Hali zenu wapendwa! Ni tumaini langu mu wazima wa afya.
Baada ya kuona ushauri wenu hapa JF, nimeona vyema nikawashirikishe mambo yanayoniumiza kichwa:
1. Nilimpata mwanamke mmoja tukaamuwa kuwa wapenzi na lengo la kuishi kama mke na mme.
Nilimtolea mahali, akawa ni mjamzito. Alidai kuwa ujauzito ni wangu, jambo ambalo sikupingana nalo na ndo nikaamua kumtolea mahali.
Alikuwa akibadilika mara kwa mara, ikafikia hatua nikaongea na ndugu yake mmoja, ndo nikagundua kumbe tunamsheya wanaume wawili.
Alikuja kukili mwenyewe kwamba ana mwingine, na ameshamwambia mimba ni ya kwake.
Mara alidai mimba yangu niilee, nikafanya hivyo mpaka mtoto ana miaka 3 sasa, ila cha ajabu sasa hivi hata picha ya mtoto nikiomba sipewi mtu anaishia mitini.
Huyu mtoto ni wangu niendelee kuhangaika hivo hivo au niachane nae tu!
Na je, vipi nikiacha na kwa badae naambiwa mwanao! Si ntakuwa nimemuumiza mtoto!
Nikizingatia nilivokua natafuta litoto la kike mwishoe ndo yamekuwa hayo!
2. Baada ya mda hapo kuachana na huyu mwanamke, nilikula tunda sehemu. Ilikuwa tarehe 1-01-2014.
Tarehe 25-09-mwaka huo, niliweza kuwasiliana na huyo mwanamama (hapo kati kati nasikia aliendaga Uganda na kupotezana) akaniambia ni mjamzito.
Nilimuuliza Hivi, mimba hiyo ni ya kwangu? Alijibu: Nadhani. Nilisubiri mtoto atazaliwa, hapo hela natoa, mpaka alikuja kujifungua tarehe 18-01-2015.
Nilichukulia poa tu, ila sasa, mwanamke kawa jeuri, safari za hapa na pale, cha ajabu anadai kabla ya kujifungua alikuwa amelogwa hivyo anaenda kupata dozi; kama kweli au la hayanihusu haya; shida yangu ni hii, hasa kwenu wale mliojaliwa kupata familia au wenye ujuzi na swala hilo; huyu mtoto atakuwa wangu?
Maana kila naeongea nae anadai mtoto hawezi kuishi tumboni mda wote huo!
Mpaka madaktari wa wanawake waliniambia hivo, nae anasisitiza mtoto ni wa kwangu; wakati mwingine ana kiburi sijapata kuona; anadai hata nisipojiskia kumsaidia niache mtoto atakuwa tu.
Naombeni ushauri wenu.