Hawa ndio mabingwa wa kuropoka bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa ndio mabingwa wa kuropoka bungeni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Alfu Lela Ulela, Apr 28, 2011.

 1. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naanza kwa kuhoji ikiwa katibu wa bunge la Tanzania Thomas Kashilila ana matatizo ktk mfumo wake wa kumbukumbu na fikra. Hii ni kutokana na taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari jana.

  Kashilila anadai wabunge wengi wanaoropoka bungeni ni wageni. Na katika kupigilia msumari hoja yake hiyo mufilisi akatoa mfano wa kauli ya mbunge machachari wa CDM kuwa eti naye aliropoka aliposema "funga mlango tupigane."

  Kupigana kwa tafsiri ya haraka ni kushambulia,kurusha kombora,au miale kwa mtu mwingine. Kushambulia huku hakujatajwa kuwa ni kwa mwili tu, bali hata kwa hoja. Kwa tafsiri hiyo kumbe mtu anaweza KUPIGANA na mtu kifikra (arguments). Yaani kurusha miale au kombora la hoja kwa mwingine ni kupigana bt si kimwili.(kupigana kwa hoja).

  Hivyo basi kwa mtu yoyote mwenye fikra pana hawezi kukurupuka na kudai Lema alimaanisha kupigana kwa maana ya body fighting. Huenda Lema alimaanisha kupigana kwa hoja. Nani ajuaye?

  Hivyo si kweli kuwa Lema aliropoka. Kama Lema hakuropoka ni nani basi aliyeropoka au mwenye tabia za kuropoka bungeni.

  Vinara hawa hapa:
  1.Stella Manyanya
  2.Simbachawene
  3.Ole Sendeka
  4.John Momose Cheyo
  5.January Makamba.

  Nitaeleza kwanini hawa, lakini kwanza tuangalie tafsiri ya neno KUROPOKA.

  Kuropoka kwaweza kuwa ma tafsiri zaidi ya moja.

  Kwanza ni kutoa kauli yoyote ya matamshi na kuingilia maongezi ya msemaji wa awali.

  Pili ni kutoa kauli au taarifa usiyoijua vyema kwa undani wake.

  Eng.Stela Manyanya aliwahi kuropoka bungeni aliposema CHADEMA kinahusika na mauaji ya Arusha kwa kuwa kiliratibu maandamano batili. Kwa kutumia tafsiri ya pili, Manyanya ALIROPOKA.

  Simbachawene aliwahi kuingilia maongezi ya Spika kwny bunge la mwezi february ambapo Makinda alikuwa akitoa mwongozo ulioombwa na Mhe.Halima Mdee. Kwa kuwa Simbachawene aliingilia maongezi ALIROPOKA.

  January Makamba huyu ndio kilaza kbs. Aliwahi kukitetea Kiswahili bungeni, kumbe hata hajui dhima hasa ya kiswahili ktk bunge la Afrika. Akakosolewa waziwazi na waziri Membe. Kwa kuwa January aliongea vitu asivyovijua naye ALIROPOKA.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Imetullia sana makala yako


  Vipi kuhusu wale wanaokaa miaka mitano bila kusikika kule mjengoni???kama vipi waropoke au........
   
 3. shegaboy

  shegaboy JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana kwa hawa wenzetu kuona kuwa wapinzani na hasa CDM wanakosea. ila tuliopembeni tunajua kuwa wakati wa ukombozi umefika ndio maana wanawaandama sana CDM. mara watetezi wa mafisadi, mara waropokaji ila mtaisoma namba tu siku si nyingi hakika
   
 4. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Thanks kwa kuweka sawa kumbukumbu
   
 5. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Na yeye Kashilila KAROPOKA maana kaongea kutetea uozo.ndio maana tumepeleka wabunge wageni wakavunje miiko ya kukaa kimya na kuburuzwa waliyoizoea hao wabunge wazoefu wa zamani
   
 6. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,408
  Likes Received: 1,964
  Trophy Points: 280
  dhana yao ni kwamba ukiwa ccm huropoki na una haki ya kuwatoa nje wabunge wa upinzani hasa cdm hapo mmchelewa yote mnayofanya bungeni kuwakandamiza wapinzani tunayaona kwanza tunawasifu wabunge wetu kwa uchache wao wanafanya kazi iliyo na thamani sana kwetu watz hao wanaopiga makofi kila kitu waendelee kwa wakati wao
   
 7. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Thanx 2 brother. An inteligent is the one who can see the end from the beggining.
   
 8. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asante kwa kuwa umeanza kuuona mwisho wa ccm wile we are at the begging of fighting.
   
 9. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,550
  Likes Received: 612
  Trophy Points: 280
  Bora hata WAROPOKWE!!! Miaka mitano kimya domo linakuwa lime chacha!!
   
 10. N

  NAHUJA JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2011
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,003
  Likes Received: 15,566
  Trophy Points: 280
  Katibu wa Bunge hakusema wapinzani ndio wanaoropoka acheni kujishuku. yeye aliongelea wabunge wapya na hasa vijana. kwani sisiem haina wabunge wa hivyo?
   
 11. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inno nakubaliana nawe kbs kuwa hata Kashilila KAROPOKA.
   
 12. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Usiwafanye Watz wote ni wajinga kama chama chenu. We unaishi dunia gani? Una access na media au huwa unasubiri wengine wafuatilie mambo afu waje kukuhadithia?

  Jana Kashilila kaongea kwa kuonesha kabisa analinda maslahi ya kile chama cha zamani (ccm).

  Na alinukuu kauli ya Godbless Lema, mbunge wa Chadema. Sasa ktk mazingira hayo utasemaje alizungumza kauli ya ujumla? Kwnn hakunukuu kauli ya mbunge wa chama kingine?

  Na kwa taarifa yako, mapambano yanaendelea. Huu si mwisho, wala si mwanzo wa mwisho. Bali ni mwisho wa mwanzo wa Watanzania kuamka and to think rationaly. Watz wa leo sio wale wa mwaka 47 mliozoea kuwaburuza.
   
 13. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kuliko kukaa miaka mitano halafu uje uandikwe kwenya magazeti hukutoa mchango wowote bungeni, ni bora upayukepayuke kama mwehu ili wajue nawe umo!!
   
 14. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #14
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Na ww umeropoka kwani hujui kanuni za bunge vizuri , jivue gamba kwa kuzisoma na kuzielewa ! hansard za bunge zaonyesha Lema ndio alisema funga mlango tupigane - umeropoka pia !
   
 15. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #15
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Doh nawasikitikia sana ccm, mbona bado asubuhi hivi? mengi yanakuja mpaka ukombozi upatikane.
   
 16. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #16
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  CCM ni kama kolokolo la kuvulia samaki...lina vilaza wengi sana kuliko watu makini hata kolokolo linanasa samaki wabovu wengi kuliko wale wazuri wa kufanya kitoweo!
   
 17. G

  Gokona Member

  #17
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili ni tatizo la kuwa na wabunge wanaopenda kupata umaarufu wa haraka kama Lema kuliko kujali maslahi ya watanzania.Mfano mdogo kwamba CDM hakijali maslahi yetu ila wanajiangalia wao maana ukiangalia rasimu ya katiba waliitaka itembezwe nchi nzima maana yetu kodi yetu itumike wakati sisi tunawalipa wabunge mamilioni kwa ajili ya kutuwakilisha kwanini wasingetaka kila mbunge arudi jimboni kwake atembelee kata zake na kutoa elimu lakini wote hao ni wabunge maslahi walitaka posho za kufanya hivyo pamoja na kujenga majina.Bunge lililopita limekuwa la kitoto mno maana ajenda za msingi tunaleta ushabiki wa kisiasa hatutafika mbali maana kazi ya mwanasiasa ni kupata madaraka thats all hana jipya .Tuwe makini sana watanzania wenzangu hatari mbele yetu tuwe wazalendo na tuurudishe uzalendo maana tukitaka kila siku kuwe na fulani ndio awe spika huo ni utawala wa kiimla.Tuwape watu wafanye kazi na kikubwa wanachofanya CHADEMA na hapa simungunyi maneno ni kutaka Mama Anne Makinda ashindwe kufanya kazi kwa kuweka vijembe.Sisi hatujakutuma mbunge ukafunge lamgo au kurushiana maneno kama kwenye taarabu sisi hata kama hubishani tunataka hoja za msingi lakini kwa sababu wamelewa na posho wanajisahau na kufanya bunge ni kama sehemu ya burudani.Acheni utoto na msifanye vijana tukakosa kuaminika maana tumepata shida sana kusemwa vijana ni taifa la kesho tujitahidi kuondoam kauli mbiu hiyo na tukapewa nafasi matokeo yake tunashindwa tunataka kuonyesha kwamba waliotuchagua walikosea.Kitathmini bunge lililopita halikufanya jambo lolote zaidi ya ahadi na wabunge walipumzika.Ukiangalia hata mahudhurio yao wabunge wengi wako busy na biashara zao badala ya kuwepo bungeni.Sasa tunawalipa kodi yetu kuwe na utaratibu wa kuwepo kwenye vikao na kama kuna attendance Register na mtu asipouzulia mara tatu mfululizo onyo hakuna jana ilikuwa hivi na leo jirani ana shida wafanye kama sekta zingine za utumishi wa umma.
   
 18. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #18
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hahahaha kweli Chadema mko hapa JF kikazi zaidi naona mnajaribu kusawazisha Uropokaji wa Lema Bungeni! Kupenda kubaya jamani naona mnatumia hoja za ushabiki Mahaba kutetea Ujinga wa Lema!
   
 19. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #19
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Makala nzuri mkuu,imetuweka sawa.
   
 20. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #20
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duuh! Hii ni aibu kwa mtu anayejiita Genious kuoneshwa wazi kuwa ana utapiamlo wa fikra.

  Napata mashaka kuwa hujui kusoma, au kama unajua basi kwa shidashida maana hukubahatika kwenda Sekondari, achilia mbali kukosa taaluma. Hilo neno hansard yamkini umelisikia kwenye media ma hujui hata dhima na maana yake kisheria.

  Kwani nani amepinga kuwa Lema hakusema TOKA NJE TUPIGANE?? Kwa kuwa una ufinyu wa kufikiri umeshindwa kuelewa thread yangu.

  Nimeeleza vzr kuwa kauli hiyo ilitolewa na Lema. Lakini nikajenga hoja kuwa si sahihi kusema kuwa Lema alimaamisha kupigama kwa maana ya body fighting. Huenda alimaanisha kupigana kwa hoja.

  Sasa wewe bila aibu unapinga kitu usichokijua, UMEROPOKA.

  It's better 2keep quet and people 2think that you are foolish, rather than to speek and remove all doubts. Now, i have no douat that you ard so FOOLISH!!
   
Loading...