Hawa ndio wabaya wa Lowassa

Hawa ndio wabaya wa Lowassa

Luno G

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2012
Posts
2,550
Reaction score
1,852
"Lowassa hawezi kupitishwa na CCM kugombea.
Taarifa ambazo kamati kuu ilipewa na kamati ya
maadili na usalama kuhusu mtu huyo hazifai na
hatuwezi kusema kila kitu" - Benjamin Mkapa

"Mimi sasa nina miaka 67. Katika umri wangu
huu kuna baadhi ya majukumu nikipewa
sitaweza. Katika umri wetu huu kuna haja gani
kujiangaisha na kazi za wananchi? Afya yangu si
imara kama zamani. Mimi nafikiri kuna umri
ukifika mtu unatakiwa kuachana na mambo haya"
- Amani Abeid Karume

"Mwaka 1995, Lowassa alikatwa kwa sababu
alikuwa na utajiri usiokuwa na maelezo. Hivi
sasa, Mwaka 2015, utajiri wake ni mkubwa kuliko
aliokuwa nao wakati ule" - Rais Kikwete

"Watu waheshimu viongozi waliomo humu ndani.
Tunao viongozi humu wametumikia Taifa kwa
juhudi na umakini mkubwa, wanaheshimika nasi
lazima tuwaheshimu na tuheshimu uamuzi
uliofikiwa ambao umeshirikisha hawa viongozi
wetu (kwenye Kamati ya Usalama na Maadili)" -
Bulembo

"Kamati Kuu lazima iwe na ujasiri. Mwenyekiti
anazo taarifa zote tena za kina, kwa hiyo lazima
wanazo sababu za msingi za kuleta humu majina
matano " - Maghji

“Tunapata wapi ujasiri wa namna hii wa kutetea
maslahi binafsi? Naona hapa ni mtu kwanza
chama baadaye, si chama kwanza mtu baadaye, Hapa hakuna mwenye taarifa za kina kama
Mwenyekiti. Ni nani huyo mwenye taarifa za kina
kumshinda Mwenyekiti? Tuna imani na uamuzi
wa Kamati ya Maadili” - Mkapa

“Ni lazima tuheshimu kiti. Lazima muwe na
uwezo wa kukubaliana na mambo
yanavyokwenda. Nashangaa watu wapo tayari
kukitishia chama, nguvu hizi za kukitisha chama
mnazitoa wapi?” - Mzee Mwinyi

“Lazima tuheshimu mamlaka, Mwenyekiti anazo
taarifa nyingi. Mimi mwaka 1995 Mwalimu
Nyerere alining’oa na akasema kama nitapewa
nafasi CCM yeye ataondoka, anakwenda
kuanzisha chama. Mimi nikanyoosha mikono na
kujitoa, Mwalimu akanifuata na kunikumbatia” -
Malecela

Raia mwema, Toleo la 414

My take
Hizi taarifa ambazo zimekuwa zikisemwa kuwa mwenyekiti anazo ni taarifa gani hasa?
 
Lowassa mwacheni akapumzike, tusiendelee kumpa presha
 
Kama Mwinyi alikua rais, amiri jeshi mkuu wa majeahi yote ya ulinzi na usalama bado hakujua utajiri wa Lowassa unatokana na nini basi alikua na matatizo. Vile vile kwa kikwete kama hajui utajiri wa Lowassa ana matatizo.

Au hii nchi haina usalama wa taifa?.
 
Mh!Kuna wengine waliingia huko kwa Pesa ya huyo ambaye utajiri wake haujukikani ulipotoka.Na wao kama yeye kwa hakika hawana USAFI walikubali kula yamini wakati wao wanagombea leo ni wabaya na wachafu?Nimeamini metheali hii'Baniani Mbaya Kiatu chake dawa.'Pole Lohassa sikuwa fan wako lakini hukustahili haya.Ni bora adui akuchome kuliko rafiki umwaminiye.

Mzee wangu Lohassa ulichele kuitafakari ile methali kwamba..."Usiamini kila rafiki"Kwa sasa unahitaji afya ya moyo,rudi kijijini utulie ule pension yako.Wasahau waliokuumiza..watoto,mke na familia yakowanakuhitaji zaidi khliko wanasihasa
 
Kama Mwinyi alikua rais, amiri jeshi mkuu wa majeahi yote ya ulinzi na usalama bado hakujua utajiri wa Lowassa unatokana na nini basi alikua na matatizo. Vile vile kwa kikwete kama hajui utajiri wa Lowassa ana matatizo.

Au hii nchi haina usalama wa taifa?.



Madoido tu hayo, wanajuana vyema hao.
 
LOWASSA alibugi 2005 alipompatia nafasi JK. asaahu legacy ya uraisi asahau.... ndo basi tena. Maembe kamwaga ugali lowassa kamwaga mboga na Ma-padlock karamba rosti...... TIA
 
Kama Mwinyi alikua rais, amiri jeshi mkuu wa majeahi yote ya ulinzi na usalama bado hakujua utajiri wa Lowassa unatokana na nini basi alikua na matatizo. Vile vile kwa kikwete kama hajui utajiri wa Lowassa ana matatizo.

Au hii nchi haina usalama wa taifa?.
Kwani hujamsikia Kingunge wakati akiongea na waandishi wa habari, alilalamika sana na kurudia mara kadhaa kuwa mtu wao EL jina lake limekatwa na KITENGO?

Hakufafanua zaidi kueleza hicho kitengo anachokishushia tuhuma nzito ni kitengo kipi.

Lakini kwa circumstantial evidence unapata picha kuwa huenda hicho kitengo alichokilalamikia sana kikawa ni kitengo cha TISS
 
......mla nawe so mfanawe!.....tends wema nenda zako.........ubaya wa rafiki mnafiki.......:car:
 
Hakutendewa haki. Jina lake lingeletwa mbele ya Kamati, wamhoji, wamwambia mabaya yake, halaf ndo wamkate. Lakini hiyo ya mtu kutembea na majina yake matano mfukoni ndo nini?
 
Kiwete ni fisadi no 1,rz 1 utajiri wake hauelezeki wote majambazi wasitudanganye kw wao ni wasafi H M, B M, ssm if tu Haina masilahi kwa tz ife
 
Kama Mwinyi alikua rais, amiri jeshi mkuu wa majeahi yote ya ulinzi na usalama bado hakujua utajiri wa Lowassa unatokana na nini basi alikua na matatizo. Vile vile kwa kikwete kama hajui utajiri wa Lowassa ana matatizo.

Au hii nchi haina usalama wa taifa?.



hivi hao usalama wa taifa ndiyo akina nani? mimi huwa nawasikieni tu mkiwataja humu na hata humu vijiweni. si vibaya mkinifahamisha kuhusu hao jamaa.
 
Wamteteao Lowasa wote ni hamnazo.Haıkuhitajika hata taarıfa ya TISS kubainı kuwa n hatarı kwa maslai mapana ya taifa.
 
Back
Top Bottom