Hatutayumbishwa na mapandikizi ya kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatutayumbishwa na mapandikizi ya kisiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, May 28, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kamwe hakitakubali kuyumbishwa na kikundi chochote au watu wanaojiunga nacho kama mapandikizi kwa lengo la kuleta mageuzi ili kukidhoofisha chama hicho kisiasa.

  Mwenyekiti wa cha hicho Taifa, Freeman Mbowe ametoa kauli hiyo jana wakati akihutubia umati wa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani waliohudhuria kwenye mkutano mkubwa uliofanyika kwenye viwanja vya Jangwani jijini hapa.

  Mbowe alilazimika kutoa kauli hiyo baada ya kila mara kukatizwa hotuba yake na wananchi ambao walikuwa wakimshinikiza amng'oe Mbunge wa Maswa (Chadema), John Shibuda wakidai ni mmoja wa wanachama ambao wanaweza kuwa ni mapandikizi.

  Ingawa Mbowe hakumtaja mtu aliyekuwa akimlenga, lakini umati huo wa watu ulipiga makelele na kusema " Shibuda huyoo….Shibuda huyooo, mng'oeeee,".

  "Sikuja hapa kumng'oa mtu
  , naomba utulivu nitoe kauli ya chama, chama chetu ni chama makini sana hakitayumbishwa na propaganda za mtu yeyote atakayekuwa pandikizi, tunafanya kazi kupitia vikao vya chama, kwanza mtu mwenyewe ni mwepesi mno,"alisema Mbowe huku akishangiliwa na mamia ya wananchi.

  Source: Nipashe.
   
Loading...