Hawa ndiyo watakaoichagua CCM Igunga? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa ndiyo watakaoichagua CCM Igunga?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dullo, Sep 22, 2011.

 1. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  [​IMG]
  Shamrashamra na hoihoi zikirindima katika viwanja vya soko la Mwanzugi Kata ya Igunga Vijijini, baada ya mgombea ubunge wa CCM, Dk. Dalaly Kafumu kuhutubia mkutano wa kampeni jana6. Khadija Kopa wa TOT akihamasisha kwenye mkutano wa CCM eneo la Mwanzugi Kata ya Igunga Vijijini

  [​IMG]
  Mratibu wa kampeni za CCM Igunga, Mwigulu Nchemba akihutubia maelfu ya watu, kijiji cha Mwanzugi Kata ya Igunga Vijijini jana

  [​IMG]
  Maelfu ya watu wakiwa wamefurika kwenye mkutano wa kampeni za CCM eneo la Mwanzugi, Kata ya Igunga Vijijini, jana wakimsikiliza mwanamuziki wa Taarab Khadija Kopa kutoka kundi la TOT.

  MY NOTE: Hawa watoto wanaojzwa katika mikutano ya CCM ndiyo wapiga kura? Au ni kutaka kuwaongopea watanzania kwamba wanajaza watu katika mikutano yao.

  Nawasilisha kwa wanaJF
   
 2. t

  tumpale JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 201
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mtu mzima mwenye akili timamu atakwenda kusikiliza nini kwenye mkutano wa ccm, watoto wanakwenda kusikiliza taarabu
   
 3. HOYANGA

  HOYANGA Senior Member

  #3
  Sep 22, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  naona watoto wengi tu hapo!!! nao wanavitambulisho vya kupigia kura????
   
 4. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Msijekuta wanagawia watoto shahada hao!!!!
   
 5. F

  FUSO JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,878
  Likes Received: 2,343
  Trophy Points: 280
  watoto nyomi wameenda kucheki maigizo ya kina Joti. aiseeee.....
   
 6. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Hivi shule zimefungwa Igunga?
   
 7. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  vuta subira tu, tarehe 2 oktoba 2011 sio mbali sana, tutaona wapiga kura wako wapi. Uchaguzi haishindwi kwa picha za umati mkubwa watu uwe wa watoto wa shule, vijana hata wazee. Uchaguzi unashindwa kwa kura zinapigwa na watu walijiandikisha na ambao wataenda kwenye vituo vya kupiga kura siku ya kupiga kura na kupiga kura zao kwa usahihi. Hayo mambo mengine yote ni ngonjera tu.

  Kwanza naamini kuna watu wengi sana ambao hawaendi kwenye mikutano na mikusanyiko mingine ya kampeni lakini siku ya uchaguzi wanawahi mapema kwenye vituo vya kupiga kura na kutumia haki yao kutoa hukumu kupitia karatasi ya kura na kisanduku.

  Hivyo nasema tena tufute subira kwani wahenga walisema subira yavuta heri
   
 8. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hivi kwanini CCM inatumia 'nguvu' nyingi sana katika jimbo la Igunga?
   
 9. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,099
  Likes Received: 1,276
  Trophy Points: 280
  ..inamaana hata Mh mkapa anawahutubia hao watoto?
   
 10. M

  Maengo JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wameshatoka shule! Hujui mikutano hufanyika jioni?
   
 11. K

  Kipre tchetche JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli ccm maji ya shingo .
   
 12. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wanakwenda na pipi wanawagawia watoto ndiyo maana wako wengi
   
 13. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Taifa la leo ni hao vijana na watoto.
   
 14. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Siyo pipi tu, bali pia masinia ya wali kwa maharage.
   
 15. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanaandaa wapiga kura wa 2050 Baada ya kukaa bench kwa zaidi ya miaka 50 kama chama pinzani wanaandaa mtaji wao
   
Loading...