Hatua za kumfukuza mpangaji nyumba

Futota

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
521
87
Wajameni nisaidieni nichukue hatua zipi kumtoa mpangaji wa nyumba yangu ambaye hataki kulipa ada ya pango la nyumba sasa miezi minne. Nifuate sheria zipi zakumuondoa haraka huku akiwa amelipa deni? Natanguliza shukran kwa majibu yenu
 
Sheria inasema kwamba ukitaka kusitisha mkataba wa makzi na tenant inabidi umempe info @lst miezi 2 so unachotakiwa kufanya ni kumpa notice ya miezi miwili then kwa madeni yako kama hatoweza ufanye mpango wa kuzuie fenicha tv na axesories zenye thaman na deni lako ukimtimua gafla itakula kwako!
 
Fuata utaratibu uliopo kwenye mkataba. Au hamna mkataba?[/QU hata mimi nimeshndwa kuelewa kwa sababu kama mkataba upo tumia kanuni zilizopo ndani ya mkataba ili kumuondoa hata hivyo hatua ya kwanza nenda kwa balozi wa eneo lako/lenu kupeleka mashtaka kabla hujashka mali ya mpangaji.
 
Mkataba ulikwisha siku nyingi tangu Jan na bado yupo ndani. Na ahadi yake kila mwezi ni kuwa anataka kuendelea kuishi na tuendeleze mkataba lakini ikifika kutoa hela za pango anakuja na sababu kibao na kuosogeza siku mbele, huku hana dalili ya kuhama

Fuata utaratibu uliopo kwenye mkataba. Au hamna mkataba?
 
Sawa mkuu, nitaenda kwa mjumbe wa nyumba kumi kumi. Mkataba upo, na ulikwisha tangu Jan na hadi leo analeta kiswahili cha kuendeleza mkataba mwingine kesho na hiyo kesho ndio hadi leo anakaa bure.

Fuata utaratibu uliopo kwenye mkataba. Au hamna mkataba?[/QU hata mimi nimeshndwa kuelewa kwa sababu kama mkataba upo tumia kanuni zilizopo ndani ya mkataba ili kumuondoa hata hivyo hatua ya kwanza nenda kwa balozi wa eneo lako/lenu kupeleka mashtaka kabla hujashka mali ya mpangaji.
 
Sasa basi ikiwa baada ya kuongea na uongozi wa mtaa/ nyumba kumi kumi, na jamaa akiendelea kuwa king'ang'anizi kukaa bila kulipa rent. Nifanyeje hatua ifuatayo?
 
Kama mkataba uliisha mpe notice ya mwezi mmoja na baada ya mwezi kuisha unaweza kumtoa kutoka kwenye nyumba. Hii ni kwa sababu muda wa kulipa kodi ni mwezi mwezi. Pia umfungulie kesi kwa ajili ya recover rent.
 
mkataba wenu unasemaje kuhusu kufikia ukomo wake? mnamakubaliono gani hadi awepo kwenye nyumba hadi leo?
 
Mkataba wake ulishaisha tangu January, na kama ukihesabu notice ya mwezi mmoja basi inakuwa February ni mwisho. Alipewa notice na akaahidi kuwa angependa ku renew contract yake. Sasa baada ya hapo ndio imekuwa neno la njoo kesho njoo kesho, hana contract, hivyo anakaa bure na hataki kuhama. sasa basi tumechoka na tumeshamwambia aahame, lakini ndio hadi leo bado yupo kwenye nyumba. Tatizo hili tumelifikisha hata kwa serikali ya mtaa na walifika kuongea naye, na akaahidi kuhama na asihame. Sasa basi nichukue hatua gani zaidi niweze kumwamisha?
ASANTENI!
Asanteni

Kama mkataba uliisha mpe notice ya mwezi mmoja na baada ya mwezi kuisha unaweza kumtoa kutoka kwenye nyumba. Hii ni kwa sababu muda wa kulipa kodi ni mwezi mwezi. Pia umfungulie kesi kwa ajili ya recover rent.
 
Serikali ya mtaa walipaswa wakupe barua ya kwenda Polisi ili waje wamtoe, RUDI HUKO SERIAKLI YA MTAA WAKUPE BARUA UENDE POLISI ILI WAJE HAPO WAMTOE
NILIISHAFANYIWA HIVYO SIKU MOJA NA NIKAFANIKIWA
 
Sawa Mkuu,
Hivi sasa hivi nakwenda serikali za mtaa.

Serikali ya mtaa walipaswa wakupe barua ya kwenda Polisi ili waje wamtoe, RUDI HUKO SERIAKLI YA MTAA WAKUPE BARUA UENDE POLISI ILI WAJE HAPO WAMTOE
NILIISHAFANYIWA HIVYO SIKU MOJA NA NIKAFANIKIWA
 
Hilo ndio tatizo la mikataba inayotengenezwa vichochoroni,sio kila anaejua kuandika anaweza kuandika mkataba, unakuta umkataba una mapungufu kibao na watu wanasaini tu,ukitokea mgogoro ndipo inapokuwa balaa maana wewe mwenye nyumba unajikuta umefungwa mikono na mkataba uliosaini wewe mwenyewe.
 
Acha ubahiri. Nenda kwa wakili aliye karibu nawe akuandalie namna bora ya kudai haki zako ikiwa ni pamoja na haki ya kupata nyumba yako. It is high time watanzania muachane na hii biashara ya kupitia kwa wajumbe wa nyumba kumikumi ambao si wataalamu wa sheria. Huku JF kuna mawakili wa kutosha ambao kwa gharama ndogo sana watakusaidia kudai haki yako kitaalamu zaidi. Pia siku nyingine ukipangisha nenda kaingie mkataba kwa wakili ili akuandalie mkataba utakaotoa taratibu za kumtoa mpangaji. Ukiwa na nyumba usifanye maisha yako yawe cheap. Seek quality service.
 
  • Thanks
Reactions: mka
Sawa mkuu ushauri umefika, nadhani ingepunguza upungufu huu naoupata sasa

Acha ubahiri. Nenda kwa wakili aliye karibu nawe akuandalie namna bora ya kudai haki zako ikiwa ni pamoja na haki ya kupata nyumba yako. It is high time watanzania muachane na hii biashara ya kupitia kwa wajumbe wa nyumba kumikumi ambao si wataalamu wa sheria. Huku JF kuna mawakili wa kutosha ambao kwa gharama ndogo sana watakusaidia kudai haki yako kitaalamu zaidi. Pia siku nyingine ukipangisha nenda kaingie mkataba kwa wakili ili akuandalie mkataba utakaotoa taratibu za kumtoa mpangaji. Ukiwa na nyumba usifanye maisha yako yawe cheap. Seek quality service.
 
Sheria inasema kwamba ukitaka kusitisha mkataba wa makzi na tenant inabidi umempe info @lst miezi 2 so unachotakiwa kufanya ni kumpa notice ya miezi miwili then kwa madeni yako kama hatoweza ufanye mpango wa kuzuie fenicha tv na axesories zenye thaman na deni lako ukimtimua gafla itakula kwako!
Notice inategemea na mkataba unasemaje, kama mkataba upo kimya sheria ya Ardhi sura ya 113 inataja kuwa notice inaweza kuwa sawa na kipindi cha ulipaji wa kodi mfano mwezi mmoja kama kodi huwa inalipwa kwa mwezi mwezi.
 
Back
Top Bottom