuhukumiwa bila kusikilizwa! ( No one is condemned unheard).

Nilikuuliza wewe William kuwa jee unazijua sababu za ni kwa nini Lowassa hakuitwa kuhojiwa?. Jee unajua Mwakiembe aligundua nini kwenye ripoti yake lakini akaamua asiseme?. Hukujibu maswali hayo wala sikutegemei sasa ndio utayajibu!.

Ninachowaeleza wanajamvi humu, kama dhambi kuu ya Lowassa ni kashfa ya Richmond, nawahakikishia tena na tena, Lowassa aliwajibika kumnusuru mhusika mkuu!. Jamani Lowassa si yeye!, alibeba tuu mizigo ya watu na mpaka sasa bado anaendelea kuibeba misalaba ya watu ila nawahakikishieni itakapo muelemea ataibwaga.

Japo Bwana Wetu Yesu Kristo alizibeba dhambi zetu na ni kwa kuteswa kwake sisi tumeponywa, vivyo hivyo ndivyo Lowassa alivyofanya kwa kukubali kutwisha zigo la Richmond ili watu fulani wapone, kitendo cha hao aliwakingia kifua kuanza kumdhihaki kitapelekea uwezekano wa kulibwaga chini hilo pakacha.

TISS iko busy ku monitor movements zake, na wakijiridhisha yuko too vulnerable anaweza kusema yote, msishangae kama atazimishwa ghafla the mafia style!.

Namna pekee ya kumponya ni kumzawadia ugombea 2015 au kumpotezea kabla ya 2015!.

Kwa sisi ambao ni wapenda haki wa dhati, hatuntetei Lowassa kuwa sio fisadi la hasha!. CCM yote imeoza na inanuka rushwa top-botom, left, right and centre, ila tunachotaka ni Lowassa atendewe haki!. Na ikibidi ufike wakati kila mtu aubebe mzigo wake mwenyewe!,
Naendelea na My Tribute to this fallen hero, Mwamba wa Kaskazini, kwa kujikumbusha baadhi ya mabandiko yangu kumhusu shujaa huyu mpaka siku atakapo pumzishwa kwenye makao yake ya milele, let's celebrate the life and the times of Edward Lowassa.

RIP Shujaa Laigwanani Comred Edward Ngoyai Ole Lowassa,

Umepigana vita vilivyo vitakatifu, Mwendo umeumaliza,
Imani umeilinda.
Bwana alitoa,
Bwana ametwaa,
Jina Lake Lihimidiwe!.

Paskali
 
Ndugu yangu Romantic, kwa hoja hizi nimemuelewa, naamini na Chadema hili wanalielewa ndio maana yeye ni mzalendo kama Sabodo tofauti zao ni ndogo tuu, Sabodo anafanya uzalendo wazi wazi, yeye ni kisirisiri!.
Sabodo kamfuata Edo!
BILIONEA SABODO AFARIKI DUNIA..

Bilionea na Mchumi maarufu nchini, Mustafa Jaffer Sabodo amefariki Dunia leo alfajiri akiwa nyumbani kwakwe, Masaki jijini Dar es Salaam.

"Mzee amefariki leo alfajiri akiwa nyumbani. Taratibu za mazishi zinaendelea na atazikwa katika makaburi yaliyoko mtaa wa Bibi Titi Mohamedi karibu na CBE," amesema Danstan.

Marehemu Sabado alizaliwa mkoani Lindi na alikuwa akifanya biashara katika nchi za Ufaransa, India, Kenya, Sudan, Nigeria, Zimbabwe na Tanzania.

Atakumbukwa kwa mchango wake ulioanzisha Mwalimu Nyerere Foundation National Lottery alipotoa msaada wa Sh milioni 800. Alihusika katika utoaji wa misaada kadhaa iliyohusisha kilimo, ujenzi wa visima na kusaidia wenye uhitaji.
Sabodo atazikwa leo saa 4:30 usiku.
Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un.
“We surely belong to Allah and to Him we shall return”
"Sisi sote ni wa Mola, na kwake tutarejea".

Paskali pia anakuaga!.
RIP Jaffar Sabodo.
 P
 
Back
Top Bottom