Hawa CUF vipi? Mbona kama wanajipinga wenyewe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa CUF vipi? Mbona kama wanajipinga wenyewe?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Anold, Jun 8, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Nimesikia tangazo kuwa siku ya Jumapili chama cha CUF kitafanya maandamano kuanzia ubungo hadi manzese nafikiri pamoja na mambo mengine ni kupinga hali ya ukandamizaji wa sheria kutokana na ukweli kuwa Mbunge wao Magreth Sakaya aliwekewa vipingamizi na mahakama hali iliyosababisha dhamana yake ishindikane kwa siku 10. Sipingani na hilo maana inaenelewa wazi kuwa sheria kwa sasa zinachagua ni nani kutoka wapi na ni wachama gani, ni mtoto wa nani au ana uhusiano na nani hayo hayana ubishi. Sijajua haya maandamano yanaelekezwa kwa nani hasa kwa maana inaeleweka wazi kuwa CUF wanamuafaka na serikali ya CCM na mzee Seff sharif Hamadi ambaye ndiyo katibu mkuu wa CUF ni makamu wa pili wa Rais Zanzibar ambapo unapotaja serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya mapinduzi inayoongozwa na shein na Hamadi ndiyo haohao. sasa kilio chao cha CUF wanampelekeaa nani sasa? Je Mzee Hamadi naye atajitokeza kwenye hayo maandamano kama katibu mkuu wa CUF ili awashutumu wenzake? hao CUF watakapobeba mabango na kuilaani serikali pamoja na viongozi wake ambao ndiyo visabababishi vya kudhorota kwa haki za binadamu na Demokrasia nchini, Muungano wa CUF na CCM utajitengavipi na laana pamoja na shutuma zitakazotolewa kwa serikali? Naona haya kama ni maigizo yasiyo na viwango! hili limekaaje wana JF?
   
 2. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Waliungana iliviongozi waishi vizuri na kupata uhakika wa ulaji.....haikuwa kwa manufaa ya umma.
   
 3. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Yule mzee katulia hata inzi amguse hawezi kupemba mkono, harafu macho anaangalia kiupande pande kama vile mtu anayeogopa kufumaniwa.
   
 4. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Waswahili wanasema "pilipili zilizoshamba......." Sisi tuhangaike na yetu tuwaachie yao muzee wataona unakijiba.
   
 5. Erick G. Mkinga

  Erick G. Mkinga Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo linakija suala hapa kwamba Mahakama za sasa tofauti na zamani....HAKIKA nakwambia TZ inabadilika,,ila wengi wetu tunategemea mabadiliko ya spidi ya light ndio tatizo,....CUF & CCM wameungana kwa ajili ya maslahi ya wote,...sababu ukisema kwa manufaa yao inabidi urudi kwenye spidi za CHADEMA,.nazo kwa ajili ya nani.....Mbunge kakosea Lazima atiwe ndani,...Acha propaganda,,
  yule alisimamia kesi sio lazima awe CCM,..ni mtendaji wa serikali aliyemaliza Degree UDSM tena alikuwa mwanaharakati,..Nchi inaharibiwa na Wasomi sio Wanasiasa ambao hawazidi hata 1000.:becky:
   
 6. B

  Bolivar JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35

  Utawala wa sheria unafanya kazi kwa wapinzani wa kisiasa tu!
   
 7. k

  kizazi kipya JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nchi inaharibiwa na wasomi wanasiasa pamoja na wanasiasa wasomi ambao hawasikilizi ushauri wa wasomi
   
 8. M

  Marytina JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Hivi Seif Sharif atakuwepo kwenye hayo maandamano??
  ukiwa mpinzani sheria inakupitia
   
 9. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hii mada upuuuuzii mtupu!!!
   
 10. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kinachofaanyika huku hakimhusu Maalim Seif, huu ni mradi wa Lipumba na watu
  wake walio nje ya serikali. usishangae sana mtoa mada.
   
 11. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kubenea amesema CUF wanakumbuka CONDOM wakati mimba imeshaingia
   
 12. A

  Albimany JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Kiongozi mzuri ni yule aupinge uovu hata nyumbani kwake, au ndani ya chama chake au serikali yake.

  watanzania wengi wanafikiria kama wewe ndio maana hatuendelei kwa kulindana,cuf pamoja na kua wako serekalini wanajukumu kubwa zaidi ya kupinga uovu na hiyo ndio nafasi yao kama hawakuitumia itakua hasara kwa.

  lakini chakushangaza mbona na chadema wana madiwani kila kona na madiwani ni watumishi wa serekali au wakiandamana itakua hawaipingi serekali ambayo na wao wamo?

  Sasa nawaelewa wale wafuasi wa chadema waliomchukia Zito aliposema taarifa za rushua ndani ya chadema zifikishwe TAKUKURU. Watu walikuja juu na kumuona zito hasidi,walitaka taarifa zibinywe ili zimalizwe kiundugu.

  Kumbe mulidhani ukiwa kiongozi hutakiwi kupinga maovu ndani ya taasisi yako?
   
 13. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Duh, hii kali. Halafu mimba yenyewe ya shoga!
   
 14. A

  Anold JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Mpuuzi huona upuuzi muungwana huona uungwana, mjinga huona ujinga
   
 15. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wanaandamana si watahatarisha usalama wa nchi na hatimaye nchi isitawalike? Je, CUF wamesahau kauli yao hiyo hadi sasa waamue kuandamana?
   
Loading...