Hawa ndo wanawake bana!

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,920
Hiki kisa mtu anaweza kudhani ni masikhara,lakini imetokea na ni kama mwezi umepita tu

Mhanga ambae ni mwalimu wa shule moja ya msingi hapa jijini Mwanza ailikuwa na mkewe wa ndoa,huyu ni mwanamke ana mvuto wa hali ya juu na vijana huwaita bomba na sio masikhara alikuwa bomba kweli

Mumewe alichukua mkopo na kumfungulia mkewe stationary ili kuongeza pato la familia,stationary hiyo alifunguliwa mwaka 2010 mwezi wa 9 hivyo ilibaki kama mwezi 1 hivi itimize miaka 4

Picha lilianza pale mkewe na mwalimu huyo kuanza kuchelewa kuja nyumbani na yule mwalimu wakati mwingine alipokuwa anapita kazini kwa mkewe alikuwa anakuta amefunga muda ambao sio sahihi na nyumbani anachelewa kurudi,mumewe akimuuliza hatoi majibu ya kuridhisha

Mumewe yule dada alikuja kuambiwa kuwa mkewe anamahusiano na jamaa mmoja hivi wa Arusha na huyo jamaa huwa anakuja huku kuponda raha mara kwa mara

Ilifikia mpaka mkewe na huyu mwalimu akawa halali nyumbani na kazini kwake haendi

Ndipo jamaa aliamua kumpa kipigo ili aseme huko anakoenda kila uchao,lakini badala ya kusema mkewe aliondoka na baada kama ya dakika 45 alirudi akiwa kwenye gari aina ya toyota vx na kushuka akiwa na yule hawara yake

Waliingia na kumkuta mumewe na yule dada akipika chakula maana alikuwa ni saa 1:45 za jioni na walikuwa na mtoto wa miaka 4, hivyo alikuwa anahitaji kula

Mkewe jamaa alipofika na hawara yake na kumkuta mumewe akipika akasema "umenipiga na kuniuliza nilikokuwa ninakwenda,sasa badala ya kukuambia nimeona nikamlete kabisa mhusika ili ujue na uone wanaume rijali na sio wewe unanitisha na kiststationary chako cha mkopo,kila siku maneno hayaishi,sasa huyu ndo mwanaume sio wewe mwanume suruali,sasa kwa taarifa yako leo ndo mwisho wako wa kuiona naondoka zangu na kama kuna chochote unachonadai sema ulipwe,sitaki unipigie simu wala kunitua sms,na mahari yako uliyowapa wazazi wangu hiyo hapo{huku akiweka burungutu la fedha mezani baadae ilikuja kugundulika kuwa zilikuwa sh 1,500,000,gharama za mahari alizolipiwa wakati anaolewa} na ole wako unifuatefuate kwa chochoye"

Mumewe hukusema kitu na baada ya kimya hicho mkewe aliondoka na hawara yake na kwa sasa wanaishi Arusha

Mwanamke huyu hadi leo ni mwezi umepita na hata hamuulizii mwanae wa miaka 4 aliemuacha huku

Mumewe ameanza maisha mengine na pale stationary ametafuta mfanyakazi!!!

Hayo ndo maisha ya kwenye baadhi ya ndoa!!!!!!!

Mnaoana kwa mbwembwe nyiiingi halafu mnatengana kijinga namna hii???????????
 
sasa mdogo wangu Eiyer kila siku na visa vya wanwake basi uje na vya wanaume basi.

Lkn bora kamuaga mumewe kuliko angetokomea kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Shaaban Dede aliimba hivi mwaka 1980 (JUWATA JAZZ BAND- Msondo)

Nimekumbuka yangu ya dunia
Maneno Baba aliyoniambia
Fukara hapendeki mbele za watu
Hata Kidogo!
​

Kweli tupu hii mkuu!!!!!!!!!!!!!
 
Mkuu Eiyer visa vya ndoa vipo vingi sana na huwezi kusema kuwa kwa kuwa ndoa zina mambo mengi basi watu wasioane au ndoa zisiwepo
Bado ndoa zipo na watu wako ambao wana raha za maisha yao ya ndoa na hawana wasiwasi
naamini kuwa kuna maisha ya ndoa mazuri tuu na shetani akiwa shetani hata siku moja hawezi kubadilika kuwa malaika
 
Last edited by a moderator:
Shaaban Dede aliimba hivi mwaka 1980 (JUWATA JAZZ BAND- Msondo)

Nimekumbuka yangu ya dunia
Maneno Baba aliyoniambia
Fukara hapendeki mbele za watu
Hata Kidogo!
​
Lakini wakati huo, ukimwi ulikuwa haufahamiki... sasa huyu mama enzi zile sijui angefanya kitu gani...??? Maana kumpeleka mume mwenza home...mhnn...
Halafu na wewe mwanaume unakubali tu kwenda, ukiuwawa ....!!!

 

Ni kweli mkuu kuna ndoa zenye furaha sana

Lakini napata wasiwasi kusema ni nyingi

Bahati mbaya ninapoishi imejemgwa nyumba moja mpya ya kulala wenyeji,siku hizi sio za wageni

Na bahati nzuri mhudumu wa pale ninamfahamu

Kila siku kuna wake za watu na waume za watu wanahudhuria pale,kumbuka wengi sio walewale

Wengi wanadai kuwa wamechoshwa na vurugu za majumbani mwao

Hii ni hatari kubwa

Ndoa nyingi ziko chali na nyingi zinavunjika au zitavunjika muda sio mrefu

Trust me!!!!!!!!!!!!
 
gfsonwin mbona hata katika hili kuna kisa cha mwanaume!
ikibadilishwa ingekuwa ni: Hawara mwanaume amrudishia mume wa mtu mahari na kutokomea na mwanamke. sasa anaponda naye maraha Arusha. huku akimshawishi huyo mwanamke kutelekeza mume na mtoto wa miaka minne!

naamini kila stori inatugusa wote wanawake na wanaume ukiamua kutumia macho yote mawili!:wave:

sasa mdogo wangu Eiyer kila siku na visa vya wanwake basi uje na vya wanaume basi.

Lkn bora kamuaga mumewe kuliko angetokomea kabisa.
 

Kweli aiseeee

Halafu huenda huyo jamaa ana mke huko Arusha!!!!!!!
 
Mkuu Eiyer sikatai wengi wa wanaoingia kwenye hizo guest house ambazo siku hizi sio guest tena wanaolala humo ni wake au waume za watu na wengine wanaingia mle bila hata kuwa na ndoa zenye mgogoro
Sio wote wanaoingia mle eti kwa sababu ndoa zao ziko ICU au zinakaribia kuvunjika ila wapo ambao ni hao niliokuambia shetani hata siku moja hawezi kugeuka malaika ni lazima ataendelea na tabia zake na kuwa shetani wa muda wote
Wengine ni wale ambao kwao kula mboga ile ile kila siku wanaona haiwezekani wakati wako viumbe wazuri tuu wanapita hawaachi mfupa kama fisi upite kila siku kiguu na njia guest na vifaa vipya
Ndoa zipo zenye amani na furaha na wapo wanaoishi kwa kujua maana halisi ya ndoa na wapo wale ambao wanafanya mazoezi ya namna ya kuendesha ndoa na hao kila siku ni migogoro
 
Last edited by a moderator:
aseee!!!!!!!!!
ngoja kwanza ntaanza kuweka visa vya wanume humu kama hakukimbia jukwaa.
Hujanielewa gfsonwin, mi sijasema wanaume hawana visa, la hasha, ila vyenu ni vingi na vya balaa... Sasa wewe ukaniletee njemba home, what do you expect..??? Na huyo jamaa alikuwa mstaarabu sana... UNAJUWA KAMA ANGEPELEKWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUPIGA AU KUTUKANA ANGEWEZA TOKA MSHINDI...???
 
Na hao unaofanikiwa kuwaona ni wale usiofahamiana nao... unaowafahamu hawaji maeneno ya karibu na wewe... Wanaenda mbaliii (akiwemo mkeo/mumeo [futa isiyohusika])
 

Kimsingi na uahlisia ni kwamba

wanawake na wanaume wengi wanaishi kimazoea kwenye ndoa zao

Mkuu nakukatalia kuwa kuna mtu ndoa yake ni imara au haina mgogoro halafu akaenda kumvua mwanamke mwingine pichu

Kile kitendo tu cha kwenda huko ni ishara tosha kuwa kuna jambo kwenye ndoa yake

Huwezi kushiba halafu ukasikia hamu ya kula bana!!!!!!!!!!
 
Na hao unaofanikiwa kuwaona ni wale usiofahamiana nao... unaowafahamu hawaji maeneno ya karibu na wewe... Wanaenda mbaliii (akiwemo mkeo/mumeo [futa isiyohusika])

Kwa mtindo huu kesi inakuwa kubwa sana!!!!!
 

Mkuu nakukatalia kabisa ;kuna wanaoshiba na kusaza ila bado wako kiguu na njia kutafuta mpango wa kando na hii sio kwamba kile cha nyumbani hakishibishi
Kinawashibisha mpaka kukinai ila kwa kuwa ashazoea kuwa hawezi kula kile kile kila siku ndio mpango mzima wa kando
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…