Hatujifunzi na hizi ajali na maafa makubwa? Sisi ni kenge, hadi tuone damu masikioni ndio tusikie maumivu?

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Hatujifunzi, hatujifunzi na hizi ajali na maafa makubwa? Sisi ni kenge? Hadi tuone damu masikioni ndio tusikie maumivu?

Kama kweli serikali hii ingelikuwa sikivu, ingelisikiliza Hoja za mbunge wa Ukerewe (CHADEMA) Joseph Mkundi wakati akiomba kivuko cha Ukerewe ~ Ukara, aliomba hadi kusikia kauli ya serikali.

Nafikiri kilichomponza ni yeye kuwa mbunge wa CHADEMA, hawakumsikia. Alitahadhirisha uchakavu wa kivuko hicho. Akisema watakuja kuomba rambirambi bungeni, kweli kimezama, na watu wamepoteza maisha.

Wakati serikali hii ikitumia Pesa nyingi sana kununua ndege na kujenga miradi mikubwa kwa fedha za nje za kukopa kwa Riba, imeshindwa kutambua umuhimu wa kulinda usalama wa raia na mali zao. Imewekeza kwenye 'vitu' kuliko 'watu'

Niwaulize tu enyi wafuasi wa CCM; Huo muda ambao mnatumia kusema "MBOWE OUT" kwanini msingeutumia kumshauri JIWE afanye kitu kwenye kitengo cha maafa ofisi ya waziri mkuu? Yaani waokoaji wanatumia mitumbwi karne ya 21?

.kweli hata baada ya teknolojia kuwa kubwa, ulimwengu kupiga hatua, Tanzania imekosa vifaa vya uokoaji? Kwamba Mkuu wa mkoa wa Mwanza anatoa amri ya kuhairisha uokoaji wa majeruhi na uopoaji marehemu kisa "GIZA?" hivyo tusubiri 'JUA' litokeze?

Ajali nyingine zinazuilika. Hii ni ajali ya kizembe. Mbunge ameomba sana kuletewa kivuko kingine au kurekebisha kilichopo, ameomba hadi kauli ya serikali bungeni. Serikali ikaweka Pamba masikioni. Kwamba mmeshindwa kuokoa watu 150M away from the land? Hakuna 'service occurrence boats?' Kazi yenu kununua madiwani tu..

Ajali ya Mv Spice Islander (Nungwi) mwaka 2011 hawa TBC walikuwa wanaonesha Taarabu huku wengine wa~kicover `story` ya ajali. Ajali hii ya Mwanza Millard Ayo walikuwa Live wakati TBC wapo bize na safari ya Dodoma. Miaka 22 baada ya ajali ya MV Bukoba yanatokea yale~yale

Nchi yetu bado ipo kwenye rehearsal! Hatujawa serious bado! Halafu kuna 'defenders of the weaknesses' ndio kisanga.. Nchi ina tatizo pia la 'Passanger Manifest' tangu 2011 ajali ya Nungwi, hatujui idadi kamili ya watu waliopoteza maisha. Hata hii ajali ni dana~dana tu.

Unaweza kumwaga Matusi, ukaonekana hauna maadili wakati mwingine.. Hapo baada ya muda, JIWE anakwenda Ukerewe, bila kutambua yeye ni 'comforter in chief' anawaambia wafiwa "SIJALETA MIMI HUYO AJALI, AJALI SIO YANGU, TUFANYE KAZI"

They never learn from their mistakes; Diving suit ni kama $40; Headlamps ni kama $10; Vifaa vingine pia vinaweza pelekea hadi $100; Hiyo pesa HAKUNA kwenye ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa [PMNRF~Prime Minister's National Relief Fund]

Nimezidi kupata sababu ya kuwachukia wakoloni hawa; Watu wanapata ajali 150M away from the land, wanazama kwenye maji, saa saba mchana, wajinga wanahairisha uopoaji na uokoaji kwenye ajali hadi kesho tena. Kweli? Hii serikali yenu mufilisi. Kazi kununua 'mindege' tu.

Wajinga wamesitisha uokoaji sababu ya giza. Yaani wamekwenda kulala. Afadhali hata wangebaki Eneo la tukio na 'tochi' zao. Kwamba waliokuwa hai waendelee kusubiri 'pakuche' waokolewe? Hii nchi alieturoga alikua na mtu katili sana..

Mkuu wa mkoa, RPC, mkuu kamandi ya JWTZ, yaani mmepata kabisa usingizi baada ya kuhairisha zoezi la uokoaji na uopoaji sababu ya giza? Au kwa sababu kwenye kivuko hakuna dada, kaka, wake na watoto wenu? Kungelikuwa na "Jesca" humo ndani zoezi lingesimamishwa kweli hadi 'pakuche?'

Unakwenda kulala, unapata usingizi, wakati kuna 'mamia' ya watanzania unaowahudumia wapo ndani ya maji? Wewe mkuu wa mkoa, Mkuu wa bandari, Msimamizi wa bandari, hamtakiwi hata kwa kuelekezwa cha kufanywa, hamtakiwi kuwa ofisini. Kwetu kule Korea Kaskazini tungelijua cha kuwafanya.

Kwamba raia wamelala kwenye maji Ziwani, wakisuburi uokoaji Jua likiwaka? Yaani kama kuna mwamba alikuwa hai, amesubiri, ametulia kwenye maji hadi Jua limewaka maana hakuna Mwanga wa kumulika... SHUBAAMITI, Crooked country!

Kazi ya mfuko wa maafa? Idara ina kazi gani?

Tangu wakati wa MV Spice, baadae mafuriko na Tetemeko, ipi kazi ya Prime Minister's National Relief Fund ~ PMNRF? Tanzania has developed a National Disaster Policy; The document was approved by the GoT in April, 2004.

There is a standing Legislation which was enacted 1990 to deal with relief referred to as 'The Disaster Relief Coordination Act, 1990'. A draft Legislation to amend the 1990 has been prepared, so that it covers all aspects of disaster mitigation, preparedness, response and recovery

Pamoja na kwamba ni jambo jema sana kuwachangia wahanga wa matukio kama haya (Mfano Kagera), lakini ni wazi tumedhihirisha hatuna 'Disaster Preparedness strategy' kabisaa katika nchi yetu. Nchi ina kitengo cha kushughulikia masuala kama haya, tena kitengo kipo kisheria...

Ni hatari sana kusubiri janga litokee ndio tuanze kuchangishana fedha na kupambana na janga, michango inapaswa kuwa nyongeza tu sio tegemezi. (serikali ilipaswa kuwa na mfuko wa kushughulikia matukio na majanga kama haya).

Tunapaswa kujifunza sana kupitia _*The United States President's Emergency Plan for AIDS Relief*_.. (tunapaswa kujifunza upya masuala haya ya _*Disaster and risk management circle*_, kama taifa tuko _shallow indeed_

Mfano kule kwenye tetemeko la ardhi Kagera, Kitengo cha maafa kilipaswa kuwa kimeanza kuwajibika tangu siku ya kwanza.. (hivi.. Kitengo hiki cha maafa hakitengewi bajeti kabisaa!!?)

Kila siku nasisitiza, ile idara ya uratibu wa maafa chini ya ofisi ya waziri mkuu, ifanywe kuwa wakala, ili ipate uwezo wa kutengewa fedha, iwe taasisi inayojitegemea, iweze kushughulikia matatizo kama haya mara tu yanapotokea.

Unaweza kumwaga Matusi, ukaonekana hauna maadili.. Hapo baada ya muda, JIWE anakwenda Ukerewe Kwenye mkutano wa hadhara, bila kutambua yeye ni 'comforter in chief' anawaambia wafiwa "SIJALETA MIMI HIYO AJALI, AJALI SIO YANGU, TUFANYE KAZI"

Mnasubiri kutuomba 'rambirambi' halafu 'mzitakase' kama za Mafuriko. SHUBAAMITI! Hatuchangiii.

#MMM, Martin Maranja Masese
 
Niwaulize tu enyi wafuasi wa CCM; Huo muda ambao mnatumia kusema "MBOWE OUT" kwanini msingeutumia kumshauri JIWE afanye kitu kwenye kitengo cha maafa ofisi ya waziri mkuu? Yaani waokoaji wanatumia mitumbwi karne ya 21?
 
This is more common than it should be, and not just with ferries. Please help raise awareness for the safety standards of all forms of transportation in Tanzania. We can do better.
 
sio vema kuanza kulaumu now ila nimekuelewa mtoa uzi maana uchungu uliokuwa nao ndio umepelekea huko;ni AIBU eti uokoaji unasitishwa sababu kubwa ni giza ....common baada ya miaka zaidi ya 50 ya kujitawala bado giza ni kikwazo katika uokoaji,wangesema hali ya hewa hairuhusu labda tungeeleweka but sio sababu hii ya kitoto;ziwa hili lina historia nyingi tu za ajali je tunajifunza nini?je ripoti ya MV Bukoba (iliyouwa zaidi ya watanzania 1000)ilitoka?je kuna yeyote aliyewajibika na ajali ile?nini tulikirekebisha kuona ajali kama ile haitokei tena,?AIBU kuona mashirika makubwa ya habari yanaonyesha uokoaji unavyofanyika kwa kutumia mitumbwi!!,kikosi maji cha polisi au jeshi vipo wapi?ni kweli mtoa hoja tunatumia pesa nyingi mno kwa vitu tusivyohitaji now wakati vitu vya msingi tunavyipuuzia because tuwa waoga wa to take serikali to task.
 
MBUNGE UKEREWE ‘ALITABIRI’ AJALI YA MV NYERERE


UNAWEZA kusema ni kama alitabiri ajali ya MV Nyerere iliyotokea jana katika ziwa Victoria, ni kutokana na Mbunge wa Ukerewe (CHADEMA), Joseph Mkundi ambaye mnamo Aprili 24, 2018 (takribani miezi mitano) iliyopita alisimama Bungeni jijini Dodoma na kumuuliza swali aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wakati huo, Prof. Makame Mbarawa kuhusu ni lini Serikali itafanya ukarabati wa MV Nyerere ambayo alidai mashine zake zilikuwa na hitirafu.

“Kuna kivuko kinachounganisha kati ya Kisiwa cha Ukara na Ukerewe, kina hudumia zaidi ya wananchi 50,000, kimekuwa kikileta shida mara kwa mara, nimekuwa nikiwasiliana na wizara mara kwa mara, hatupendi kuja kuomba rambirambi kwa sababu ya wananchi kuzama kwenye kivuko kile.

“Tangu mwaka jana tuliahidiwa kwamba mpaka Desemba mashine mbili ambazo zilikuwa zimeagizwa zingekuwa zimeshafungwa lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea. Niombe kauli ya serikali, ni lini mashine hizo zitafungwa ili kivuko hicho kitoe huduma katika mazingira ya usalama.

Aidha, zoezi la uokoaji wa abiria waliokuwemo katika kivuko cha MV Nyerere kilichozama lilisitishwa jana usiku kutokana na giza na litaendelea tena leo ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela amesema mpaka sasa watu waliookolewa wakiwa hai ni 37 na waliopoteza maisha ni 44.
%E2%80%AA%2B255%20676%20870%20787%E2%80%AC%2020180921_093446.jpg
 
Yani mambo yanayoongelewa mbungen huwa kwa asilimia kubwa yanaachwa mlemle mjengon huwa hakuna ufuatiliaji wowote kwa sababu kama ajenda zote zingekuwa zinafuatiliwa kulingana na kero iliyowasilishwa na mb tungekuwa mbali sanaaa.
Yan hata hakuna haja ya kupeleka wawakilishi bungen
 
MBUNGE UKEREWE ‘ALITABIRI’ AJALI YA MV NYERERE


UNAWEZA kusema ni kama alitabiri ajali ya MV Nyerere iliyotokea jana katika ziwa Victoria, ni kutokana na Mbunge wa Ukerewe (CHADEMA), Joseph Mkundi ambaye mnamo Aprili 24, 2018 (takribani miezi mitano) iliyopita alisimama Bungeni jijini Dodoma na kumuuliza swali aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wakati huo, Prof. Makame Mbarawa kuhusu ni lini Serikali itafanya ukarabati wa MV Nyerere ambayo alidai mashine zake zilikuwa na hitirafu.

“Kuna kivuko kinachounganisha kati ya Kisiwa cha Ukara na Ukerewe, kina hudumia zaidi ya wananchi 50,000, kimekuwa kikileta shida mara kwa mara, nimekuwa nikiwasiliana na wizara mara kwa mara, hatupendi kuja kuomba rambirambi kwa sababu ya wananchi kuzama kwenye kivuko kile.

“Tangu mwaka jana tuliahidiwa kwamba mpaka Desemba mashine mbili ambazo zilikuwa zimeagizwa zingekuwa zimeshafungwa lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea. Niombe kauli ya serikali, ni lini mashine hizo zitafungwa ili kivuko hicho kitoe huduma katika mazingira ya usalama.

Aidha, zoezi la uokoaji wa abiria waliokuwemo katika kivuko cha MV Nyerere kilichozama lilisitishwa jana usiku kutokana na giza na litaendelea tena leo ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela amesema mpaka sasa watu waliookolewa wakiwa hai ni 37 na waliopoteza maisha ni 44.View attachment 873003

Mungu mbariki Mh Mbunge
 
Back
Top Bottom