Hawa UDART hawaguswi?

Msitari wa pambizo

JF-Expert Member
Sep 25, 2014
2,880
4,883
Huu mradi umekua kero mpaka inatia hasira kuuzungumzia. Yani magari bado hayatoshi na hata hayo machache yaliyopp mengi ni mabovu. Yani unafika pale gerezani foleni kila mahali na kuna magari zaidi ya 20 yamepaki. Sasa unajiuliza nani huyo anayekula hii nchi asiyeguswa? Nani huyo ambaye anawatesa wananchi na hakuna hata anayewaonea huruma hawa wananchi?

Mbaya zaidi wamezuia route za daladala za kutoka mbezi-ubungo-magomeni to kariakoo/posta. Sasa u ajiuliza wao wamezuia daladala alaf wameleta magari yao ya mwendokasi ambayo hayakidhi mahitaji.

Yani nchi hii ni upigaji upigaji upigaji. Hao UDART wanapigiwa kelele kila siku lakini hakuna anayesikiliza. Hii hii serikali ina viongozi kweli?
 
Hili ni la mda mrefu, na sijaona mtu wakutatua hizi kero.
Hali ilipofikia sasa CCM wametuona Watanzania ni mandondocha wanafanya wanavyojisikia kwakuwa wameajiaminisha hatuwezi kuwafanya chochote na kweli kwa sababu hatuwezi kuwatoa kupitia sanduku la kura hata iweje wao ndiyo watatangazwa kuwa washindi hivyo kama ikitokea siku Watanzania watasema wamechoka na maloloso ya CCM watajua cha kufanya vinginevyo tutaendelea kulalamika kupitia humu mitandaoni huku wenzetu wameziba masikio,ebu fikiria leo hii imefikia hatua wanaona chochote wanachofanya katika kutekeleza wajibu wao wao wanaona ni kama wanatoa msaada kwa Watanzania ndiyo maana kila kukicha wanatoa shukurani kwa mwenyekiti wao kwa kutoa hiki au kile kwa sababu wao hawaoni kama serikali ina wajibu kwa wananchi wake bali wanachokiona wao ni misaada tu inayotolewa na mwenyekiti wao ambaye ni Rais wa nchi japo hawasemi hayo mabilioni anayotoa kama msaada(kwa mujibu wao) anayatoa wapi! Lakini wanayafanya yote hayo kwa kuwa tu wanatudharau wananchi na wanatuona mabwege nazi.
 
Eti mkuu wa mkoa akajifanya kuwapa wiki 2 anataka kuona hakuna basi bovu na yote yako barabarani

Yaani yule mzee sura yake msanii msaniiiiiiii

Ila waTz tuna shida sana. Yesu tu arudi kwa kweli. Watu wanaotakiwa kuwa serious ndio bosheni balaaa.
 
• 🤔, Nina wasiwasi na ule mwenge unaotembezwa kila mkoa😀,

• Sisi watanzania ni wapole sana, hata viongozi walete ujinga kiasi gani, kuandamana hatuwezi, tunabaki kusikitika mitandaoni ,
 
je week 2 zimepita? Na kama zimepita wamemdharau?
 
• 🤔, Nina wasiwasi na ule mwenge unaotembezwa kila mkoa😀,

• Sisi watanzania ni wapole sana, hata viongozi walete ujinga kiasi gani, kuandamana hatuwezi, tunabaki kusikitika mitandaoni ,
Ule mwenge ni uchawi tu hauna faida yoyote nyingine nchi hii tunaabudu mizimu bila kujijua.
 
Yaani huwa nashindwa kuielewa Serikali hii ya Awamu ya 6 ya Mh Samia,..yaani CHANGAMOTO ndogo kama hiyo mnashindwa vipi kuitatua?

Mna instrumentals zote..ndio mnasema ninyi eti MNAJALI wanyonge..KWELI?

Jaribuni basi kufanya haya;
1.Ongezeni mzabuni mwingine binafsi awasaidie,kama sheria ni shida,badilisheni

2.Ruhusuni mabasi/daladala zirejee njia hizo

3.Wapeni JWTZ wasimamie,kwani hali ni zaidi ya DHARURA

Hivi huwa hamuoni AIBU?..
 
Sio tu huo mradi, miradi ambayo inasuasua ipewe JWTZ kusimamia tuone matokeo chanya.
 
Back
Top Bottom