Kuna mawili nimeona hapa:
Labda weye kila mwanamke unayelala naye unajigamba kuwa leo nimekuzalisha na usiitoe hiyo mimba yangu.
Au, huenda wanajua kuwa huwezi lolote halafu unapoenda kuulizia kama mama alipata mtoto, wanakubambikizia.
Why??
Kwa sababu, haiwezekani ugundue kuwa mama wa mtoto anakuchuna tu fweza akiwa na mwingine anayemchuna pia, weye baado uendelee kumtafuta ili umpe fweza za kumlea mtoto ambaye umeshaambiwa sio wako. Hii sijui imekaaje.
Pili, mwanamke gani atakayebeba mimba miezi 12+?? Haya, kasema alilogwa, je mda woote huo alikuwa kishakuambia kuwa ana mimba??
Ushauri;
Ili uwe na amani, kapime DNA. Kuna upimaji wetu wa kienyeji, Mchunguze mtoto, Paji la uso, vidole vya mikononi, nywele na umbo wa uso. Hafaninii kwenu hata kidogo?? Kama ni hapana, nenda kwenye kipimo cha kizungu. DNAtest. Hii ni ghali lakini.
Kipimo kingine;
Mwambiye akupe mtoto ukamlee mwenyewe. Akikubali chukua, mweke mahali wiki 2 hivi, halaf mwambiye aje kumlea mwanaye. Akikubali chukua mkeo, kitanda hakizai haram.