MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema “Rushwa ni jambo la hatari kabisa, huwezi kununua haki. Haki hainunuliwi, thamani yake ni shilingi ngapi”
Kuna habari imetoka katika gazeti la Mtanzania la leo,Tue, March 22, 2016 kuhusu wabunge wala rushwa. Repoti hii imepelekwa kwenye ofisi ya Spika baada ya kazi za uchunguzi zilizofanywa na taasisi za kiuchunguzi za serikali (TISS, TAKUKURU) katika kuchunguza mienendo ya wabunge wakati Rais Magufuli akitafuta wabunge ili awateuwe kwenye Baraza la Mawaziri.
Repoti imebainisha wabunge wengi ni wala rushwa kitu ambacho kimempelekea Spika kuwaondoa katika nyadhifa za Kamati zao na wengine kuwahamisha katika kamati zingine.
Leo Spika amelazimika kuwavua uwenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge wanaotajwa katika tuhuma hizo na kuhawamisha baadhi ya wabunge kutoka kamati moja hadi nyingine, kutokana na majina yao kutajwa na wengine kuhusishwa moja kwa moja na tuhuma za rushwa.
Hawa ni wabunge ambao wameaminiwa na wananchi na wanawategemea kuwawakilisha ili kuisimamia serikali lakini wanachofanya ni kuwa sehemu ya wala rushwa na corrupt cartel.
Kuna majina ya wabunge ambao huwezi kuamini kama ni wala rushwa. Ukimsikia Kangi Lugola bungeni unaweza kudhani ni mzalendo wa kweli kumbe ni usanii tupu.
Wabunge kama Dk. Mary Mwanjelwa, Richard Ndassa na Dk. Raphael Chegeni wana sura za kizalendo lakini ndani ya mioyo yao ni mawakala wa rushwa.
Kama hawa wabunge wanakuwa wala rushwa, nani ataisimimamia serikali?
Vita vya rushwa na ufisadi ni pevu na kwa mantiki hii, inahitaji nguvu, werevu na hekima ya kiwango cha juu katika kupambana nayo ili kuishinda.
Kwa kazi aliyonayo Rais Magufuli, sishangai kumsikia akisema, ''Mtuombee kwa Mwenyezi Mungu''. Kwa mwendo huu, ndio maana Rais Magufuli alichukua muda mrefu kupata Mawaziri mpaka akaenda kukopa wengine kwenye nafasi zake 10 za kuteua wabunge kwa mujibu wa katiba.
Hii ndio orodha ya wabunge waliobadilishwa kwenye kamati kutokana na baadhi yao kuwa na tuhuma za rushwa kutoka kwa watumishi wa taasisi za serikali na mashirika ya umma.