Hawa jamaa vipi?

Hawa jamaa vipi?

Kasiano Muyenzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
13,972
Reaction score
22,922
Nimesubiri makarani waje kuhesabu tupo wangapi kwetu, masaa 12 yamepita sijaona hata mmoja akipita kwangu, nilipotaka jioni ya leo hawa hapa 2 wapo kwa mangi wanapata vichangamshi

Najiuliza walikuwa wapi muda wote huo?

Kesho siwasubiri, imetoka hiyo.

IMG_20220823_182549_003.jpg
IMG_20220823_183135_155.jpg
 
hahahaha noma,
wamehesabu bia na kumwagia moyo, hao wamejichekecha
 
Si wanasema ni zoezi endelevu kwa siku 7
 
Hujafanya poa kurusha picha yao huku, ungeziba sura.
Ustaarabu ni kitu cha bure
Ustaaraabu gan pumbafuuu...yaan watu wamepewa kaz badala wafanya wanazunguka kunywaa beer..na huo ni muda wa mchana kabisaaa..bora ingekuwa jioni tungenyamaza..
 
Hujafanya poa kurusha picha yao huku, ungeziba sura.
Ustaarabu ni kitu cha bure
Wao wenyewe walipaswa kuvua hivyo vikoti vyao, wala camera isingetumika Ila kwa walivyotufanyia leo popote wakiinekana na vikoti vyao camera inawahusu.

Kama wewe imekuboa hiyo action basi jitahidi kuwastua wavue hivyo vikoti baada ya kazi wanawindwa kila kona.
 
katika nchi ya ovyo kila kitu lazima kiende ovyo, wewe ulitarajia nini labda ?. mimi nilipo ziona zile sarakasi zilizotokea kwenye zoezi zima la kuwapata makalani nikajua hakuna cha maana kitakachofanyika hapa ni vile tu tumeamua kuchezea pesa za serikali basiii.
 
I

Inauma sana tunapoona kodi zetu zinatumika isiyo
 
Hujawafanyia sawa mkuu, hakuna kibaya walichofanya hapo
Wangekuwa hawajavaa hivyo vikoti wala nisingewafuatilia, hawa watu wako na bifu kwetu waambie kabisa si kila pub ni ya kupita wakiwa wamevaa hivyo vikoti 😂
 
Back
Top Bottom