Hawa ndio wanaweza kusema ni Wapinzani wa kweli barani Afrika

Magema Jr

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
1,299
1,201
Taifa hili tangulilipoachwa na muasisi wa wake mwl nyerere bado halijapata mpinzani wa kweli hasa mwenye nia ya dhati ya kuleta mabadiliko ya kiutawala,zaidi ya waganga njaa wenzangu ambao mwanzoni wanajidai kuwa na misimamo, lakini huishia "kuunga juhudi" za serikali.

Vile vile kwa upande wa Afrika,ni mataifa machache sana ambayo kimsingi "nayaona" bayana pengine ndo yenye upinzani makini na wenye tija kwa mataifa yao.

Baadhi ya mataifa na wapinzani hao ni kama ifuatavyo;

1. Malawi - Mch Lazaraus Chakwera
Huyu ni mtu makini kabsa kwa wanamalawi. Nimiongoni mwa wanasiasa wenye moyo wa subira, wapenda amani na kiufupi mchngaji chakwera anapenda kufuata utaratibu. Kumbuka "walimuibia kura" katika uchaguzi, lakini alichukua maamuzi ya busara ya kukata rufaa na siou kuwapambanisha raia na jeshi lao la polisi, ambapo matunda yake amepewa haki yake. Hongera sana
Razaraus.

2. Bob Wine - Uganda
Kijana huyu, anaonekana kumnyima usingizi dikteta Mseveni.Licha ya dikteta kuwa na nguvu ya jeshi lakini bado anaonekana kuzidiwa maarifa na kijana huyu mdogo.

Kinachompaisha Bob ni ujasiri wake, msimamo na kutokulipaza visasi kwa mpinzani wake, kitu ambacho kinamshaliliaha sana dikteta wa Uganda. Japo mh Robert Kagulanyi (Bob wine) kutokutimiza vigezo vya kuwa Rais wa Uganda (kwa vigezo vyangu binafsi)lakini ni miongoni mwa wanasiasa makini sana Afrika.

3. Jusa Jusa - Zanzibar
Ni miongoni mwa wanasiasa wanaopambana kwa hali na mali kuweza kubadili utawala huko visiwani zanzibar. Hiyo imempelekea kuingia katika mkwaruzano na jeshi la polis visiwani humo, ambao waliamua kumpa kipigo, akapelekwa kenya kwaajili ya matibabu. Baada ta kupona ameamua kurudi nchini kwake kwaajili ya kuendeleza mapambano na kuijenga zanzibar (kumbuka kuna baadhi ya wanasiasa wametoroka kwa kigezo hicho hicho) lakini kwa mwanasiasa huyu hali ni tofauti. Jecha ni mzalendo wa kweli na taifa Lake.

4. J Mahama - Ghana
Sote tumeshuhudia jinsi zoezi la uchaguzi lilivyoendeshwa huko nchini ghana.hakuna aliye kuwa anamtukana mwenzake wala hakuna aliyetumia madaraka yake kuvuruga zoezi pa kampeini. Mh Mahama na Rais mteule wa taifa hilo wanaelewa maana halisi ya Demokrasia na kwamba upinzani sio ugomvi. Hongera Mh Ado kwa kuchaguliwa tena. Hongera Mahama kwa kudumisha amani kwa Raia wa hapo Ghana.

5. Elen Johnson - Liberia
Pengine kwakuwa alisomea katika mataifa ambayo ni "baba wa Demokrasia ". Katika kipindi cha ungozi cha mwana mama huyu,ni matukio machache sana au pengine hakuna ambayo yalilipotiwa juu ya kutesa wapinzani wake kws namna yoyote Mama Sales ameliongoza taifa hilo maskini kwa weledi bila mikwaruzano ya mara kwa mara kutokana kuwanyanyasa wapinzani wake. Wapinzani wake pia hawakuthubutu kumkejeli na ama kumbughudhi rais wao kwa namna yoyote.

Afrika ni miongoni mwa mataifa yaliyo na laana kisiasa na kidemokrasia,hasa mataifa yaliyoko chini ya jangwa sahara,lakini baadhi ya mataifa yana "uafadhali" tofauti na mataifa haya yafuatayo ambayo bado nafanya utafiti juu ya aliye "waroga" watu hawa

Congo DR- Felix Tsheked na mwenzake Joseph Kabila "wamerogwa " hawa watu sio bure.

Tanzania- Ufipa na Lumumba. hawa watu sio bure, kunasababu ambayo iko behind the scene
Uganda ya Mseveni, huenda kuna mtu anampa kichwa huyu jamaa sio bure kama wengi ambavyo mnaweza kufikiri.

Kwanini Afrika tusiige siasa na demokrasia za kweli zenye tija kwa mataifa yetu na sio kuvunja Raia miguu, kuchonganisha mataifa yetu kwa wadhamini na wadau wa maendeleo, na kutukanana kila uchwao?

Kwanini tusikubaliane katika kukubaliana na sio kila siku kubeza na kukashfu na kupinga hata mambo ambayo kimsingi hakuna sababu ya kufanya hivyo??


NI MAWAZO YANGU LAKINI, SIKUZUII KUSEMA YAKO AMA KUNIKOSOA ILIMRADI NAAMINI UJUMBE UMEFIKA.

#Jr
 
Jifunze kupenda vitu vyako. Tabia hii ya kulinganisha na kuona kila kitu cha Tanzania ni kibaya ni tabia mbaya sana. Inajenga kutojiamini kulikopitiliza. We ulishawahi sikia mzungu anasifia vya mwengine? Udhaifu na mapungufu yapo kila nchi, na usidhani huko Ghana au Malawi au Liberia hicho ukachokisifia wao wanakiona hivyo.
 
Nchi ya Tanzania inaongozwa na jiwe. Jiwe ni mfungwa wa the Hague aliyevaa kofia ya urais. Siku akiivua hiyo kofia inhiiiiiiiiiiii!!
 
Linganisha na mazingira wanayofanyia siasa zao.

Usijekuta unapambanisha kwa kutozingatia masharti yake

Mazingira ya siasa zao ni sawa?
Sera za vyama tawala ni sawa?
Mitazamo ya walioko madarakani ni sawa?

Elimu ya uraia kwa raia wake ni sawa?

Vyombo vinavyoshughurikia na kusimamia siasa ni sawa?

Ukitoka hapo ndio naweza jikita kwenye hoja zako aseee
Vinginevyo............
 
Hii mada imenichaganya sana. Wewe unazungumzia wapinzani ama aina za serikali zinazotawala Africa! Mtu akitishwa kuuawa unataka akae avumilie kifo ili aitwe shahidi wa siasa ama aitwe mpinzani mzuri?

Nani kama Mbowe aliyefanyiwa yote hayo na bado akitoa hotuba yake wakati wote anaonekana statesman!
Tundu jana ulimsikia akipokea tuzo?

Ni kwa nini mtu akisema ukweli anaambiwa ametukana!

Na kwa nini unadhani kuwa tunahitaji wainzani wazuri lakini hatuhitaji watawala wazuri??
 
Hii mada imenichaganya sana. Wewe unazungumzia wapinzani ama aina za serikali zinazotawala Africa! Mtu akitishwa kuuawa unataka akae avumilie kifo ili aitwe shahidi wa siasa ama aitwe mpinzani mzuri?...
Tuzo ya kinafiki tu hiyo kama hufaham.
 
Jifunze kupenda vitu vyako. Tabia hii ya kulinganisha na kuona kila kitu cha Tanzania ni kibaya ni tabia mbaya sana. Inajenga kutojiamini kulikopitiliza. We ulishawahi sikia mzungu anasifia vya mwengine? Udhaifu na mapungufu yapo kila nchi, na usidhani huko Ghana au Malawi au Liberia hicho ukachokisifia wao wanakiona hivyo.
Nimezungumzia Africa bwashee, so kama umeona nimesifia EU, tafadhali wahi Milembe mkuu
 
Taifa hili tangulilipoachwa na muasisi wa wake mwl nyerere bado halijapata mpinzani wa kweli hasa mwenye nia ya dhati ya kuleta mabadiliko ya kiutawala,zaidi ya waganga njaa wenzangu ambao mwanzoni wanajidai kuwa na misimamo,lakini huishia "kuunga juhudi" za serikali...
Kukuru kakara zote hizi kumkwepa Lissu.

Nyundo ipo pale pale.

Lissu kamatia hapo hapo hadi mataga watapike nyongo.

Huenda ndio ikawa kupona kwao.
 
Dr. John Pombe Joseph Magufuli ni mpinzani namba 1 Afrika, anapambana na wale wasioitakia mema nchi yetu.

Amejitoa kupambana na rushwa, maradhi, ujinga, uzembe na ufisadi. Anapingana na nadharia ya kwamba Afrika ni masikini.

Hakika huyu ni mpinzani wa mfumo unaotaka kutudidimiza watanzania na Afrika kwa ujumla.
 
Kukuru kakara zote hizi kumkwepa lissu.
Nyundo ipo pale pale.
Lissu kamatia hapo hapo hadi mataga watapike nyongo.
Huenda ndio ikawa kupona kwao.
Lissu hamtikisi yeyote labda wana Ufipa wenzake
 
Back
Top Bottom