Hawa ndio wachezaji walioighalimu Yanga dhidi ya Zesco

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,802
Wachezaji pekee ambao wanaweza wasilaumiwe moja kwa moja ni Yondani,Moro, Mitacha Minacha na Mapinduzi. Ila wengine wote walikua na makosa kibao!
1.Ali sonzo. Nakumbuka mpaka mechi inaisha akilipiga cross 2 tu za maana. Matatizo yake ni yale yale hapandishi timu.Anawaza kulinda tu. Siku hizi beki wa pembeni ndio mpga cross
2.Fei toto, Makame,na Banka wanamatatizo yanayofanana. Wanacheza wamerundika km nyanya huku wakipeana pasi vupi vupi bila kwenda mbele. Lakini pia wote hawana speed ili kuupeleka mpira eneo la hatari la adui. Pia hawajui nani akabe eneo la chini na nani apandishe timu mbele hali iliyopelekea mipira mingi kupotea eneo la 18 .
3.Bigilimana.Tofauti na kufunga penati alikua anazurula tu uwanjani. Hakupiga shuti la maana golini hata moja. Hakuna drible ya maana aliyofanya hata moja.
4.Sadney ana mapepe mno,hana utulivu kabsa akiwa na mpira. Sioni cha maana anachomzidi Ngasa mpaka amuweke bechi.
5. Shishimbi. Huyu kwa mtu asiejua mpira hawezi ona makosa yake. Kwangu ndo anaighalimu sn Yanga kwa siku za hivi karibuni. Anapoteza sn mpira tena kwenye maeneo muhimu. Analazimisha kupiga chenga na mwishowe anapolwa mpira. Wakati mwngine anaweza akafanikiwa kupiga chenga,ila pasi yake ya mwisho ikawa hovyooo kabsa!! Jana nusura achomesha baada ya kufanya masihara eneo la 18
Kwa nyongeza , Zahera ameshi dwa kuitengeneza timu. Toka aje Yanga haileweki anafundisha nini, Timu inacheza ovyoo ovyoo haijapata tokea. Bahati ake anapendwa na mashabiki,lakini anastahili kupeba lawama za moja kwa moja. Hayo ndo machache niliyoyaona, karibuni.
 
Tegemea kukosoa makosa makubwa zaidi ya hayo wakienda kukipiga zambia
 
Kwa timu kama Zesco kama ingekutana na timu mbovu kiasi hiko nadhani wasingesubiri mpaka jua limezama kuchomoa goli!! kingine lazima uelewe uwezo wa Yanga na Zesco ukoje kwa game ya jmos Yanga aliingia kama underdog
 
Kweli aiseeeee..
 
Huu siyo wakati wa kumtafuta mchawi. Tusubiri mechi ya marudiano tuone wachezaji na benchi la ufundi watapambana vipi kuhakikisha wanasonga mbele. Tukishindwa kuendelea, bado tuna nafasi ya kuangukia kombe la shirikisho.
 
Back
Top Bottom