Madela Wa- Madilu
JF-Expert Member
- Mar 24, 2007
- 3,062
- 731
Ndiyo maana katiba mpya inamapendekezo yatakayotutoa hapa tulipo, mapendekezo ambayo binafsi nayaunga mkono na kuamini kwamba yakifuatwa 90% ya mawaziri watakuwa ni wale walio mahiri katika kazi.
Mawaziri wataomba kazi hizo au watapendekezwa na watu wa kawaida kwa rais.
Rais atawateua Bunge litawahoji umahiri wao ili kuamua uteuzi uhalalishwe au aletwe mtu mwingine kuwania kazi hiyo.
Rais akiteua mtu hufanya hivyo kwa sababu sheria inaruhusu kuteua na ukweli kwamba aliyembali haangukiwi na mti.
Rais halazimishwi kuchagua watu mahiri na wenye uwezo. Elimu ni kigezo lakini si kigezo pekee muhimu. Namna mtu anavyoitumia elimu yake katika kutatua matatizo yake binafsi na jamii ni muhimu hata kuliko ile sifa kwamba amesoma.
Rais mara nyingi huteua timu ya watu wanao mjenga kisiasa, japokuwa anajua fika kwamba timu yake ya mawziri ni lazima iwe na watu wenye uwezo wa kuijenga nchi. Akiwa na timu ya watu wanaomjenga kisiasa ana uhakika wa kuendelea kuwepo msimu unaofuatia, pia anauhakika wa kuendelea kuwa na influensi fulani siku akikaa Benchi.
Mawaziri wenye uwezo wa kuijenga nchi si lazima wawe ndiyo wenye uwezo wa kumjenga MH Rais kisiasa na kumhakikishia KURA na KULA.
Viongozi muhimu kama mawaziri wanatakiwa kuwa wasomi wenye historia ya utendaji wa kazi katika maeneo yao ya utaalamu. Muhimu zaidi ya usomi, wanatakiwa kuwa watu wenye uwezo wa kuona mbele,nia na hamu ya kutatua matatizo mengi ya kiutendaji yaliyolundikana kila wizara.
Elimu ni zana au ni kama NYENGO ya kule kwetu Lilinga(Iringa). Nyengo inaweza kuwa na makali yote lakini mtumiaji akawa si mtaalamu wa kuitumia ipasavyo kwenye Rili Werldi. Kwa mfano Namna anavyoshika mpini wake, Angle anayoiprojecti kwenye tageti, pia Fosi anayo iaplai wakati wa kukata Wihala(Vichaka) nk.
Naamini mama huyu akikubali kuwa mwanafunzi tena anaweza kugeuza mambo katika wizara.
Mimi natambua kwamba,Mtu yeyote mwenye PhD ni mwanafunzi wa kudumu.
Nisahihishwe.