Haujakaa Uswazi!!!

The Finest

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
21,605
6,071
Kama haujawahi kucheza kombolela
Kama haukuangalia "The Hard Way" , mniga aliliwa na mamba
Kama hauwezi kuimba "**** kina kaaloki.....Na Jimmy, acha acha hilo gitaa..ahaaahaaa aya madiscoooo dansa
Kama haujacheza kombolela usiku
Kama ya Arnold ya jini (terminator)haujaiona kwenye kibanda cha sinema
Kama haujawahi kudandia gari halafu likaongeza kasi ukashindwa kuruka halafu unashushwa 5Km away
Kama haujawahi kukimbia na kumtosa mshikaji baada ya kudondoka juu ya mti na kuumia
Kama haujapiga chabo
Kama haujagombea ndege zinazopita angani
Kama haukupigwa kwa kuwatia vidole watoto wenzako na kuchungulia wamevaa chupi ya rangi gani
Kama haujawahi kuchonganisha majogoo hadi yakapigana
Kama siku ya kuogesha mbwa haujasababisha wakadandiana
Kama haujawahi kucheza mchezo wa kujipikilisha na baba na mama
Kama haujachungulia dirisha la jirani kuangalia video
Kama haujawahi kwenda shule na fagio la chelewa na kidumu cha maji
Kama haujawahi kugombania kusukuma baisikeli za viwete ili uingie uwanjani bure

Endeleza na wewe......

Wikiendi Njema
 
umenitabasamisha.

Hasa hapo penye kupiganisha majoo + ng'ombe + mbwa.

Siku ya kuogesha mbwa, manjikusanya kama 50 hivi.

Afu kombolela na rede na msita.

Kuchungulia video kwa mwarabu lol
 
Chagulaga ni kiboko ya mambo..........................LOL
Halafu kuna ile kuwek kioo chini ya miguu ya mabinti ili kuchungulia c.h.u.p.i
 
Pia kuna ule mchezo wa ana ana anado..........................Malizieani basi
 
Mdako ndio msita.

Afu kulikuwa na kuwinda ndege, wee kwale na njiwa pori.

Afu jorowe na kiramaua walikuwa watamu.

Dodolima eti walikuwa hawaliwi hasara.

Kuna ile ya mdako................Weweeee.............
 
Mdako ndio msita.

Afu kulikuwa na kuwinda ndege, wee kwale na njiwa pori.

Afu jorowe na kiramaua walikuwa watamu.

Dodolima eti walikuwa hawaliwi hasara.
Kongosho umenikumbusha mbali Dodolima na Jorowe
 
Nimefanya vyote, ila mbwa sijafuga na wala sijasukuma baiskeli ya kiwete, game nilikuwa natatazama viwanja vya Chumvini.
 
kuna dizaini tulikuwa tunatengeneza mbao na bearings kama baskeli ya kusukuma chini.

Ila mnasukumana sehemu ambazo hazina mchanga.

Kulikuwa na kuendesha maringi.

Au kugongesha mabetri (al maarufu kupunana) na kamari ya visoda.

Bado gololi lol

Pia kukodisha baiskeli na kuandika kwenye ukuta wa mzee said
 
kuna dizaini tulikuwa tunatengeneza mbao na bearings kama baskeli ya kusukuma chini.

Ila mnasukumana sehemu ambazo hazina mchanga.

Kulikuwa na kuendesha maringi.

Au kugongesha mabetri (al maarufu kupunana) na kamari ya visoda.

Bado gololi lol
Kuendesha maringi lol nimeendesha sana aiseee
 
Back
Top Bottom