Hatukataa misaada, hatutaki misaada yenye masharti

Michael Chairman

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
922
583
Hayo yamesemwa na mh, Dr Ally Mohamed Shein wakati akihutubia waandishi wa habari wakati akitangaza baraza la mawaziri kumi na tatu (13) kutoka kumi na sita (16) wa serikali ya mapinduzi iliyopita.

Akieleza kuhusiana na misaada ya mataifa ya mbalimbali amesema wako tayari kupokea msaada utakaoletwa na wala hawataomba msaada lakini ukija wataupokea na hawatapokea misaada yenye masharti.

Kwa msingi huo napenda kumpongeza Dr Shein kuliona hilo kwa serikali yake hii amabayo naiona kuwa yenye nasaba na serikali ya "hapa kazi tu" ya Mh, Rais John Magufuli ambazo zote zimejinasibu kuto husudu misaada ya wahisani yenye masharti mengi.

VIVA SHEIN.
 
masharti ya kuufanya uchaguzi kuwa huru na haki? wanapenda waeleweke kuwa wao ni nchi ya kagumashi hivyo uchaguzi magimashi uruhusiwe tuu!

Waafrika tuna fuse iliyokatika vichwqmi
 
Kwa kujenga tu fikira za utayari wa kupokea msaada, inatosha kuthibitisha kuwa lipo tatizo na mhusika anahitaji msaada na hana budi kutambua kuwa hakuna msaada usiokuwa na masharti - yawe yametamkwa wazi au vinginevyo! hata ndugu zetu Wachina ambao wanakuwa wa kwanza kuunga mkono ubakaji demokrasia, masharti ya misaada yao ni kuwaruhusu wachimbe madini, mafuta, na gesi kama si kuvuna pembe zetu za ndovu!
 
acha kudanganywa na wanasiasa.midomoni watakuambia hawataki misaada yenye masharti lakini wakikutana na wafadhili wanageuka 'hewala bwana'.unadhani hiyo misaada ikikatwa itapunguza mshahara na marupurupu ya Dr Shein? thubutu.wewe mlalahoi ndie utaambiwa 'heri ule nyasi'. kalagabaho.
 
Hatukataa misaada, hatutaki misaada yenye masharti
Naona wanamodify sentensi kila mara. Walianza na "Tanzania ina uwezo wa kujitegemea", sasa tunaambiwa vingine. Nadhani wameshtukia kuwa bajeti inagoma mahali fulani, sasa wanalainisha kauli
 
acha kudanganywa na wanasiasa.midomoni watakuambia hawataki misaada yenye masharti lakini wakikutana na wafadhili wanageuka 'hewala bwana'.unadhani hiyo misaada ikikatwa itapunguza mshahara na marupurupu ya Dr Shein? thubutu.wewe mlalahoi ndie utaambiwa 'heri ule nyasi'. kalagabaho.
Wanasiasa kama wakina Dj na chama chao kubadili gia angani walituaminisha kwamba nchi hii ni tajiri haina haja ya msaaada na sasa wanalia lia tu kuhusu Mcc , hv ni nan katuroga mpaka hatuwezi yafikiria haya yote tunashabikia siasa kama mpira wa miguu , wanasiasa wetu wa upinzani Ni Wanafiki na Wazandiki wakubwa. Ni vyema wangepambana na kujenga hoja juu ya uchgz wa marudio kuliko kuongelea misaada
 
Back
Top Bottom