Wajumbe kamati za bunge zinazoongozwa na watuhumiwa wa ufisadi na rushwa kwanini msijiuzulu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wajumbe kamati za bunge zinazoongozwa na watuhumiwa wa ufisadi na rushwa kwanini msijiuzulu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Aug 7, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,035
  Likes Received: 37,814
  Trophy Points: 280
  Hili bunge letu limeundwa na wabunge wengi wasaio na uzalendo kabisa.Hivi kweli inaingia akilini kwa bunge zima kuridhia watu ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi na rushwa kupewe uenyekiti wa kamati za bunge?Watu hawa licha ya kutokustahili hata uenyekiti wa kamati hizo hawakustahili kuendelea kuwa wabunge katika bunge hili.Hivi nikisema kuliita hili bunge kuwa ni bunge tukufu ni unafiki mkubwa na tusi kwa watanzania nitakuwa nakosea?Bunge tukufu linaweza kuundwa na watuhumiwa wa ufisadi na rushwa?Mahakama ndio chombo pekee ambacho kingeweza kuwasafisha ila maadam hawakufikishwa mahakamani bado watanzania wengi hatuna imani na uadilifu wao.

  Kama kweli wabunge wetu wana uzalendo hasa wale ambao ni wajumbe wa kamati zinazoongozwa na watuhumiwa hawa nafikiri iatakuwa ni hatua sahihi kwa wao kujiuzulu nafasi zao ikiwa ni kuonyesha kupinga wao kuungozwa na watuhumiwa wa kashifa hizi kwani ni fedheha na aibu kwao.Ingawa watakuwa wamechelew ila ni bora wakafanya uamuzi huu kuliko kutokufanya kabisa.

  Watu hawa hata kwenye chama chao kulikuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari zikidai kuwa wanatakiwa wajiuzulu nafasi zao ndani ya chama maarufu kama kujivua gamba.Sasa watu hawa kama hata kwenye chama chao walitakiwa kujiuzuli wanapata wapi uhalali wa kuwa wawakilishi wa wananchi ndani ya bunge kwa ticket ya chama kile kile kilichowataka wajiuzulu kwa tuhuma za rushwa na ufisadi?Hivi kijivua gamba ilikuwa na danganya toto?Nani mpaka leo hii amewajibishwa chini ya falsafa feki hii ya kujivua gamba?

  Mwisho tukumbuke ni bunge hili hili ndio lilitoa maazimio ya kutaka wahusika katika kashifa hizi wawajibishwe.Sasa kukubali watuhumiwa ambao walihusika ktk kashifa kupewa nafasi za uongozi maana yake ni nini kama sio hadaa na usanii mtupu kwa watanzania?
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Unaongelea Lowasa, Chenge na Zitto? Hao wameukamata vilivyo muhimili huu wa Dola. Walianza kwa kumdondosha Sitta kwenye Uspika. Wakamtaka abadili jinsia yake ili aendelee kuwa Spika. Akashindwa kwa kuwa yeye sio Mungu. Akaishia kutupwa kule kwenye mhimili mwingine walikotimuliwa mafisadi hawa.
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Maombi yake hayakupokelewa na Mungu kwa sababu na yeye Sitta sio msafi kihivyo.... Mungu hashindwi kubadilisha jinsia
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Hapo sasa!!! Mafisadi ndio wamekabiziwa bank walinde fedha!! Mlinzi Mwizi Mweka hazina Mwizi Muasibu mwizi hapo sasa!!
   
 5. m

  makelemo JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunakandamizwa na kudhalilishwa na kundi la watu wachache ambalo linajiona lina hati miliki na nchi hii. Hawa watu ndio wanaokipaka matope chama cha mapinduzi, chama kwa sasa kinabaki na watu waroho wa madaraka na wenye kutaka kujipatia mali kwa njia zisizo sahihi. Watu makini hawataki tena kutokana na kushindwa kuchukua hatua kwa wanachama wake wenye tuhuma kubwa za rushwa harafu serikali inatoa majibu mepesi.
   
 6. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  baadhi ya watu humu JF ni wasema hovyo bila ushahidi, LOWASA sio mwizi ni kiongozi imara amabye JK kamtoa kafara
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Lowasa ni wa kutolewa kafara na JK! Lowasa sio mwizi. Alishavuka kiwango hicho. Wezi wako Tandale kwa Mtogole!
   
 8. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Bungeni kutamu jamani na hasa kwenye kamati! Sikia tu.
   
 9. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,035
  Likes Received: 37,814
  Trophy Points: 280
  Angekuwa mzalendo angejiuzulu mwenyewe na si kusubiri mpaka mambo yawe hadharani.Ukioana bosi wako anakiuka sheria na ashauriki kwa mwanasisa makini dawa ni kijiuzulu.Hapa bongo kuna anaefanya hivyo?Kila siku wanalia kutolewa kafara na hawabadiliki sasa na wao kwanini wasihusishwe?
   
 10. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #10
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,994
  Likes Received: 6,773
  Trophy Points: 280
  Ni dhahiri sasa kuwa mafisadi wameiteka nchi, si umeona jinsi Membe alivyoshindwa kibarua cha kuwashughulikia na kuwapeleka mahakamani watuhumiwa wa rada, kisa mmojawao ndiyo huyo amekabidhiwa kuwa mwenyekiti wa kamati muhimu sana ya fedha ya bunge, ambaye sasa tutaanza kumwelewa kwa kauli yake aliyowahi kuisema hapo nyuma kuwa gamba limeishia kiunoni, LIMESHINDIKANA KUVULIKA!!!
   
 11. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  business as usual, mi naamini kama kuna dua ambazo Mwenyezi Mungu huwa anatujibu kwa adhabu badala ya huruma ni hii ya bunge letu. sijui ni kwa nini huwa linaitwa tukufu wakati ni sawa na kichaka cha kupitishia dhuluma kwa watanzania wanyonge. uwiano hapa ni mazuri 15%, mabaya na hasa uongo na wizi 85%. chini ya serikali ya wabunge wengi wa ccm hili bunge tutegemee maajabu tu katika maamuzi. jamani watanzania tujipangeni kuiondoa hii serikali ya magamba. MABADILIKO HAYAEPUKIKI kama kweli watanzania tunataka ukombozi. hebu jiulize inakuwaje mtu leo wanamwita fisadi, halafu kesho anapewa usimamizi wa fedha! hivi hii nchi haina watu wengine kweli ni hao hao tu?????????????
   
 12. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,035
  Likes Received: 37,814
  Trophy Points: 280
  Mkuu hiyo sio sababu.Tumewachoka.
   
 13. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Umewachoka wewe,huko bungeni wamechaguliwa kwa kishindo kuongoza hizo kamati. Kwa hiyo ndugu yangu usidhani hawa jamaa ni wachache. Wapo wengi sana! Kama utaendelea kuwaza kwamba ni wachache utakuwa huna tofauti na kutwanga maji ktk kinu!
   
Loading...