G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Hawa ndiyo wahadhiri ambao Rais Magufuli aliwatoa pale UDSM kwa mbwembwe ili wamsaidie lakini wote pamoja na aliyewachukua wamefeli. Ajabu ni kuwa pale UDSM walikuwa walimu wazuri sana.
1. Alianza kumvuta Dr. Mussa Mgwatu kutoka Engineering. Huyu Dr. Pale UDSM alisifika sana kwa kuwa eneo la kazi muda wote na kuwajibika. Alimvuta kuwa Mkurugenzi mkuu wa TEMESA ila aliishia kumtumbua baada ya kivuko cha Ukerewe kilichozama Ukara na kuua watu wengi. Kwa sasa naamini atakuwa karudi zake UDSM na anawahi kazini kama kawaida. Aidha alimsaidia sana Magufuli kwenye masomo yake pale UDSM.
2. Dr. Titto Mwinuka: Huyu na Dr. Mgwatu ni marafiki sana na wote walikuwa wanashinda pale workshop za UDSM wakipiga ishu ndogo ndogo za "Fabrications" na walivutwa wote kipindi kimoja aidha wote walimsaidia sana Magufuli wakati anasoma. Huyu ni mkurugenzi mkuu wa Tanesco ingawa ni rafiki yangu sana ila sioni tija anayofanya pale zaidi ya Mramba. Kinachomlinda ni kuwa hajapata janga.
3. Maprofesa Ussoro na Mruma wa CoNAS. Hawa walishiriki kwenye tume za kuchunguza ubadhirifu wa madini na wakaja na ripoti zilizoandikwa na magazeti yote pamoja na kutangazwa live huku tukimshuhudia Prof. Mruma akitokwa machozi wakati akisoma ripoti yake. Ilikuwa mwaka 2016 ila hadi leo hakuna jipya lililotokea na zaidi yale makontena ya makinikia pale bandarini yamejengewe uzio yako pale tu bila kufanyiwa chochote.
4. Prof. Lorence Luoga. Huyu akiwa pale kitivo cha sheria alikuwa mwalimu mzuri sana. Magufuli akamvuta akampeleka kwenye tume alipokuja na ripoti ya kumpendeza akaamua amkabidhi majukumu pale BoT ili akaishughulikie hiyo ripoti. Ajabu hajaweza kufanya hata robo ya kazi aliyoifanya Beno Ndulu huku akiwa Gavana wa kwanza kutumia majeshi ya JWTZ katika kazi zake za kifedha.
5. Prof. Palamagamba Kabudi. Nadhani wengi wetu ni mashahidi kuwa huyu Prof. alikuwa na kiburi sana kiasi cha kuipuuza Law School of Tanzania. Pia kwenye degree yake ndiye mwanafunzi aliyegomea B+ aliyopewa na Mgongo Fimbo akidai kuwa alistahili alama A. Mgongo Fimbo akasema hajawahi kumpa mwanafunzi A maana atakuwa katunga naye mtihani. Pia huyu Prof. Baada ya kuletewa wanafunzi wa TCU kipindi hicho akiwa mkuu wa kitivo aliwatisha kuwa baada ya muda mfupi wale wa TCU wataondoka na watabaki wanafunzi wa UDSM... Alivutwa na Magufuli kuwa waziri wa sheria wakaja vijana wa CCM wakidai eti Lissu amepata mwalimu wa sheria bungeni. Badala ya kumshinda Lissu kwa hoja wakamshinda wa mtutu. Baadaye alihamishwa wizara anayoimudu na kupelekwa ugenini. Kwasasa kwenye vikao vya Baraza la mawaziri ni mwalimu mzuri wa mistari ya Biblia!
6. Prof. Kitila Mkumbo.. Huyu yupo wizara ya maji ila kwa sasa ni mtunzi mkuu wa mapambio ya kumsifu Mkubwa kwenye magazeti.
Pamoja na hayo pia Magufuli ameualia mbali vipaji vya wanasiasa wazuri kama Dr. Slaa (Ambaye kwa sasa kule Karatu akiitisha mkutano hapati hata watu 100), Kafulila, Katambi na wengine wengi.
Waliojitenga naye tunawaona...Au tuseme tena?