Hawa ndio wabunge tutakaowachagua katika uchaguzi mkuu 2020

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,132
7,711
Tangu Octoba 2015 hadi leo hii Februari 2020 ni kipindi kirefu kuweza kufanya tathmini juu ya Mbunge wako katika jimbo lako husika kama anastahili kupewa ridhaa ya kuendeleea tena kipindi kingine au la.

Kwa maoni yangu mimi Mbunge anayestahili kupewa tena ridhaa lazima awe ametimiza sifa zifuatazo:

1. Awe ametatua kero za wananchi angalau kwa asilimia 90, na kero hizo ni maji, afya, barabara, migogoro ya ardhi/wakulima na wafugaji, pembejeo za kilimo, n.k

2. Mbunge aliyeshiriki kikamilifu au aliyeshirikiana na wananchi wake kwa karibu katika kuleta maendeleo ya wananchi wake. Mfano ni kama alivyokuwa marehemu Deo Philip Kunjombe

Naamini vyama husika havito fanya kosa kuwateua wabunge "mizigo" mwaka huu 2020, mwaka huu wananchi hawatochagua suran bali wabunge walio tuletea maendeleo katika majimbo yetu,
mwaka huu wananchi hawato tazama majina wala uwezo wa mtu, bali mtu mwenye mbinu za kutatua matatizo ya wananchi.

Mbunge ambaye hajaonekana jimboni kwake mpaka karibu na uchaguzi tutamtosa.

Watanzania wenzangu kila mmoja amtathmini Mbunge wake wa sasa kwa mafanikio aliyo yaleta katika jimbo lake, tafakari sasa kwa makini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moja taasisi inatumia hela nyingi sana (kodi za wananchi). Kungekuwa na mbadala wake lingefutwa hela ikafanye maendeleo
 
Back
Top Bottom