Mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani Anachoangalia Ni uwezo wa mtu atakayekuwa na uzalendo wa kuwatumikia watanzania bila kuchoka, pia uongozi siyo umri Wala Rika Bali Ni uwezo wa mtu kuweza kumudu majukumu na kazi fulani kutokana na Elimu na uzoefu alionao mtu
Mtu anaweza kuwa kijana akaongoza vizuri na kuleta matokeo chanya na mifano ya vijana hao Ni mingi tu, lakini pia mtu anaweza akawa kijana akapewa nafasi fulani akaharibu au akaboronga Hadi mteuaji akabaki kushangaa tu na mifano ya aina ya vijana Hawa tunayo pia mingi tu hapa nchini
Lakini pia mtu anaweza akawa mwenye umri mkubwa akapewa nafasi na akafanya vizuri Sana kwa kutumia uzoefu alioupata katika safari yake ya kiuongozi mpaka kufika umri huo, vilevile huyo huyo anaweza akaharibu na kufanya kazi chini ya kiwango mpaka kushindwa kuleta matokeo chanya au tarajiwa,
Mimi Kama kijana naamini mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani anateua watu na watu watateuliwa kuongoza au kushika nafasi fulani kutokana na uwezo walionao wa kuweza kumudu majukumu ya kazi fulani
Ikumbukwe pia kijana wa Leo ndio mzee wa kesho, hivyo kesho yake ya uzee ikifika hatuwezi tukamuacha tu kwa kuwa Ni mzee wakati tunajuwa namna alivyo mchapa kazi na anauzoefu wakutosha katika kazi, hivyo busara uzoefu hekima zinahitajika pia katika uongozi na siyo nguvu tu pekee, Tuangalie sifa za mtu na uwezo alio nao kiuongozi na siyo habari za kusema huyu aliwahi kushika nafasi fulani hivyo asipewe, kufanya hivyo Ni Kama kugawana ulaji badala ya kugawana majukumu ya kuwahudumia wananchi ,mbona hata marekani tunaona wazee wengi tu wakiteuliwa , jiulize hata Joe Biden anamiaka mingapi? Alipata Urais akiwa na miaka mingapi? Vipi ingekuwa huku kwetu? Si tungesema Ni mzee?
Mimi binafsi Nina Imani kubwa Sana na dhamira ya mh Rais wetu mpendwa katika kuijenga Tanzania yetu, Naamini Hateui mtu Kama sehemu ya kumpa ulaji Bali anamteua mtu amsaidie kuwahudumia na kuwatumikia watanzania
Lakini pia nimeona na sote Tumeona vijana wengi tu walioaminiwa na kuteuliwa na mh Rais wetu mpendwa kushika nyadhifa kubwa tu serikalini, Hivi mmesahau hata Yule mkurugenzi wa huko morogoro wilaya fulani ambaye alikuwa binti mdogo kabisa lakini ndani ya muda mfupi kaleta tija kubwa kimaendeleo licha ya kwamba uteuzi huo ulileta maswali Mengi? Naomba Tumwamini mh Rais wetu mpendwa katika dhamira yake njema ya kututumikia watanzania