halafu wakimweka kibonde kwenye tangazo wajitahidi asicheke maana yale meno watoto watahisi anazungumzia kilimo kwanza sababu yapo kama majembe.
duh.! Kumbe wabongo hatuwezi eti
Kwa kweli Wtz hutujui kutengeneza matangazo ya biashara lakini nimeliangalia tangazo la Simtank ambalo limemshirikisha mchekeshaji Ramadhani Mwinshehe 'Kingwendu' kwa kweli nimelikubali pamoja na kasoro zake chache. hebu nawe sema chochote kuhusu hili au macho yangu yana makengeza!
Nitakushitaki umeiba kero yangu!LOL yaani lile tangazo huwa najiuliza wenyewe wakikaa wanafikiri nini? na hujui kama wanatangaza godoro au kingine !ukiangalia lile la Vita Foam hutakaa ununue hilo godoro milele. linatapisha
tangazo ni lile la zantel epic nation bana......hawa wengine wanachekesha tu
Ebana lile la Hallow Mpenzi ndio tupo Kona ya Mwisho hapa! hivi bado lipo Sijatizama kitambo Local Channel.
Me matangazo niliyokuwa nayapenda :-
1.La ITV--- Hebu Tueleze Siri ya Mafanikio Yako... Mtoto wa Kiiraqw anajibu Sio Siri Ni Revola tu Jamaa anauliza Revola Peke Yake? cute anajibu ''Ndio Kwani Mwasho ni Laini na Huniweka Fresh Mchana Kutwa...
2.Lile la Salama Condom... japo si lilikuwa ni la Kenya au Tz? Salama changuo la kisasa!!!!!! Mpya bora kwa bei nafuuu..!!!!
Hivi kuna anae likumbuka la Ntindilititindilo Cafenol ni Bora haina asprin peke yake, hupunguza maumivu ya kichwa homa mafua na Fluu, Cafenol ni dawa bora hushinda Maumivu.. imeshinda zingine zote, Cafenol ni dawa namba One Cafenol Cafenol bambaaa!
Kuna La Relova Revola Revola Revola.....revooola ah Sabuni Mpya
Haha hilo pia nalikumbuka hadi midundo yake oina lile la kiwi... Heeeebuu jitoookeeeeze, simaaaama,..jioonyesheeee... Mbele za watuuuuu...
mie nalichukia lile la Aietel Wamekata sipendi hata kulisikia
hahaha hili na lile la unatoa wapo meeni nilikuw nayapenda, Rip sharo.''Kule hakusomeki Meeen!..............NIMEHAMIA!'' hahahahahahahahahahahaaaaa!
halafu wakimweka kibonde kwenye tangazo wajitahidi asicheke maana yale meno watoto watahisi anazungumzia kilimo kwanza sababu yapo kama majembe.
kuna la protex la zamani kweli, We omari, Kazi kujikuna tu ngwaara ngwara, em peleka chai. then omari anadondosha vyombo. bosi anamaind "Omariii"
Na yale ya fanta ya zamani. kuna mshkaji anaitwa Fred, msanii kweli.