Hausigeli akutwa akiwanga kwa tajiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hausigeli akutwa akiwanga kwa tajiri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Feb 15, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 41,934
  Likes Received: 37,181
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mfanyakazi ya ndani anayedaiwa kuwanga akiwa katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungu (UBT) tayari kusafirishwa kurejeshwa kwao Morogoro baada ya tuhuma hizo za kuwangaAbambwa na ndumba kibao na ungo

  • Asimulia mambo ya kutisha
  • Maombi yasaidia kumnasa
  VITUKO simanzi vimetawala nyumbani kwa Mzee Naftal Chacha (60), mkazi wa Ukonga ambaye ni mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), baada ya hausigeli wake, Odillia Mikka (15), kukutwa chumbani kwake akiwanga huku akiwa amekaa ndani ya ungo.

  Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza katika nyumba hiyo baada ya mtoto wa mwenye nyumba hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Miriam Naftal kumkuta msichana huyo akiwa amechuchumaa ndani ya ungo uliosheheni ndumba kibao pamoja na nguo za ndani za mtoto mkubwa wa kike wa familia hiyo.

  Miriam baada ya kuingia katika chumba hicho ghafla alianza kupiga mayowe kumshtua msichana huyo ambapo familia nzima iliyokuwamo ndani ya nyumba hiyo iliingia chumbani huko ili kujionea kinachoendelea.

  Baada ya kufika umati wa watu walimshuhudia hausigeli huyo akiwa ameshikwa na butwaa na walipomhoji alidai kuwa amechukua nguo za ndani za msichana wa mwenye nyumba huyo, Bhoke Naftal, ili azipeleke kwa bibi yake anataka kumuua kwa kumuweka msukule.

  Kutokana na kauli hiyo mwenye nyumba hiyo ambao ni Wasabato walianza maombi ndipo hausigeli huyo aliyefikia nyumba hiyo Desemba 24, 2009, alipoanza kujieleza mambo mbalimbali anayoifanyia familia hiyo kwa kushirikiana na bibi yake anayeishi kijiji cha Kitete mtaa wa Yangeyange Morogoro.

  Hausigeli huyo alidai kuwa tangu afike katika nyumba hiyo bibi yake amekuwa akija usiku na hutembelea vyumba vyote vya nyumba hiyo na kuichezea familia nzima.

  Amesema kazi hiyo aliinza tangu akiwa na umri wa miaka minne ambapo mafunzo hayo aliyapata kwa bibi yake ambapo tangu aanze amefanikiwa kumuua mtoto mdogo wa miaka miwili wa tajiri yake mmoja anayeishi Morogoro ambaye hadi sasa wamemuweka msukule.

  Ameongeza kuwa alimuua mtoto huyo aliyekuwa na umri wa miezi mitatu ndani ya nyumba hiyo. Baada ya kukiri kufanya kitendo hicho, wanafamilia ya mtoto huyo walimpiga na kumtimua kazi bila ya kumpa hata senti tano.

  Akizungumza na gazeti hili, hausigeli huyo amesema mara baada ya kufika katika nyumba hiyo bibi yake alikuja usiku na kumuomba damu ya Miriam Naftari (25), mtoto wa mwenye nyumba hiyo ambaye alikwenda kumchukua Morogoro bila kumuaga.

  Amesema kuwa usiku huo alijitahidi kumnyonya damu dada huyo aliyekwenda kumchukua lakini jitihada zilikwama kwa kuwa dada huyo alikuwa ameokoka.

  Kutokana na hali hiyo, bibi akaamua achukue nguo za dada mkubwa wa familia ya Mzee Naftal ili wamtoe kafara ambapo ilitakiwa afe jana ndipo aliamua kuchukua nguo ili amkabidhi bibi yake huyo.

  Msichana huyo amedai kuwa akiwa kwenye maandalizi hayo ndipo Miriam alipogundua kisha kupiga kelele kabla ya yeye kutimiza azima yake. Kwa hiyo familia iliamua kuchukua uamuzi wa kumfikisha kituo cha Polisi Stakishari kwa ajili ya hatua zaidi ambapo kulifunguliwa kesi namba STK/RB/ 2520/2010 iliyoripotiwa jana.

  Akizungumza na gazeti hili, baba wa familia hiyo, Mzee Naftal, amesema anamshukuru Mungu kwa kuwa familia hiyo ni ya watu wenye kumcha Mungu kwani tangu hausigeli huyo afike katika nyumba hiyo kulikuwa na mabadiliko ndani ya nyumba hiyo ikiwa ni pamoja na homa za watoto zisizokwisha.

  Amesema kuwa wakati mwingine walikuwa wakilazimika kukesha kwa ajili ya maombi kutokana na kuchoka na vituko vinavyotokea mara kwa mara usiku.

  "Kwa kweli ilikuwa ni hali ya kutisha kwani kila baada ya siku mbili mtoto anaumwa mara huyu kesho huyu lakini hatukuacha maombi ambayo ndiyo yametoa majibu," amesema.

  Habari hii itaendelea kesho ambapo tutawaelezea zaidi kuhusiana na namna ambavyo hausigeli huyo alikuwa akiifanyia familia hiyo na pia jinsi alivyokuwa akitumia ndumba na utaalam wake wa kurusha ndege hewani usiku.
   
 2. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  lol, masiki weeeee, she is too young to do so!
   
 3. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  naona huruma tu watu kuajiri watoto wadogo..hayo mengine mmmh isije tu kuwa gea ya kutaka kumnyima binti haki zake.
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,852
  Likes Received: 22,943
  Trophy Points: 280
  bongo burudani kila siku...
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  Feb 15, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Boss na wewe kila sehemu uko wewe,mpaka kwa mahouse girl..haya bwana jirushe jukwa ni lako.
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,734
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 180
  ...na kweli! inasikitisha sana...
   
 7. Typical

  Typical JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 268
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  duu kuna watu wanaishi miasha ya ajabu sana!

  inashangaza mno.
   
 8. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,378
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  ni kweli lakini ni afadhari sana kuliko kuwaka tamaa mitaani, maana kuna wadogo kuliko huyo ambao wanapanga foreni maeneo ya Buguruni ili wajitumikishe kwa Ngono....tuombe Mungu ndivyo serikali ilivyotengeneza mazingira kwa mtoto wa kike
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 0
  ENEO LA AJIRA ZA MAHAUSGELI LINAHITAJI RESEARCH YA KINA!
  Kuna mengi sana kuhusu hawa watu ( siyo wote) hadi sasa hayajawekwa bayana japo yapo sana.

  Hawa watu japo huwa ni msaada na necessary evil huweza kusababisha madhara makubwa hasa ya kisaikolojia kwa watoto na wakati mwingine hudumaza maendeleo ya watoto.

  Huyu wa familia ya Naftali kwa bahati nzuri amekamatwa peupe.Hebu pateni picha ni hofu iliyoje kwa watoto wetu kuwa na hawa watu more than 14hrs wakati mwingine.. fikiria mwanao mdogo unayempenda sana analala chumba kimoja na mchawi usiku kucha.. ukiacha mateso ya hapa na pale....kuna sasa ushirikina! Kila nikifikiria hii ishu nasisimkwa mwili.

  Ingewezekana tukaanzisha mjadala wa vituko na vimbwanga vya hawa watu nadhani tungejipatia kitabu cha kutosha na huenda mauzo yake yangetunisha mfuko wa JF!
  Invisible...kazi kwako..huu ni mradi tosha!
   
 10. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,378
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,464
  Likes Received: 117,260
  Trophy Points: 280
  Nami nakiona hicho hicho huyu binti sidhani kama kafikisha hata umri wa miaka 15. Inasikitisha sana lakini kwa kweli hawa wafanyakazi wa ndani nvhini wananyanyaswa sana na waajiri wao kwa namna moja au nyingine.
   
 12. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,378
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  unadhani tufanyaje ili kuwasaidia?
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,464
  Likes Received: 117,260
  Trophy Points: 280
  Ni Serikali kusimamia ipasavyo ajira za hawa Wafanyakazi wa ndani ili kuhakikisha wanatendewa haki. Sasa Serikali yenyewe Mhhhhhh! yenyewe haiwatendei haki wananchi wake je itaweza kuhakikisha haki za hawa zinalindwa!? I doubt it!
   
 14. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  mi nakwambia kaka sikia tu hivi hivi juu juu lkn mateso wanayopitia hawa watoto ktk majumba ya baadhi ya matajiri hayabebeki moyoni.kwa kweli hawathaminiwi kabisaa.hata hivyo mateso haya yanasababishwa na viongozi wetu maana madogo zetu kama hawa walitakiwa wakafanyie fujo darasani lkn wanaishia uchokoraa na ktk majumba ya watu huku wakikosa haki yao muhimu ya kuufaidi utoto wao.
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  na sisi wabongo uchawi umekuwa uchawi loh hatari kweli kweli ,mambo mengine yanachekesha
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Feb 15, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,734
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 180
  WoS bana,
  hebu weka pembeni imani za kishirikina. Katika karne hii na usomi ulokuwa nao bado unatishika na visa vya 'vimbwenelehi?'

  ...Ubaya tunauanza wenyewe sisi waajiri! Wengi wetu huchukulia kwakuwa kaajiriwa kama "MTUMISHI" wa ndani, basi si haki yake kujua masaa yake ya kazi, si haki yake kulala kabla ya waajiri, si haki yake kulala masaa ya kutosha, si haki yake kula chakula wanachokula wanafamilia, wala kula nao mezani, na mengineyo katika hayo...

  Ubaya tunauzanza wenyewe, "umleavyo ndivyo akuavyo..."

  ...ofcoz ndugu yangu, unadhani angekuwa anapatiwa malezi mazuri huko alikoajiriwa angekuwa na hali mbaya kiasi hiki? ndio kusema katika kipindi chote cha ajira wameshindwa hata kumnunulia raba mtumbani au begi la nguo kiasi kwamba arudi kwao na 'mfuko wa mchele'

  ...Kama hiyo familia kweli wanaishi kiroho, wangesaidia kumpa mafunzo ya kiroho huyu binti ili abadilike hivyo wanavyomtuhumu!

  Hii kesi ni ya kusingiziwa, kama kawaida yetu waajiri kuwatafutia sababu tu waajiriwa ili tuwanyanyase. Ipo siku, 'what goes around comes around'
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,464
  Likes Received: 117,260
  Trophy Points: 280
  Yaani nakwambia nimejionea Bongo baadhi ya waajiri wanavyowanyanyasa wafanyakazi wa ndani hadi unakasirika. Maana kwanza wanafanyishwa kazi kwa masaa chungu nzima kwa siku kati ya 16 au hata zaidi. Hawana haki ya kula chakula anachokula muajiri na familia yake, labda kama kuna mabaki. Mishahara wanayolipwa hailingani kabisa na masaa chungu nzima wanayofanyishwa kazi kwa siku. Halafu bado manyanyaso ya hali ya juu ambayo waajiri hao wanasahau kabisa kwamba wale wafanyakazi wao ni binadamu pia na hivyo wanastahili kupewa heshima yao badala ya kuwa treated kama wanyama au hata kuliko wanyama. Siamini kabisa huyu binti wa miaka 15 anaweza kuwa ni mwanga.
   
 18. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,734
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 180
  ...Bro, huwezi kumtuhumu mtu kuwa ni Mwanga unless nawe ni "mwanga!" Huyo Binti Mlokole anajinsi yake ya kuwanga ndio maana amejaribu na kufanikiwa kuitengeneza 'sinema' hii...

  Thanks God 'mob justice' haikuchukua mkondo wake, maana sehemu nyingine wangempiga kibiriti bure huyu binti wa watu. So long as ana kwao, Mwenyezi Mungu atamfungulia tu njia...
   
 19. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Hivi kima cha chini cha mshahara wa house-girl Dar ni liasi gani? Je, kazi zake zinatambuliwa na sheria zetu? i.e muda wake wa kufanya kazi nk. wapi anapata chakula chake? na mambo mengineyo kama umri wa mfanyakazi nk.
   
 20. Suzzie

  Suzzie Member

  #20
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Hivi jamani kwani si amekiri mwenyewe kuwa ni mwanga na ametumwa na bibi yake?
  Na pia amethibitisha kuwa ameshafanikiwa kuua mtoto huko morogoro?
  Sasa mnamtetea nini au amelazimishwa kusema hivyo?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...