Hatutaki kusikia wabunge watuhumiwa wala rushwa kuongoza kamati za bunge.

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Ukishatuhumiwa kua mla rushwa ukakamatwa na TAKUKURU na kupelekwa mahakamani wewe ni fisadi, mwizi na mla rushwa tu!

Ndungai tafadhali tengua utezi wa Richard Ndasa na Kangi Lugola! Nina imani TAKUKURU hua hawakurupuki, walijiridhisha mpaka kuwakamata watuhumiwa hao wala rushwa. Wanatuharibia kasi ya Rais Magufuli! Usionee huruma tupilia mbali hao hawafai.

Mbunge mzima kukamatwa na TAKUKURU kwa tuhuma za rushwa si bure! Wanalichafua bunge ikiwezekana Wananchi wao wawakatae. Hatutaki kuwasisikia, wengine wanajifanya wazalendo hakuna kitu ni walafi tu
 
Mtu gani muadilifu kabisa anaweza kugombea ubunge siku hizi! Wengi watumishi wa umma fisadi na wafanya biashara wakubwa ndio wenye hiyo hela ya kugombea ubunge. Yafaa umma kwa umoja wao kuhakikisha wabunge wala rushwa hawakwepi mkono wa sheria ili wafungwe jela na wananchi kupewa fulsa ya kuchagua mtu mwenye heshima kuwawakilisha bungeni.
 
Back
Top Bottom