Hausigeli anayedaiwa kuwa mchawi abwaga manyanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hausigeli anayedaiwa kuwa mchawi abwaga manyanga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Feb 18, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 41,980
  Likes Received: 37,263
  Trophy Points: 280
  JANA gazeti hili liliandika taarifa za hausigeli Odillia Mikka (16), binti anayedaiwa kufanya vitendo vya kishirikina nyumbani kwa mzee Naftali Chacha jijini Dar es Salaam.

  HATIMAYE hausigeli anayedaiwa kuitikisa nyumba ya Mzee Naftali Chacha kutokana na kufanya ushirikina akishirikiana na bibi yake wamejikuta wakirejesha amani ya kuishi kwa upendo na majirani baada ya kupewa dawa ya kuwasafisha ili kuondokana na vitendo hivyo.

  Hatua ya wanakijiji cha Simangulu mkoani Morogoro walifikia uamuzi huo baada ya hausigeli huyo kukiri hadharani kuwa yeye pamoja na bibi yake wamekuwa wakifanya ushirikina na kuwaua watu.

  Mbali na familia hiyo, wanakijiji wengine watatu waliokuwa wakishirikiana nao, ambao wamebainika kujihusisha na vitendo hivyo, nao pia wameondolewa uchawi na kupewa onyo kali ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha iwapo watarudia kufanya vitendo hivyo.

  “Nimeshuhudia eneo la tukio wanakijiji wakifanya tambiko ambapo wazee wa jadi walitoa dawa na kuwapa washiriki wote wa vitendo hivyo kisha kuwapa masharti mazito ya kuacha kuendelea na ushirikina huo,” alisema Sabato Naftal, kaka mkubwa wa mtoto wa tajiri aliyekuwa akiishi na hausigeli huyo jijini Dar es Salaam.

  Wakiwa kwa wazee wa jadi hausigeli pamoja na washiriki wengine waliwataja watu waliowaua kijijini pale na kukubali kwenda kuwatoa msukule kisha kuwarejesha kuwa hai.

  Baada ya kumaliza operesheni hiyo baadhi ya wanakijiji waliwataka washiriki hao kuhama katika kijiji hicho na endapo wataendelea na vitendo vyao wapo tayari kuwachomea nyumba zao.

  Mwanzoni mwa wiki hii familia ya mzee Naftali Chacha wa Ukonga Mazizini ilijikuta ililazimika kumrejesha hausigeli wao nyumbani kwao Morogoro baada ya kubaini kuwa anajihusisha na vitendo vya kishirikina.

  Familia hiyo ililazimika kuchukua hatua hiyo baada ya kumkuta hausigeli huyo akisota ndani ya ungo chumbani kwao huku akiwa ameweka nguo za msichana mkubwa wa mzee huyo ambaye alidai kuwa bibi yake anataka damu yake amuue.

  Baada ya mahojiano makali na msichana huyo alikiri kuhusika na vitendo hivyo ambapo alidai kuwa anashirikiana na bibi yake ambaye anaishi mjini Morogoro na kwamba si mara yake ya kwanza kuua.

  Tajiri huyo alilazimika kwenda kituo cha Polisi Stakishari kutoa taarifa ambapo inadaiwa kuwa kuna baadhi ya dawa zilichomwa kituoni hapo ambapo binti huyo alidai kukabidhiwa na bibi yake kwa ajili ya kuiwangia familia hiyo.

  Hata hivyo baada ya mahojiano makali msichana huyo alirejeshwa nyumbani kwao ambapo mambo yalizidi kupamba moto kwa hausigeli huyo kuwafichua baadhi ya watu anaodai kushirikiana nao katika vitendo hivyo.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 41,980
  Likes Received: 37,263
  Trophy Points: 280
  source: darleo
   
 3. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  mmmh uncle mara huyu ana miaka 15 leo 16,lkn uncle ww si mwandishi wa habari kweli?unanipa wasiwasi sana
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 41,980
  Likes Received: 37,263
  Trophy Points: 280
  Kwanini unawaogopa waandishi wa habari wakati silaha zao ni kalamu na karatasi?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...