CHADEMA haitoi nafasi ya viti maalum kama zawadi na hii inajidhihirisha zaidi na namna inavyowasaidia wanawake jasiri walioshiriki katika mchakaoto wa kukiletea chama ushindi. Tofauti na watani wetu mtu ukiwa viti maalum unakaa kusubiri siku ya kuapishwa. Hebu tuangalie list ya wagombea wa viti maalum wa chadema:
1.Lucy Owenya (Amekuwa mchangiaji na mmoja wa wafadhili wakuu na wakusanyaji hela wa CHADEMA. Ikumbukwe kuwa wafanyabiashara wengi wanaogopa kuchangia chama directly na wanaogopa pia kuchangia kwa Mbowe au Ndesamburo kwa kuwa hawa wanajulikana. Hivyo wako radhi kumpatia fedha Lucy ili aziwakilishe kwenye Chama. Ushindi wa ubunge mkoa wa Kilimanjaro ambako CCM ilikuwa na bajeti ya Bililioni moja umefanikishwa kwa kiasi kikubwa na mchango wa LUCY na Grace Kihwelu).
2.Eather matiko
3. Mhonga Ruhwanya (Chief Strategist kwa kampeni ya Chadema mikoa ya Magharibi. Amempa tough ya kutosha Zito na Mlee wa Kigoma Mjini na wengineo waliogombea mikoa ya Kigoma ambako kulikuwa kugumu mwaka huu kwa kuwa NCCR nayo ilikuwa imewekeza hasa na Chama tawala nacho kilikuwa kimejipanga).
4.Anna Mallac
5. Paulina Gekul (Mgombea mahiri wa CHADEMA jimbo la Babati Mjini. Alipigana kufa na kupona na jabali la Siasa Kisyeri Chambiri na kushindwa kwa kura chache sana. Chambiri alipata 13506 na Pauline alipata 9899
6. Conjesta Rwamlaza
7.Susan Kiwanga
8.Grace Kiwelu (Aliyofanya Owenya ndio aliyofanya Kihwelu. Ametumia utajiri wa familia yake na kujulikana kwao kuleta mafanikia tele kwa CHADEMA)
9. Susan Lyimo (Mbunge wa zamani wa viti maalum na waziri kivuli wa elimu ya juu. Mchango wake kama msomi mchambuzi ulikuwa mzuri na alitetea maslahi ya wananfunzi na walimu katika vyuo. Alikuwa muungwana kuachia jimbo la Kinondoni ligombewe na Mogendi kwa kuwa ilidhaniwa Mogendi angeweza kuleta chachu ya ushindi. Alikuwa miongoni mwa wanamkakati walioshiriki sana kuleta mtazamo chanya wa CHADEMA kwa wasomi wetu).
10. Regia Mtema (Mgombea Mahiri wa Chadema huko Kilombero. Ameshindana kwa nguvu zote na Tapeli la Kimataifa Abdul Mteketa na nusra achukue jimbo kama siyo uchakachuzi wa dakika za Mwisho. (Mteketa alichakachua na kupata 50% ya kura dhidi ya 44% ya Regia - kesi yake imepelekwa Tume)
11.Christowaja Mtinda - Msomi mwenye degree tatu kutoka Mkoa wa Iringa akifundisha Chuo Kikuu cha Mkwawa na mtu anayeshiriki sana shughuli za Chadema huko Iringa na Dar es Salaam: Christowaja Mtinda - WiPaHE Doctoral Scholar, Mkwawa University College of Education
12.Anna Komu - Amepigana vya kutosha CHADEMA Kwanza kama mgombea mwenza wa Mbowe 2005, kama mbunge wa Viti maalum na mwaka 2010 kama Mgombea wa jimbo la Kigamboni. Nusura ashinde lakini uchakachuaji umemponza naye. Amepigana sana na Dk. Faustine Ndugulile wa CCM aliyepata kura 53389 dhidi ya Anna Komu wa Chadema aliyepata kura 25176). Hata hivyo matokeo bado yana mgogoro maana vituo vingi bado havijahesabiwa na wanajeshi walilazimisha matokeo yatangazwe.
13.Mwanamrisho Abama (Mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema kutoka Zanzibar na mgombea wa CHADEMA katika jimbo la Chumbuni huko Zanzibar). Kujitokeza kwanke kugombea jimbo la zanzibar akiwa mwanamke ni ujasiri tosha.
14.Joyce Mukya
15. Naomi Kaihula
16. Chiku Abwao: Huyu ni mpiganaji wa kuigwa mfano na ndiye chachu ya Ushindi wa Mchungaji Msigwa pale Iringa Mjini. Kwa waliokuwa kwenye kampeni ya Iringa watakubaliana na mimi nini kimefanywa na Abwao. Kwa waliokuwepo siku ya utangazaji wa Matokeo watakumbuka nini kilifanywa na huyu mama. Ameshakuwa Mbunge kwa muda mrefu pia.
17. Rose Kamil Sukum - Diwani maarufu wa CCM ambaye siku zote ameuwa mpinzani ndani ya CCM. Alichujwa na Nagu kwa mizengwe na kuamua kugombea Hanang kwa tiketi ya CHADEMA. Pamoja na misukosuko aliyokutana nayo wakati wa kampeni iliyomhusisha mzazi mwenzie Dr. Slaa amepigana mno na kuleta kura nyingi kwa CHADEMA. Jimbo lake nalo limechakachuliwa.Kura 21,986 (Kamili)
CCM 34, 338 (Nagu)
18. Christina Lissu Mughiwa (mdogo wa mpambanaji wa CHADEMA Tundu Lisu na mwanaharakati wa siku nyingi wa CHADEMA. Walikuwa ni wapiganaji walioasi chama Tawala na kwenda upinzani. Kaka yao Alute Mugwahi wakili alibaki CCM na aligombea kura ya maoni CCM na kusindwa na Njau ambaye naye alilipiziwa kisasi na Tundu Lisu. Christina na Tundu Lisu wanategemewa kuichangamsha Singida na kuileta upinzani polepole.).
19. Raya Hamisi (Mjumbe wa Baraza Kuu la Wanawake la CHADEMA na mwakilishi wa CHADEMA Zanzibar. Amesaidia sana kuijenga CHADEMA zanzibar ingawa siasa za kule ni ngumu.
20. Philipa Mturano
Maelezo mengine nitawapatia kesho. Hivyo nategemea kuwa mtaona kuwa Chadema si chama cha upendeleo bali nafasi inatoka kwa merit.