mwankuga
JF-Expert Member
- Aug 30, 2010
- 334
- 120
Viongozi wengi wa bara la Afrika ni wahuni na waroho wa madaraka ambao wanatumia kila aina ya udhalimu ili wabaki madarakani kwa gharama ya umasikini wa wananchi.Hamna shaka kuwa watu wengi barani Afrika ni masikini sana,huku watawala wakiishi maisha ya anasa na kugeuza ofisi au Ikulu zao kuwa mapango ya wanyanganyi au madalali wan chi za Magharibi na Marekani.
Kutokana na hali tuliyonayo,kazi kubwa inayotukabili ni jinsi ya kuwapata viongozi bora kuliko kuwaondoa viongozi wabaya.Je,tutawapataje viongozi bora.Kabla sijajibu swali hili,niseme tu kwamba mara nyingi wanasiasa sio viongozi wazuri kwani wengi wao wanakosa personality,moja ya sifa muhimu sana ya kuwa kiongozi bora.
Kwa muda mrefu kuna mjadala kwenye mashule au vyuo na hata mitaani kama viongozi bora huzaliwa ama la.Wachambuzi wengi wa mambo ya kisiasa wanasema suala la uongozi haliwezi kuwa la kuzaliwa pekee.Kiongozi lazima awe na maarifa,ujuzi na uzoefu katika Nyanja mbalimbali za maisha.
Kiongozi au kulongola ni kuonyesha njia na kuijua njia vyema.Uongozi ni kuwafanya watu wengine wakufuate katika kutimiza malengo ya kikundi,jamii au nchi.Kiongozi ni Yule ambaye ana kitu cha kuwafanyia watu wengine katika harakati za kuboresha maisha yao.
Ubunifu na mwono wa mbali ni moja kati ya nguzo kuu ya uongozi.Nia ya kuongoza pekee haitoshi kumfanya mtu kuwa kiongozi bora.Kiongozi lazima awe na maarifa,ujuzi na uzoefu wa kutosha katika mambo yahusuyo nchi au watu.Maarifa na uzoefu lazima viendane na uzalendo kabambe.
Haitoshi tu kuwa na maarifa na ujuzi.Kuwa na maarifa na uzoefu ni suala moja,na kutumia maarifa hayo kwa manufaa ya umma ni suala la pili.Maarifa yanakuwa na maana pale yanaposaidia umma au watu.
Moja kati ya sifa za ndani za kiongozi bora ni kama vile,to be fair (not favour or fear),tabia njema,mpenda amani,mtulivu,mwaminifu,mwenye busara,anayependa kusaidia watu,si mbaguzi,mchapakazi,anayeweza kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati,mtu wa wote,asiyemilikiwa na kikundi chochote,awe na uwezo wa kuwasiliana na watu anaowaongoza,awe tayari kusikiliza pande zote za hadithi kabla hajatoa maamuzi,mkweli na muwazi,asiyehukumu bila ushahidi,awe tayari kukosolewa,awe mcha Mungu n.k
Kiongozi bora hupenda kuwafunza wengine na kuwaanda viongozi wa baadae.Viongozi bora mara nyingi hawapendi kujitokeza hadharani,wengi wao wanaona uongozi ni mzigo.Viongozi bora hawaandai watoto wao au wana familia kushika madaraka.
Viongozi wengi wa Afrika wanatumia vibaya nafasi zao za madaraka kwa kujinufaisha.Mifano ya viongozi wabaya imetapakaa kila kona ya Afrika.Kutoka Capetown hadi Cairo,kutoka Dar es Salaam hadi Dakar,kutoka Abuja hadi Algiers,kutoka Lome hadi Luanda,Kutoka Kampala hadi Kinshasa n.k.
Unafikiri kiongozi bora ni yupi,na tutampataje?Naomba mchango wenu wadau,naomba kuwasilisha.