Hausigeli akutwa akiwanga kwa tajiri

front20pix.jpg

Mfanyakazi ya ndani anayedaiwa kuwanga akiwa katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungu (UBT) tayari kusafirishwa kurejeshwa kwao Morogoro baada ya tuhuma hizo za kuwangaAbambwa na ndumba kibao na ungo
  • Asimulia mambo ya kutisha
  • Maombi yasaidia kumnasa
VITUKO simanzi vimetawala nyumbani kwa Mzee Naftal Chacha (60), mkazi wa Ukonga ambaye ni mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), baada ya hausigeli wake, Odillia Mikka (15), kukutwa chumbani kwake akiwanga huku akiwa amekaa ndani ya ungo.

Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza katika nyumba hiyo baada ya mtoto wa mwenye nyumba hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Miriam Naftal kumkuta msichana huyo akiwa amechuchumaa ndani ya ungo uliosheheni ndumba kibao pamoja na nguo za ndani za mtoto mkubwa wa kike wa familia hiyo.

Miriam baada ya kuingia katika chumba hicho ghafla alianza kupiga mayowe kumshtua msichana huyo ambapo familia nzima iliyokuwamo ndani ya nyumba hiyo iliingia chumbani huko ili kujionea kinachoendelea.

Baada ya kufika umati wa watu walimshuhudia hausigeli huyo akiwa ameshikwa na butwaa na walipomhoji alidai kuwa amechukua nguo za ndani za msichana wa mwenye nyumba huyo, Bhoke Naftal, ili azipeleke kwa bibi yake anataka kumuua kwa kumuweka msukule.

Kutokana na kauli hiyo mwenye nyumba hiyo ambao ni Wasabato walianza maombi ndipo hausigeli huyo aliyefikia nyumba hiyo Desemba 24, 2009, alipoanza kujieleza mambo mbalimbali anayoifanyia familia hiyo kwa kushirikiana na bibi yake anayeishi kijiji cha Kitete mtaa wa Yangeyange Morogoro.

Hausigeli huyo alidai kuwa tangu afike katika nyumba hiyo bibi yake amekuwa akija usiku na hutembelea vyumba vyote vya nyumba hiyo na kuichezea familia nzima.

Amesema kazi hiyo aliinza tangu akiwa na umri wa miaka minne ambapo mafunzo hayo aliyapata kwa bibi yake ambapo tangu aanze amefanikiwa kumuua mtoto mdogo wa miaka miwili wa tajiri yake mmoja anayeishi Morogoro ambaye hadi sasa wamemuweka msukule.

Ameongeza kuwa alimuua mtoto huyo aliyekuwa na umri wa miezi mitatu ndani ya nyumba hiyo. Baada ya kukiri kufanya kitendo hicho, wanafamilia ya mtoto huyo walimpiga na kumtimua kazi bila ya kumpa hata senti tano.

Akizungumza na gazeti hili, hausigeli huyo amesema mara baada ya kufika katika nyumba hiyo bibi yake alikuja usiku na kumuomba damu ya Miriam Naftari (25), mtoto wa mwenye nyumba hiyo ambaye alikwenda kumchukua Morogoro bila kumuaga.

Amesema kuwa usiku huo alijitahidi kumnyonya damu dada huyo aliyekwenda kumchukua lakini jitihada zilikwama kwa kuwa dada huyo alikuwa ameokoka.

Kutokana na hali hiyo, bibi akaamua achukue nguo za dada mkubwa wa familia ya Mzee Naftal ili wamtoe kafara ambapo ilitakiwa afe jana ndipo aliamua kuchukua nguo ili amkabidhi bibi yake huyo.

Msichana huyo amedai kuwa akiwa kwenye maandalizi hayo ndipo Miriam alipogundua kisha kupiga kelele kabla ya yeye kutimiza azima yake. Kwa hiyo familia iliamua kuchukua uamuzi wa kumfikisha kituo cha Polisi Stakishari kwa ajili ya hatua zaidi ambapo kulifunguliwa kesi namba STK/RB/ 2520/2010 iliyoripotiwa jana.

Akizungumza na gazeti hili, baba wa familia hiyo, Mzee Naftal, amesema anamshukuru Mungu kwa kuwa familia hiyo ni ya watu wenye kumcha Mungu kwani tangu hausigeli huyo afike katika nyumba hiyo kulikuwa na mabadiliko ndani ya nyumba hiyo ikiwa ni pamoja na homa za watoto zisizokwisha.

Amesema kuwa wakati mwingine walikuwa wakilazimika kukesha kwa ajili ya maombi kutokana na kuchoka na vituko vinavyotokea mara kwa mara usiku.

“Kwa kweli ilikuwa ni hali ya kutisha kwani kila baada ya siku mbili mtoto anaumwa mara huyu kesho huyu lakini hatukuacha maombi ambayo ndiyo yametoa majibu,” amesema.

Habari hii itaendelea kesho ambapo tutawaelezea zaidi kuhusiana na namna ambavyo hausigeli huyo alikuwa akiifanyia familia hiyo na pia jinsi alivyokuwa akitumia ndumba na utaalam wake wa kurusha ndege hewani usiku.

Tumsifu yesu Kristo daa!!! Dunia imekwisha sasa hawa mahousegeli tutawapata wapi? Kwani mtu unayemuachia mtoto ndo mchawi ok tutazidisha maombi kila Housegeli akija kwangu lazima aokoke kama hataki kwako
 
WOS: tukikubaliana na wazo lako la kuandika kitabu ni vyema basi ukawaalika na wadau andamizi wa majamboz hayo. Maana unakubaliana nao.mwalike yahya shee useni,mapaka paka,na wote uwajuao but mie kwa hilo naomba niwe wa mwisho kuamini. Angalia bint mwenyewe alivyojazia pengine ana ujauzito wa mwenye nyumba na ktk kuua soo limeundwa hilo. Wajemeni tuangalieni na upande wa pili wa fweza.mweeee mi simo
 
We Ngala... nilipoanza kusoma post yako... I was disturbed kidogo maana nilikuwa nashindwa ku link nilichoshauri on documentation na mimi kukubaliana na hao unaowaita wadau! Ila niliposoma hapo kwenye bold ya blue nikakuelewa na nikarejea amani yangu niliyokuwa nayo.

Nadhani tuko masafa tofauti sana.
Mimi naongelea research and documentation on a social issue, wakati wewe unaongelea blah blah tulizozoea kila siku....

ofcourse ukiamua ku document moja ya methodology inaweza kuwa kuwapata hao wadau wako ili usikie maelezo yao na haina ubaya!

Im sure unajua kuna fani kama anthropology na sociology ambazo hujaribu kutafuta kuelewa maisha ya watu , tabia zao na kwanini hufanya mambo fulani fulani, nk. Wako watu ambao wameshafanya utafiti sana kwenye suala hili na siyo kitu cha ajabu sana hadi kifanye watu kama wewe kukataa kuandika!
 
Haya mambo ya kuajili watu wa ndani ni tabia ya kuwafanya watumwa na pia kuna haja ya serikali ya kukataa mambo ya ajabu na kutunga sheria za kuwafanya watu hawa kuacha kufanya hivi na kutaka watumishi wa ndani wanataka na kupata haki zao za kila siku juu ya maisha yao. Na pia tabia ya ushirikina ni tabia ya mtu binafsi
 
Mkuu hapa sasa umenena.
Mtu anayefanya kazi ya kulea watoto na kutunza nyumba, anatakiwa awe mwenye kuweza kujitetea kwa kila hali - kiumri, kiakili n.k.Tatizo la watanzania wengi wenye kuajiri housegirls ni ama hawana uwezo kulipa mishahara ya kuridhisha na kwa vile hawataki mabishano huishia kuajiri wasichana/vijana wadogo wasio na uwezo hata wa kujitetea kupata mazingira bora ya kazi.Umasikini uliokithiri hupelekea kuongezeka kwa demand na supply.Endapo ingetungwa hiyo sheria ( which is very unlikely ukizingati kuwa hata maboresha ya mishahara yaliyofanyika chini ya sheria mpya aya ajira 2004 hayawahusu watumishi wa ndani) ungeshuhudia kupungua sana kwa watu wenye kuajiri housegirls na houseboys.
Binafsi naamini katika kutoa ajira decent na kwa watu wenye uwezo hasa kiumri.Sifagilii kabisa ajira za hawa mabinti au vijana wadogo maana
 
Kazi ipo! Ina maana amepelekwa polisi ili ashitakiwe kwa kosa la kufanya Ushirikina?. Lakini nafikiri hakuna sheria inayohusu mambo ya kishirikina.
 
<i>
front20pix.jpg

Akizungumza na gazeti hili, hausigeli huyo amesema mara baada ya kufika katika nyumba hiyo bibi yake alikuja usiku na kumuomba damu ya Miriam Naftari (25), mtoto wa mwenye nyumba hiyo ambaye alikwenda kumchukua Morogoro bila kumuaga.
Amesema kuwa usiku huo alijitahidi kumnyonya damu dada huyo aliyekwenda kumchukua lakini jitihada zilikwama kwa kuwa dada huyo alikuwa ameokoka. (bjbj - source pls) Uchawi upo jamani hata kwenye bible imeandikwa lakini nguvu ya maombi ndio mhimili pekee wa kuweza kusimamia.
 
Sue,
HATA MIMI HAPO NDO NIMECHOKA KABISAAAAAA! KAKIRI MWENYEWE..WATU WANAANZISHA TOPIC OHH mahausigel wanaonewa, wananyimwa mshahara na waajiri! Mbona hii topic tofauti?

Ndugu yangu BAK na wengineo, Suala hapa ni vitendo vya kihuni na vya kijinga vya hawa watu vinazungumziwa.Haina maana ati kwa vile kuna wanaonyanyaswa basi maovu yao mengine yasizungumziwe na watu wasijue kinachoendelea.

Suala la imani hizi za kijinga za kishirikina hufanywa na baadhi ya hawa watu ..si Tanzania tu bali hata sehemu nyingine duniani. Nadhani mwaka jana kuna tukio liliripotiwa kwenye vyombo vya habari ambapo hausegeli huko asia sikumbuki ni nchi gani alimpikia mwajiri wake chakula akachanganya na menstrual blood kwa imani ati asifukuzwe kazi na boss ampende! Issue hapa siyo kuamini..bali ni utovu wa adabu wa hawa watu na imani chafu za kishirikina!

Ndugu yangu Mbu..nakuelewa sana na hata mimi sifagilii imani hizi..ila nashindwa kuelewa iweje tuogope kukemea vitendo hivi kwa vile tutaonekana washirikina?

...Wos,

Ni kweli hawa watumishi wa ndani wengi wanavitendo na matendo ya ajabu pia, lakini bado na mashaka na hiyo confession ya huyu anatuhumiwa ni mwanga!

Hata Rama aliyekutwa na kichwa cha mtoto "kaachiwa huru", ...
Kuna walakini hapa.
 
jamani tudumishe kusali katika familia zetu nimefikiria sana housegirl wangu mpaka naogopa. Mungu nisaidie
 
Mchezo wa Kuigiza huu!

Kwahiyo maombi ndiyo yameitika hiyo juzi?

Nadhani Hela ya kulipa mshahara hamna halafu pia yawezekana "kuna kijana ndani ya nyumba hiyo ka-mla!"

Au, hizo zana ni za Familia hiyo na imetokea kuwa mtoto amezigundua! Mbona tunapata visa kila siku vya Wazazi kuwatoa watoto kafara?
 
Haya mambo ya kuajili watu wa ndani ni tabia ya kuwafanya watumwa na pia kuna haja ya serikali ya kukataa mambo ya ajabu na kutunga sheria za kuwafanya watu hawa kuacha kufanya hivi na kutaka watumishi wa ndani wanataka na kupata haki zao za kila siku juu ya maisha yao. Na pia tabia ya ushirikina ni tabia ya mtu binafsi

Mkuu usisahau kumuomba Mungu akunusuru haya mambo yapo.
 
front20pix.jpg

Mfanyakazi ya ndani anayedaiwa kuwanga akiwa katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungu (UBT) tayari kusafirishwa kurejeshwa kwao Morogoro baada ya tuhuma hizo za kuwangaAbambwa na ndumba kibao na ungo
  • Asimulia mambo ya kutisha
  • Maombi yasaidia kumnasa
VITUKO simanzi vimetawala nyumbani kwa Mzee Naftal Chacha (60), mkazi wa Ukonga ambaye ni mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), baada ya hausigeli wake, Odillia Mikka (15), kukutwa chumbani kwake akiwanga huku akiwa amekaa ndani ya ungo.

Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza katika nyumba hiyo baada ya mtoto wa mwenye nyumba hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Miriam Naftal kumkuta msichana huyo akiwa amechuchumaa ndani ya ungo uliosheheni ndumba kibao pamoja na nguo za ndani za mtoto mkubwa wa kike wa familia hiyo.

Miriam baada ya kuingia katika chumba hicho ghafla alianza kupiga mayowe kumshtua msichana huyo ambapo familia nzima iliyokuwamo ndani ya nyumba hiyo iliingia chumbani huko ili kujionea kinachoendelea.

Baada ya kufika umati wa watu walimshuhudia hausigeli huyo akiwa ameshikwa na butwaa na walipomhoji alidai kuwa amechukua nguo za ndani za msichana wa mwenye nyumba huyo, Bhoke Naftal, ili azipeleke kwa bibi yake anataka kumuua kwa kumuweka msukule.

Kutokana na kauli hiyo mwenye nyumba hiyo ambao ni Wasabato walianza maombi ndipo hausigeli huyo aliyefikia nyumba hiyo Desemba 24, 2009, alipoanza kujieleza mambo mbalimbali anayoifanyia familia hiyo kwa kushirikiana na bibi yake anayeishi kijiji cha Kitete mtaa wa Yangeyange Morogoro.

Hausigeli huyo alidai kuwa tangu afike katika nyumba hiyo bibi yake amekuwa akija usiku na hutembelea vyumba vyote vya nyumba hiyo na kuichezea familia nzima.

Amesema kazi hiyo aliinza tangu akiwa na umri wa miaka minne ambapo mafunzo hayo aliyapata kwa bibi yake ambapo tangu aanze amefanikiwa kumuua mtoto mdogo wa miaka miwili wa tajiri yake mmoja anayeishi Morogoro ambaye hadi sasa wamemuweka msukule.

Ameongeza kuwa alimuua mtoto huyo aliyekuwa na umri wa miezi mitatu ndani ya nyumba hiyo. Baada ya kukiri kufanya kitendo hicho, wanafamilia ya mtoto huyo walimpiga na kumtimua kazi bila ya kumpa hata senti tano.

Akizungumza na gazeti hili, hausigeli huyo amesema mara baada ya kufika katika nyumba hiyo bibi yake alikuja usiku na kumuomba damu ya Miriam Naftari (25), mtoto wa mwenye nyumba hiyo ambaye alikwenda kumchukua Morogoro bila kumuaga.

Amesema kuwa usiku huo alijitahidi kumnyonya damu dada huyo aliyekwenda kumchukua lakini jitihada zilikwama kwa kuwa dada huyo alikuwa ameokoka.

Kutokana na hali hiyo, bibi akaamua achukue nguo za dada mkubwa wa familia ya Mzee Naftal ili wamtoe kafara ambapo ilitakiwa afe jana ndipo aliamua kuchukua nguo ili amkabidhi bibi yake huyo.

Msichana huyo amedai kuwa akiwa kwenye maandalizi hayo ndipo Miriam alipogundua kisha kupiga kelele kabla ya yeye kutimiza azima yake. Kwa hiyo familia iliamua kuchukua uamuzi wa kumfikisha kituo cha Polisi Stakishari kwa ajili ya hatua zaidi ambapo kulifunguliwa kesi namba STK/RB/ 2520/2010 iliyoripotiwa jana.

Akizungumza na gazeti hili, baba wa familia hiyo, Mzee Naftal, amesema anamshukuru Mungu kwa kuwa familia hiyo ni ya watu wenye kumcha Mungu kwani tangu hausigeli huyo afike katika nyumba hiyo kulikuwa na mabadiliko ndani ya nyumba hiyo ikiwa ni pamoja na homa za watoto zisizokwisha.

Amesema kuwa wakati mwingine walikuwa wakilazimika kukesha kwa ajili ya maombi kutokana na kuchoka na vituko vinavyotokea mara kwa mara usiku.

“Kwa kweli ilikuwa ni hali ya kutisha kwani kila baada ya siku mbili mtoto anaumwa mara huyu kesho huyu lakini hatukuacha maombi ambayo ndiyo yametoa majibu,” amesema.

Habari hii itaendelea kesho ambapo tutawaelezea zaidi kuhusiana na namna ambavyo hausigeli huyo alikuwa akiifanyia familia hiyo na pia jinsi alivyokuwa akitumia ndumba na utaalam wake wa kurusha ndege hewani usiku.

lakini mkuu bujibuji mbona stori zako nyingi huwa zinahusiana na ushawi au na wewe ni mdau?
 
hii mijitu ndio imekuwa laana kubwa kwa familia zetu.
sijui miafrika tufanyeje ili uchawi uondoke miongoni mwetu?
 
lol, masiki weeeee, she is too young to do so!

respect mkuu pape....tuambie umri sahihi basi...au mpaka afikie umri wa yule aliyenaswa na cctv akimwaga unga mweupe kule mjengoni?????????
 
leo nimeamini uchungu wa mwana aujuaye msasi..mweee.uchungu wa huyu binti aujuaye ni yule mama aliyemzaa kwa uchungu lkn sie wengine watoto ni wale tuliozaa tu!!loooh sijazaa bado lkn hamna maneno yeyote yatakayonifanya niamini huyu mtoto ni mchawi!!!hata akikiri mbele yangu bado sitaamini na nitaendelea kulia naye sbb..i mean.we r talknig about a child here..a child..miaka 15 akipigwa kofi 1 tu la kijeshi na huyo mwanajeshi mstaafu si anaweza hata kukiri kuwa anajua osama alipo!!!!najua kuna uchawi na biblia imeandika kua upo lkn kama hao watu kweli ni watu wa maombi hata huko kuumwa umwa kwa watoto wao kusingekuwepo na tena mungu angewapa ishara siku ile ile ya kwanza kuwa wasiruhusu huyo binti kuingia malangoni mwao kwani ni mchawi..lkn hapana..wamesubiri kawafanyia kazi zaooo weee labda walikua hawamlipi madeni yamekua makubwa au baba kamlala ndio sasa mtoto anakiri uchawi na kupelekwa polis central akajibu tuhuma za kumuwangia mjeshi mstaafu..kwanza angekua analipwa na kua treaded vizuri asingeonekana kama anavyoonekana pichani..picha nzima hiyo inanuka manyanyaso aliyokua akifanyiwa mtoto na hao walokole..afrika vituko,vioja,aibu na mateso kwa wanyonge hayataisha leo..imani hizi siziiti tena potofu bali naziita HATARISHI kwani ndizo zilizomwaga damu nyingi ya albino,wazee wenye macho mekundu,na watu wanaofia kwa makarumanzara sbb yakutopelekwa hospitali,etc.nachagua kua upande wa huyu mtoto na hata kama niko wrong poa tu lkn ndivyo moyo wangu unavyojisikia.h
 
queenkani tuko pamoja, kisa hiki kinafanana sana na visa vingi vinavyoendelea kati ya wasichana wa kazi na waajiri. Mara nyingi kama msichana hakutuhumiwa kutoka na baba mwenye nyumba, ataambiwa mwizi na sasa hili la uchawi ili asipewe haki zake pamoja na kazi ngumu walizofanyishwa. Kuna mama mmjoa alikuwa anachukua msichana anakaa nae kwa majaribio kwa mwezi, kisha anamwambia huwezi kazi anamuondoa anachukua mwingine bila kuwalipa maana wapo kwa majaribio!

Kuhusiana na hii kesi nimeshindwa kuelewa ujasiri wa huyu mjeshi wa kwenda polisi kumshitaki mtoto wa 15 na akakiri alikuwa amemuajiri - hii ni sawa na kwenda polisi kulalamika umeibiwa bangi! Huwa najiuliza, unajisikiaje kumfanyisha kazi mtoto wa miaka 15 huku una mabinti zako wakubwa kuliko haka katoto wamekaa wanaangalia Sex and the City kutwa kucha? Halafu tunalalamika ndoa hazidumu, what a joke, mabinti hawaandaliwi kuishi maisha halisi, wanaishi maisha ya tamthilia...

Annina
 
....Huyu mtoto inawezekana ameonewa au ni kweli amefanya huo uchawi.Baadhi ya hawa wasichana wa kazi wana vituko vyao jamani.
....Kuna binti alikuwa msaidizi wa kazi kwa sista, huyu binti naye alikuwa anaamini sana nguvu za giza......alikuwa amevaa vitu vya ajabu nadhani wanaita hirizi. Sista ni mtu wa imani sana, alivyoletewa msichana akawa anaenda naye kanisani.Siku moja kukatokea kitu cha jabu sana, kanisani kulikuwa na maombi ya nguvu, yule binti akawa kama anapiga makelele na kuongea vitu vya ajabu.Mchungaji akamuuliza matatizo yake, ndipo hapo yule binti akaelezea jinsi alivyokuwa analindwa na nguvu za giza na kwamba amevaa hirizi kiunoni.

Alisema kwamba kuna hirizi alipewa na baba yake huko kijijini ni kinga inamlinda usiku na kuwaona wachawi. Mchungaji alimuombea yule binti na baada ya maombi yule binti akaamua kumpokea Yesu na kukubali zile hirizi zichomwe moto. Hadi leo amekuwa ni msichana mzuri na anaendelea kumsaidia sista.

.........Inawezekana kweli huyo binti alikuwa naye na nguvu za giza, lakini walichofanya hao kumpeleka polisi wala sio vizuri. Wangemuweka kwenye maombi na hizo nguvu za giza zote zingeteketea kwa jina la Yesu na yule binti angebaki tu hapo kwao kuendelea na kazi.
 
Maswali ni mengi kuhusu jinsi ya kukomesha utumwa wa kisasa (aka ma-housegirl)
Hivi hakuna sheria inayosema huwezi kumuajiri mtoto chini ya miaka 18? Kama ipo kwanini chama cha mawakili wakike haki chukui hatua kutetea haki za wanyonge kama haka kabinti? Kabla ya ku-deal na uchawi huyo aliyeajiri mtoto wa miaka 15 anatakiwa afunguliwe mashitaka.
 
Back
Top Bottom