Pan-Africanist
Member
- Feb 12, 2020
- 12
- 6
Mara zote ukitaka mabadiliko lazima uonyeshe uwezo mkubwa na wakuaminika bila kupingwa na zaidi ya asilimia hamsini ya watu unaoishi nao. Binafsi napenda sana kusikia mawazo ya watu hasa kuwapatia uhuru wa kueleza mitazamo wao na malengo yao.
Kitu ambacho WaTanzania tunakosa ili kufanya mambo yetu yaende kwa weredi ni kusahau historia yetu, hata kama tukio limeshatokea miaka si zaidi ya kumi iliyopita. Mara zote mtu ambaye hajui historia yake halisi iwe kisiasa, kijamii, kidini na kiuchumi huyo ni mtu tu mpumbavu ambaye anatembea bila kujua anakotoka wala anakoelekea. Kitu ambacho unatakiwa kujiuliza ni kwamba UPINZANI Katika nchi hii ni watu tu wanaotembea hawajui historia yao. Hii inasababisha kukosa mvuto na idadi kubwa ya watu waliokuwa wanazidi kuongezeka tokea kipindi cha Dr. Slaa.
CCM wameimarika sana kisiasa na wamejizolea umaarufu kila kukicha hii ni kwa sababu ya historia yao kutosahaulika na misingi yao kuwa imara zaidi. Hii inasababisha wawe na weredi katika kazi zao na mambo yao kiujumla.
Sisi kama waTanzania, licha ya kuwa na vyama vingi kitu tunatakiwa kukifahamu nikwamba tunahitaji maendeleo. Tunahitaji taifa lenye nguvu kisiasa na Kiuchumi, tunahitaji kutengeneza taifa lenye mfano barani Africa. Vyama vingi visiwe kikwazo kwetu vya kimaendeleo. Tukumbuke kuwa Uzalendo wa chama fulani cha siasa unaokufanya usione maendeleo hata ya wazi yanayofanywa na vyama vingine hugeuka na kuwa utumwa wa fikra, lakini pia kuwa mzalendo na chama chako ukashindwa kuona hata makosa ya wazi ndani ya chama chako hugeuka na kuwa utumwa na upumbavu kifikra.
Kwa hiyo basi, tarehe 28/10/2020 tukapige kura tukachague kiongozi mwenye maono na maslahi mapana ya taifa hili. Kiongozi atakayeishangaza dunia kwa maendeleo ndani ya taifa letu, Kiongozi shupavu atakayetetea Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kiongozi atakayetoa uelekeo sahihi wa taifa hili, Kiongozi atakayelinda maliasili zetu, misitu yetu, wanyama wetu, madini yetu, na ardhi yetu. Tuache kufanya maamuzi kwa hisia tuhusishe akili na ufahamu wote kabisa.
Nchi hii na Afrika kwa ujumla ni tajiri sana, changamoto iliyopo ni kuwa hatujawahi na hata kama tumewahi ni mara chache sana kupata Viongozi halisi (Viongozi waAfrika na weusi), mara nyingi tumekuwa na Viongozi wenye ngozi nyeusi lakini ndani ni watu weupe (Caucasian).
Kwa hiyo Tanzania na Afrika kwanza (Uzalendo), mambo mengine baadae.