Hawa ndio aina ya Makandarasi wetu


Kama wataalamu wetu mmefikia hatua hii basi ni hatari, Inawezekana kweli mimi ni mtu wa kijiweni, lakini sio kwamba sijui..
Tatizo hapa ni kutia siasa kwenye mambo ya kitaalam, na ndio sababu kila siku tunajengewa barabara mbovu,
Iko hivi,
Client anataka kitu ilichokamilika cha world standard
Consultant ndo anawaunganisha
Contractor ndo mwenye dhamana yote ya project, kwa taarifa yako mkandarasi timamu hawezi kukubali kuendelea project ambayo anahisi itamuharibia sifa yake, au hata kumchafulia , kwa kesi ya hii picha, hiyo nguzo halikuwa jukumu la mkandarasi, na kama kweli ni timamu toka siku wanafanya site viewing akiwa na client ilitakiwa hilo swala liwe limeshakuwa wazi kwa kandarasi ili lisiwe kikwazo na kumalizia muda wake ambao pia ni pesa nyingi.

Hivi kwa hii picha , unadhani inamuharibia nani, client au contractor? ,when worse come kama ghorofa yaliyoanguka unadhani mkandarasi anabaki salama,
?
 

hatari hiyo anatakiwa aione client na mshauri wake. Mkandarasi hapo hausiki. Mkandaras hata akiambiwa leo katoe nguzo na hakikisha inasimikwa sehemu sahihi tutakulipa, hapo bila kusita angefanya. Unamuonea bure au hujui majukumu ya 3 -C`s katika tasnia ya ujenzi. Hizo C tatu ni Client-Consultant-Contractor. Kila mmoja ana majukumu yake.
 

una matatizo kuliko hata huyo mkandarasi! wewe ulitaka yeye mkandarasi ndiyo ahamishe hizo nguzo bila malipo?
 
mkuu unamueleza RRONDO kuhusu 3-Cs atakuelewa? labda ungejua kwanza taaluma yake!
 
Last edited by a moderator:
Wewe Client na au Consultant unajua mnawajibika kuwasiliana na TANESCO kuhamisha line ya umeme before contract signing. Urasimu wenu unasababisha nguzo zisihame hadi Contractor anakuwa kwenye full swing site. Naamini hatasubiri urasimu wetu umwingize hasara kisa mjadala usioisha. Kuliko charges atakazowapa kwa kumchelewesha kwa jambo dogo kama hilo ni bora kawachallenge physically.
 

Kesi unayoonglea ni tofauti kaka, kuna dharula zinakubalika sio kila kitu , labda tuseme kokoto aliyotegemea ilikuwa natoka sehemu x, halafu ghafla sehemu hiyo kokoto zikaadimika, hapo mkandarasi anaweza andika barua akielezea hali halisi.kuwa kokoto sasa zinatoka sehemu' y' hivyo naomba kuongezwa muda,

Hapa tunazungumzia nguzo ambayo kimsingi kandarasi aliiona toka siku anafanya site viewing akiwa na client pamoja consultant, unataka kuniambia alianza project bila kuelewa mustakabali wa hiyo nguzo?
 
t blj, site visit wakati wa tendering process ni jambo moja lakini uhamishaji wa miundombinu kama nguzo ni jambo linalomgusa Client moja kwa moja. Mengine ni kama nilivyoeleza hapo juu.
 
Last edited by a moderator:
Ebu nisaidie mkuu tofauti ya engineer na contractor?! samahani

Contractor/Mkandarasi ni kampuni ambayo hupewa comtract/kandarasi kwa mkataba uliowekwa ili kutekeleza kazi fulani. Kama inahusiana na ufundi basi Mkandarasi atajili Engineer/Mhandisi ili kufanikisha kazi hiyo.
 
t blj, site visit wakati wa tendering process ni jambo moja lakini uhamishaji wa miundombinu kama nguzo ni jambo linalomgusa Client moja kwa moja. Mengine ni kama nilivyoeleza hapo juu.

Kaka naelewa unachozungumzia, na kimsingi tuko pamoja, yes clients na consultant wanahusika moja kww moja kutokana na lawama hiyo, post zangu za mwanzo nimesema kuwa mkandarasi mzuri hawezi akasaini contract huku akiacha mwanya wa client au consultant kumcheleweshea kazi yake,
Sad kuna wakandarasi wanafanya kazi kutokana na matakwa na si maomb i ya clients na kwa staili hii maghorofa yatatuanguka sana.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu unapotamka uimara wa barabara unakuwa umezungumza jambo pana zaidi. Sasa mwenzetu kama "umeangalia" huo uimara ungekuja hapa ukatutajia sifa ulizokutana nazo za barabara hiyo katika matabaka yake haya.
  1. Sub grade layer
  2. Sub base layer
  3. Base Course
  4. Wearing Course, ambayo katika picha inaonesha ni surface dressing (Hapa unaweza kutuambia kama ni single au double surface dressing zilizotanguliwa na prime coat materia.
Ukifanya ufafanuzi wa kutosha uta add value kwenye comments zako, vinginevyo lalamikia hiyo nguzo hayo mengine waachie wenye taaluma yao:cool2:.
 
una matatizo kuliko hata huyo mkandarasi! wewe ulitaka yeye mkandarasi ndiyo ahamishe hizo nguzo bila malipo?

alitakiwa asijenge hadi nguzo iondolewe. ila kwasababu ana akili kama zako akajenga na nguzo ipo katikati.
 

kwanini mkandarasi ajenge wakati kuna nguzo?? si angemwambia client aondoe nguzo ndio aendelee...kwangu mimi client na mkandarasi wote wana makosa.
 
ina maana tanesco wamegoma kusogeza....
 

Unapozungumza kuhusu mkandarasi unazungumzia mfanyabiashara. Na kawaida ya mfanyabiashara ni mtu ambaye yuko after profit baasi. Kwenye eneo la upenyo kama huu wa kuchelewa kuhamisha miundo mbinu ndo wakati anapo claim mambo lukuki. Atakuletea bill tu kwamba am on site since.... with the the following resources... na kwa kuwa infrastructure(s) hizi ni obligation zako client na kwa kuwa i have to be on site full time na kwa kuwa schedule yangu ilitakiwa nimemaliza section x y & z na kwa kuwa huna majibu ya kutosha bwana client, basi nasitisha operation till we settle the problem. Concomitant to that jambo hili litanifanya niingie extra cost za ku contain na ku maintain construction equipments. Hivyo basi note kwamba cost hizo utazibeba kama clause zetu zinavyosema. Hii inaitwa "contract games" ku maximize profit bwana t blj. Ndo maana nasema huyo kandarasi wa "mbeya" kawa mzalendo na kawaacha na urasimu wenu. Mtarekebisha mkishatoshana ubishi. Nadhani tunakwenda pamoja sasa.
 
Last edited by a moderator:
mkuu unamueleza RRONDO kuhusu 3-Cs atakuelewa? labda ungejua kwanza taaluma yake!

acha ujinga kuna asiejua client,consultant,contractor ni nini? mimi nimeishia form 2 lakini kiingereza nakibahatisha. mnanipa wasiwasi nyinyi wenye hio taaluma ya ujenzi mnasapoti huyo mkandarasi kujenga na nguzo ipo barabara. ndio maana povu linawatoka ni wabovu acha wachina wapewe kazi.
 
Hii ni hatari kweli! Hapo dreva mlevi atahatarisha maisha yake akigonga hiyo nguzo na nyumba jirani zitaweza athirika kwa shoti ya umeme kama hiyo nguzo itaanguka. TZ kila kitu kinawezekana!
 

kwahio hapa alitakiwa afanye hivyo....ila kwasababu ya 'uzalendo' akaamua kujenga na nguzo ipo ila hakutakiwa kujenga na nguzo.
 
kwahio hapa alitakiwa afanye hivyo....ila kwasababu ya 'uzalendo' akaamua kujenga na nguzo ipo ila hakutakiwa kujenga na nguzo.

Hivi unaujua urasimu uliopo linapokuja jambo linalokutanisha mamlaka na au taasisi zetu kwenye utekelezaji wa miradi?
 
alitakiwa asijenge hadi nguzo iondolewe. ila kwasababu ana akili kama zako akajenga na nguzo ipo katikati.

biashara ya ukandarasi hasa unapo-deal na halmashauri ni ngumu na inahitaji roho ngumu kuifanya! ungekuwa na akili ya kupembua mambo kwa umakini ungetafiti kwa nini aliamua kujenga bila kuitoa hiyo nguzo ya umeme! in short you are a hard headed guy, you can't learn easily!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…