Hawa askari wamepata mafunzo ya aina moja?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,314
72,740
Hawa ni askari wa Tanzania
ImageUploadedByJamiiForums1466397167.835134.jpg

Hawa ni Askari wa Nchi nyingine
ImageUploadedByJamiiForums1466397239.903648.jpg

Nimehitaji kujua kwani wafanyayo ni tofauti kwa raia.
 
Askari wa bongo ni kama vile wanashauku itokee vurumai kidogo tu ili waanze kupiga watu. Wamejengwa kiuonevu zaidi kuliko kiutetezi. Mfano dhahiri mtu akienda kukushtaki kituoni, wewe mshtakiwa hupewi nafasi ya kujitetea. Automatically unachukuliwa ni muhalifu, ni ngumi, teke na rumande. Ukweli ukija kujulikana hata samahani hupewi. Hii ndio Tanzania yetu yenye amani na utulivu.
 
Mungu ANAKOSEA?! Duh!

Acha kukufuru.

Aliumba kila kitu kikiwa kikamilifu, tofauti inakuja kwenye MACHAGUO yetu. Tulichagua kuishi hivi.

Tusimsingizie Mungu hata kidogo.
Mimi ni mkristo mzuri tu, tena sana . Najiuliza haya mapungufu aliyonayo mwafrika ni ya Mungu? Kama Mungu aliyaweka kwa waafrika, basi alifanya kosa kutuumba na mapungufu haya! Kama ni ya kwetu baada ya kutuumba wakamilifu, basi atuangamize tuipishe dunia!
 
Askari wa bongo ni kama vile wanashauku itokee vurumai kidogo tu ili waanze kupiga watu. Wamejengwa kiuonevu zaidi kuliko kiutetezi. Mfano dhahiri mtu akienda kukushtaki kituoni, wewe mshtakiwa hupewi nafasi ya kujitetea. Automatically unachukuliwa ni muhalifu, ni ngumi, teke na rumande. Ukweli ukija kujulikana hata samahani hupewi. Hii ndio Tanzania yetu yenye amani na utulivu.
Concept ya POLICE, ililetwa na Wakoloni. Kazi yake ilikuwa ni ipi? Kudhibiti waafrika wasifanye "fujo" waweze kutimiza malengo yao ya kuja hapa. Malengo yapi : KUTUTAWALA AND THE PROCEEDS FROM THEREOF
 
Yani bado tunatumia methods za colonial police za kukandamiza umma jeshi la polisi la sasa na ukoloni tofauti yao ni ss hivi tunakandamizwa na watanzania wenzetu ila jeshi na mbinu ni zile zile za kikoloni kikosi cha FFU kilianzishwa na wakoloni tumepata uhuru bado jina ni lile lile na linatumika kutuliza sauti za wananchi wanapodai haki zao hii nchi mabadiliko yanayotakiwa sio ya kisiasa tu hata taasisi za ulinzi kama hawa polisi zibadilike kimfumo wengi wanaoenda polisi ni waliofeli form 4 na 6 na wale ambao jamii imewatenga unadhani watatetea haki za raia??
 
We acha kuchukulia picha moja tu kuhalalisha chuki yako dhidi ya nchi yako, na hawa je, wamepata mafunzo gani?
1466399051452.jpg
1466399056716.jpg
 
Mimi ni mkristo mzuri tu, tena sana . Najiuliza haya mapungufu aliyonayo mwafrika ni ya Mungu? Kama Mungu aliyaweka kwa waafrika, basi alifanya kosa kutuumba na mapungufu haya! Kama ni ya kwetu baada ya kutuumba wakamilifu, basi atuangamize tuipishe dunia!
Ha ha ha! Anawapa nafasi ya kubadilika.
 
Mimi ni mkristo mzuri tu, tena sana . Najiuliza haya mapungufu aliyonayo mwafrika ni ya Mungu? Kama Mungu aliyaweka kwa waafrika, basi alifanya kosa kutuumba na mapungufu haya! Kama ni ya kwetu baada ya kutuumba wakamilifu, basi atuangamize tuipishe dunia!

Kosa letu siyo kuwa weusi,kosa letu ni kukosa viongozi,kuukosa umakini na kuukosa uzalendo au UTAIFA ndani mwetu.Tumejikuta tunajiwekea wigo wa umimi,choyo na wale wenye kutafuna nchi wameamua kuweka wigo wao wakiitumia polisi.

Na sababu hatuna viongozi bali watawala wenye sifa moja kubwa KUUA UCHIMI wa mataifa yao.Tumuangalie Mugabe,amejisheheneza kwa utajiri ilhali watu wake wakikosa huduma bora za kijamii,uchumi ukiwa unadorora lakini ona yeye na viongozi wa chama chake wakijilimbikizia mali na kuwatishia wananchi huku wakiudanganya umma eti wapinzani wanapata nguvu toka nje kuhujumu uchumi.

Watawala hawaoni tena,wapo tayari kuua ili kuendelea kutawala,tunaona Sudan ya Kusini Uganda na Kenya ni yale yale,wakishaanzisha vita wanakimbiza familia zao kwenda ughaibuni wakijifanya wanatafuta suluhu huku wakikaa kwenye mahoteli makubwa wakifadhiliwa na mataifa makubwa,niwalaani wote wanaowarudisha nyumbani Afrika watawala waliosababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini kwao.

Ninashangaa Umoja wa Mataifa unashindwa kuonya nchi husika kabla vita haijatokea,wanasubiri tuuane ndipo waje mbio inatia hasira sana.Bara langu la Afrika tuko busy kuwapa wazungu raslimali zetu kwa kuua raia wetu wasiojua au wasio na elimu.
 
Kumbe alituumba wakamilifu. Tumemkiuka Mungu, tu wa nini duniani?
 
Wewe jichunguze, usihusishe dhambi zenu na mivurugano kumkufuru Mungu.
Vyote viliumbwa na Mungu! Lazima nimuhusishe. Ondoa neno kukufulu, ukiliendekeza hutahoji lolote kuhusiana na Mungu! Unahoji kupata maarifa na si kukufuru
 
Umehoji nini hapo zaidi ya kumhukum Mungu kuwa alikosea kumuumba mwaafrika!!! Je, una upeo kiasi gani wa kumhoji mwenyezi Mungu!? Jiulize alivyovifanya vizazi mpaka leo vinaendelea unafikiri wewe na Mungu mko kundi moja kiasi cha kuwa na ujasiri na jeuri ya kuhoji au kumkosoa?
 
We

we hatuwezi kudebate, hutaki kuhoji, kwa heri, siko hivyo mimi nakwambia!
 
Back
Top Bottom