Kihistoria kuna wale viongozi wa kijadi na kimila, ambao wengi wao walikuwa wakipatikana kwa kupendekezwa na wazee au wananchi wenyewe moja kwa moja bila kupitia chama chochote....! Wengine walikuwa wanaandaliwa kwa muda mrefu unaotosha kumsoma vizuri mwenendo wake na matarajio yake dhidi ya matarajio ya wale anaotegemewa kuwaongoza....! Changamoto kubwa ni kwamba, kiongozi bora hutawaliwa na fikra zifuatazo:
- Huwa ni mtu asiyetaka kufeli, na hivyo mara nyingi hutawaliwa na hofu ya kushindwa kuongoza....! hii hutokea kwa kuwa hana kundi lolote linalomuahidi kumlinda hata akiteleza....!
- Huelewa fika kuwa awapo madarakani, rafiki yake ni mnyonge, asiye na sauti, na masikini. Na maadui wake ni wale wenye nguvu, sauti, na matajiri.... hujua kuwa anaenda vitani kupambana na wenye nguvu, sauti na matajiri kwa manufaa ya wanyonge, masikini, na wasio na sauti....!
- Hujitambua kuwa ni binadamu mwenye kukosea, ilhali hayupo tayari kupata hati au historia chafu maishani mwake.... hivyo anaelewa kuwa ni kazi ngumu kujihakikishia hili akiwa kiongozi....!
Kutokana na hayo, basi huwa hapendi kujitokeza kuongoza, lakini akifuatwa na watu na kumuomba awaongoze anakuwa tayari, japo huzungukwa na hofu kwa kuwa hana kundi lolote mwenye ajenda ya siri nayo na hivyo haelewi vema kwa nini watu wamemfuata yeye.... Hii ni kwa sababu mara zote yeye hujifananisha na watu wengine wote na hivyo yeye haoni unique characters ambazo zingemfanya yeye apendekezwe badala ya fulani ndani ya ile jamii....!
Lakini kutokana na busara, hekima na kauli zao, siku zote wanakuwa wakisikika ndani ya jamii hata kama wapo nje ya utawala wa jamii husika...! Ni kwa sababu hii, mara nyingi huweza hata kutumika na viongozi wabovu kwa kujenga urafiki nao, na kupretent kama wao ilimradi tu wafanikishe kupata uongozi wanaotaka kwa maslahi yao....!
Hivyo basi, kama walivyosema wahenga kuwa;
"kibaya chajitembeza, kizuri chajiuza", hata hivyo viongozi wabovu hutembea huku na huko kujitangaza na kujinadi, hata kwa kutoa vishawishi kama vile usafiri, zawadi mbalimbali, vitumbuizo, attractive sitting arrangements, etc. Huku wale bora wakishtukia tu sisimko kubwa likitokea kwa jamii kuonesha kukubalika kwao. Mikusanyiko yao huwa havina gharama zisizo za lazima kama vile maigizo, matangazo ya ziada kuhusu kuja kwao, ulinzi wa kupindukia, nk.
Hivyo, katika kizazi chetu sio kweli kwamba viongozi bora hawapo, bali viongozi hawa ni watu wasiopenda kujitokeza na hivyo kuwa vigumu kupatikana, ilhali wamejaa tele....! Wamefunikwa na kunyimwa nafasi na mifumo inayotumika sasa ya kutangaza nia mwenyewe au kutangaziwa na kikundi fulani cha watu....! badala ya kutangaziwa na jamii yenyewe....!
Haya ni maoni tu....!