Hawa ndio wabunge ambao hawatarudi tena 2025, Waanze kubeba virago

Liyan

JF-Expert Member
Apr 7, 2023
300
893
Wafuatao ni baadhi ya wabunge ambao hawatarudi 2025 na waandae kabisa makorokoro yao kabisaaa.

Hii ni kutokana na KUTOKUKUBALIKA NA WANANCHI WA JIMBO HUSIKA, KUTOKUPELEKA MAENDELEO MAJIMBONI MWAO, na kadhalika

Wengine wadau mtazijazia;

1. Mbunge wa UKONGA (Jerry Silaa)

- Huyu ameshindwa kabisa kuweka miundombinu ya barabara kuanzia hapo hiyo barabara ya ukonga mombasa mpka kule moshi bara na kwa diwani barabara ina ma-pot holes kibao imejengwa kwa kiwango cha chini, cha kushangaza hiyo lami haina hata miak 10, barabara za ndani za gongo la mboto ni hovyo, miundombinu ya maji ni zero kabisa, anawaza kuongeza tozo ya tsh 100 kwa wakaz wa dar tu

AAANZE KUFUNGASHA KABISAAAA

2. Mbunge wa Tarime Vijijini (Mwita Waitara)

-Huyu jamaa namkumbuka sana kuanzia miaka ya nyuma sana wakati anagombea uchaguzi wa ndani wa chadema wa kupata mgombea atakayeiwakilisha chama cha CHADEMA kwenye uchaguzi nakumbuka walisimamishwa wagombea watatu na yeye akaibuka mshindi wa kuiwakilisha ukonga kwa tiketi ya chadema kwenye uchaguzi na badae akaamua kuhamia CCM huko Tarime vijijini, hawamtaki na hana ushawishii, Na amekwisha kujijua kuwa hatorudi tena 2025.

AANZE KUAGA

3. Mbunge wa Mikumi. (Jina limenitoka)

- Niliwahi kukaa mikumi kwa mwezi mmoja kwa kazi maalum na niliweza kukutana na wadau mbalimbali ambao katika kubadilishana mambo ya kazi na stori za hapa hapa, Niligundua kuwa wengi wao bado wana imani na PROFESA JAY, na waliuumia kunyan’ganywa ubunge kupitia CHAFUZI za kipindi kile, bado wanampenda na PROFESA JAY ikimpendeza tena na kugombea ataSHINDA. kwa kishindo.

AANZE KUJIANDAAA KUONDOKA BUNGENI

4. Mbunge wa Kawe ( Gwajima)

- Ndugu yangu huyu wala nisitumie nguvu kubwa kueleza chochote hapa ila nadhani kila mtu anajua kuwa huyu jamaa hamna kitu.Huyu alipachikwa baada ya kukatwa jina la mhe..... wa Sisiem lakini yajayo yatatushangaza

ASUBIRI WANA-KAWE WANA JAMBO LAO

5. Mbunge wa Mbeya Mjini(Mwansasu speaker wa bunge)

- Mbeya ilivyoaachwa enzi zile za mbunge wa chadema mpaka leo hakuna maendeleo yoyote ya maana yaliyofanyika.Mbeya itarudi kwa upande wa chama chetu cha Chadema na hilo liko wazi.

Mbaya zaidi ni baada ya kuona vituko kwenye bunge na kuzuia hoja za msingi kujadiliwa kwa mgongo wa kanuni na miongozo ambayo inashindwa hata kueleweka vizuri.Hivi ripoti ya CAG ilishindwa hata kujadiliwa kwa hati ya dharura, kwani wizi na ufisadi si tishio kwa nchi?

MBEYA WATAKUFURAHISHA JUST WAIT

Wengine mtajazia wadau ili wapite hapa wajue kuwa Watanzania tumeamuaa

ni yuleyule
 
Jerry silaa Hana chake mjinga yaani ajitafutie chimbo lake mapema
Kuna yule jamaa wa Arusha.. Kila siku yupo kanisani mara sokoni mara vijiwe vya boda boda...
Kila siku anasema halamshauri ya Arusha kuna ufisadi... Lengo lake ni kujijenga mwenyewe...

Sasa kaambiwa na wewe ni sehemu ya uhusika... Ukiwa kwenye vikao vya ndani husemi... Ukienda bungeni kelele kujitafutia umaarufu...
2025 kazi anayo..
 
Umekosea kwa Waitara maana umeonyesha chuki yako binafsi sababu aliwahama Chadema!

Huna uthibitisho kwamba wananchi wa jimbo lake hawamtaki,bali wewe na Chadema ndio mnaolitaka jimbo lile.
 
Mimi si chadema ila nilikuwa naishi jirani na ofisi za chadema huko ukonga.

enzi hizo nazikumbuka kwasababu tulikuwa tunasali naye waitara kanisa moja.


Acha kuropoka ropoka mkuu
 
Kuna yule jamaa wa Arusha.. Kila siku yupo kanisani mara sokoni mara vijiwe vya boda boda...
Kila siku anasema halamshauri ya Arusha kuna ufisadi... Lengo lake ni kujijenga mwenyewe...

Sasa kaambiwa na wewe ni sehemu ya uhusika... Ukiwa kwenye vikao vya ndani husemi... Ukienda bungeni kelele kujitafutia umaarufu...
2025 kazi anayo..
Kwani anayoyasema ni uongo?
Kama yangekuwa uongo mkurugenzi Pima asingekuwa ananyea ndoo saa hizi!

Gambo bado anatosha Arusha pamoja na bungeni pia.

Ni mmojawapo wa wabunge wallioukataa kutumika!
 
Mimi si chadema ila nilikuwa naishi jirani na ofisi za chadema huko ukonga.

enzi hizo nazikumbuka kwasababu tulikuwa tunasali naye waitara kanisa moja.


Acha kuropoka ropoka mkuu

[mention]voicer [/mention]
 
Kwani anayoyasema ni uongo?
Kama yangekuwa uongo mkurugenzi Pima asingekuwa ananyea ndoo saa hizi!

Gambo bado anatosha Arusha pamoja na bungeni pia.

Ni mmojawapo wa wabunge wallioukataa kutumika!
Ni hivii issue ya Pima ipo kwenye mfumo wa sheria....
Sasa yeye kila siku anairudia hii issue wakati iko mahakamani...
Anairudia makusudi ili ionekane Arusha watu ni wezi na hatua hazichukuliwi...
 
Back
Top Bottom