The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 836
Rais wa Kenya, William Ruto, amejibu hatua ya Marekani ya kutaka kupitia tena hadhi ya nchi yake ya mshirika mkuu asiye mwanachama wa NATO, akisema kuwa machaguo yake ya sera za masuala ya mambo ya nje yanazingatia kile ambacho kinafaa zaidi kwa Kenya.
Akizungumza na sekta za kibinafsi, Ruto alitetea ukuaji wa kibiashara na nchi kama China, akisema kuwa lengo la utawala wake ni kunufaisha wazalishaji wa Kenya na kurekebisha kile ambacho hakijakuwa sawa kwa muda mrefu.
Rais Ruto alikiri kuwa baadhi ya washirika wake wanahoji ukuaji wa kibiashara kati ya Kenya na China, lakini akasisitiza kuwa maamuzi ya hatua hizo yanashinikizwa na mahitaji ya Kenya kiuchumi.
“Baadhi ya marafiki zetu wanalalamika kwamba tunafanya biashara nyingi na China. Wakati nilikutana na Rais Xi Jinping, nilimwambia Kenya inaingiza bidhaa za Sh600 bilioni kutoka China, lakini tunasafirisha tu labda 5%. Usawa huo wa kibiashara ni mbaya,” Ruto alisema.
Ruto aliongeza kuwa China imekubali kufungua soko lake kwa bidhaa za kilimo za Kenya.
“Wamekubali kufanya mabadiliko ya usawa wa kibiashara kati ya Kenya na China. Wamekubali kuondoa ushuru wote kwa chai yetu, kahawa, parachichi, na bidhaa zote za kilimo tunazouza nje ya nchi.
Tunaendeleza mazungumzo na India. Tuna uhusiano mzuri na Uturuki na Canada,” Ruto alisema.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge juu ya Masuala ya Ulinzi nchini Kenya, Nelson Koech, amemwandikia mwenzake, Seneta wa Marekani, Jim Risch, akisema:
“...Namuomba mwenzangu wa Marekani, Seneta Jim Risch, Mwenyekiti wa Masuala ya Mambo ya Nje, kufikiria upya mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya Uidhinishaji wa Kitaifa wa Ulinzi (NDAA) ya Mwaka 2026 kwa maslahi bora ya mataifa yetu mawili ya kirafiki.
Mapitio yaliyopendekezwa na Seneta Risch, ikiwa yataidhinishwa, yatajumuisha tathmini ya sera za kigeni na za kidiplomasia za Kenya, kama vile kujifungamanisha na Marekani na ushirikiano wake na China, Urusi, na Iran, pamoja na makubaliano yanayowezekana ya Kenya, uhusiano wa kisiasa au kifedha na wanamgambo wenye silaha kama vile al-Shabaab na Rapid Support Forces (RSF), na mengineyo.”